Kipindi cha ujana, nilisafiria Penzi kwa binti wa mkoa fulani, mkoa ambao niliutamani sana kuutembelea kutokana na sifa zake wanazoujaza watu.
Basi kwakuwa huyo manzi anaishi huo mkoa nikaona hapa ndio fursa ya kumaliza ndege wawili kwa jiwe moja, kidume nikakata tiketi kusafiria penzi lisilo na matumaini.
Picha linaanza nmekaribia stendi napiga simu, manzi haipokei, tuma sana meseji bado manzi haitaki kujibu, wee nikaona asinitanie nikatuma sana sms za vitisho na malalamiko lkn wapi ndio kwaanza simu ikazimwa[emoji28].
Basi matumaini ya kupata penzi yakaishia hapo, nikashuka kwa basi kinyonge sana huku nikijipa matumaini labda atapokea simu , nilikaa sana stend zaid ya saa zima kila nikipiga simu haipatikani na ikipatikana haipokelewi, ase nikaona huu upuuzi kama plan A imefeli wacha niendelee na plan B haswa ambayo ilikuwa ni kufanya utalii wa huo mkoa, usiku huo huo nikachukua usafiri huyoo Hotelini nkamalizia usingizi wangu huko na asubuhi na mapema nikaanza sasa Rutii za chocho to chocho kujionea kwa macho sifa za huo mkoa watu wanazoujaza,
Basi siku ya 2 nikageuza huku machungu ya kukosa penzi yakiwa yamekauka uku nikijipa matumaini kuwa namimi nimeshautembelea huo mkoa "X" unaotajwa sana na hamu yangu ikaishia hapo, kwa hakika ulikua ni ujinga wa aina yake yaani nilikula nauli yangu mimi mwenyewe sio mbaya[emoji28].