Veteran Sailor
JF-Expert Member
- May 28, 2025
- 2,042
- 4,416
Mimi baada ya kumaliza chuo, nikawa niko nyumbani tu sina mishe.. Yani kifupi choka mbaya hata hela ya vocha wakati mwingine nakosa.
Basi bwana, siku moja nimepanga miadi na binti wa mtaa wa pili,afu jamaa sina hata mbuni. Na sijui napata wapi.
Wakati nishakata tamaa nimefeli, mara naitwa ndani...
Bi Mkubwa: una ratiba gani leo?
Me: nipo mama sina safari.
Bi Mkubwa: jiandae basi ukamuone mjomba wako kibaha anaumwa..
Me: sawa Mama.
Basi nilivyokuwa tayari Bi mkubwa kanipa 50,ya nauli na matunda kwa mgonjwa..
Kijana nikatoka home, nafika kitaa yule binti anantext vipi tunatoka?
Dah mwanenu nna 50 tena,nikamjibu fasta tukutane sehem flani..
Basi tukakutana huko maeneo mpaka jioni. Sina hata mia narudi home hata kwa mgonjwa sijaenda.
Nafika home namuona Mama na mzee kama wanajiandaa kutoka..
Bi Mkubwa: za huko?
Me : kwema mama.
Bi Mkubwa: mgonjwa anaendeleaje?
Me: hajambo, yani yuko poa, kasema msiwe na wasiwasi kabisa.
Bi Mkubwa: sawa si tunaenda kibaha mjomba yako hali mbaya kalazwa toka jana.
Aibu aibu.