Jambo gani lililowahi kukufanya ujisikie aibu/Ujivunie Utanzania wako?

Jambo gani lililowahi kukufanya ujisikie aibu/Ujivunie Utanzania wako?

Fedheha na aibu nyingine ni Mtanzania mtoa mada asiyejua kuandika AIBU, yeye anaandika HAIBU. Huko Zambia na Malawi nadhani alijinadi anajua Kiswahili vizuri.
🤗🤣🤣🤣😂
Well hapo ni auto-correct ndiyo imeniferisha bila mie kujua mkuu....
 
Wahutu na Watusi lugha yao ni moja Kinyarwanda. Hakuna lugha inayoitwa ya kabila la Kitusi au ya Kuhutu.

Labda useme walikuwa wanaongeleshana kwa kuangalia urefu wa pua, wembamba wa miili na urefu wa kimo
Huyu jamaa amebuni tu haya aliyoandika. Halafu ana chembe chembe za uchawa!
 
Nilifika msumbiji,
1. simba na yanga zinashangiliwa na jezi wanavaa
2. Kiswahili safi kinaongelewa kama bongo
3. Bongofleva inapigwa kila sehemu
4. Wanaangalia channel za tv za kibongo na favourite yao ilikuwa ETV ya majizo
5. Wanaamini bongo ni nchi yenye maendeleo makubwa kama South Africa
6. Mwamposa ndo mtumishi anaeminika sana kule kiasi kwamba ndoto za wakristo wengi ni kufika kawe siku moja
7. Wanaamini kila mbongo hachelewi kukutapeli akijua ni wakuja hasa kutoka nchumbiji
 
Kiongozi mmoja kusema kuwa jina la Tume ya Uchaguzi litabadilishwa kuwa Tume Huru ya Uchaguzi eti itaifanya tume husika kuwa huru... Niliona aibu miye
Ni sawa na mbwa umuite simba
Mbwa ni mbwa tu.
 
Kutojua kiingereza , oya kuna wana nchi angalau wanatema yai sio mchezo !!

Hii mibroken inanikosesha vitu vingi jamani 😆😆😆
 
Nilifika msumbiji,
1. simba na yanga zinashangiliwa na jezi wanavaa
2. Kiswahili safi kinaongelewa kama bongo
3. Bongofleva inapigwa kila sehemu
4. Wanaangalia channel za tv za kibongo na favourite yao ilikuwa ETV ya majizo
5. Wanaamini bongo ni nchi yenye maendeleo makubwa kama South Africa
6. Mwamposa ndo mtumishi anaeminika sana kule kiasi kwamba ndoto za wakristo wengi ni kufika kawe siku moja
7. Wanaamini kila mbongo hachelewi kukutapeli akijua ni wakuja hasa kutoka nchumbiji
Hiyo namba 7,,
Yani Bongo ndiyo kama Nigeria ya nchi za SADC...
 
Niliyojivunia:

1. Nilipata safari ya kikazi mkoani Kagera wilaya ya Ngara. Kwenye lile basi raia wengi walikuwa ni wa Rwanda na Burundi. Wakati nipo kwenye basi, nilishuhudia wale jamaa walikuwa wakiongea kwa kuangaliana makabila tu, yaani Mhutu kwa Mhutu au Mtutsi kwa Mtutsi hata kama wamekaa siti moja, Mhutu na Mtutsi hawaongeleshani.

2. Nilienda kikazi nchini Zambia, nyimbo za wasanii wa Bongo zinapigwa sana. Diamond, Harmonize, Rayvan ni majina maarufu.

3. Nilienda Malawi kikazi, nilipata bidhaa nyingi sana zinazotoka makampuni ya Bongo, kama vile vinywaji vya Azam na Mo. Sheli za kampuni ya Meru ni nyingi sana. Barabara za Bongo ni nzuri sana.

4. JWTZ:
  • Ilizuia mapinduzi Comoro.
  • Imesaidia kupata amani Msumbiji.
  • Ilisaidia Malawi katika mafuriko.

Ya haibu:

1. Katika safari ya Zambia, wale wajamaa ni waaminifu sana, hawana longolongo kwenye biashara. Kulikuwa na story nyingi sana za wafanyabiashara wa Zambia waliotapeliwa Bongo.

2. Mbunge fulani kusimama bungeni na kuuliza, "Kwanini Serikali imesitisha uzalishaji/usambazaji wa sarafu kama shilingi 1, shilingi 5 na 10, haioni kama watoto watakuwa hawazijui?" Cha haibu ni kuwa huyu mbunge ameshawahi kukaa ikulu kwa miaka 10, yani alipataje ubunge hutu.

3. Kiongozi mkubwa kutoa tamko la kuzuia asiyeoga kufika katikati ya Jiji la Dar. Halafu ilikuwa kipindi cha joto kali sasa.

Matukio ya haibu ni mengi...
sio haibu ni aibu
 
Vijana kutoka vijijini na kukimbilia mjini. Hii ni aibu!!

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Huwa nikicheza mechi za online za game FIFA nikifungwa sana huwa najitambulisha kama MKENYA. Siwezi kulifedhehesha taifa langu.
 
Back
Top Bottom