Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Huu ndio ukweli mchungu, ni kwamba aidha viongozi wetu(watawala) wanatuona sisi wananchi hatuna upeo wa kufikiri au viongozi wetu wana upeo mdogo wa kufikiri.
Wao ndio hupitisha bajeti za sherehe hizo kisha baadaye haohao hutengua bajeti na kuzipeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo.
Hii tabia aliianzisha Magufuli, awali tulimuunga mkono maana ile bajeti aliyoipindua na kuamuru ijenge barabara ya Morocco-Mwenge haikupita mikononi mwake. Lakini baadaye tuliendelea kumwona akivunja bajeti za sherehe zilizopangwa yeye akiwa Rais na kuamuru fedha zikafanye jambo jingine.
Mfano: Sherehe ya Uhuru 2020 aliiahirisha na kuamuru fedha zikajenge Hospitali Dodoma.
Kwani wizara ya Afya katika bajeti zake hawakuliona hili?
Rais anageuka mungu mtu halafu Watanzania wanashangilia.
Maendeleo bila mkakati?
Hapa tunajifunza kuwa viongozi wetu wana udhaifu au wanatumia udhaifu wa wananchi kujiimarisha kisiasa(kuchukua ujiko).