Jambo hili ni Udhibitisho tosha kabisa Taifa Stars bado haipo Tayari Kushindana AFCON

Jambo hili ni Udhibitisho tosha kabisa Taifa Stars bado haipo Tayari Kushindana AFCON

....haters wanna hate ballers wanna ball, it feels good say it again..
This is our turn for real no doubt and the players are making us feel so right as we move to Egypt....
..Feelin on that....
 
Ni wendawazimu tu kufikiri eti KUNA ZAMU ZA KUSHIRIK AFCON. hii akili sijui ni ya wapi? Afcon inataka maandalizi na mapambano ya dhati ya nia dhabiti na malengo mahsusi. Specific Objectives.

Sasa mnaposema NI ZAMU YETU hii kauli mbiu ya kichovu imeasisiwa na nani?kudhani kuwa kuna kupeana zamu katika kushiriki AFCON? kuwa sasa tunaanza kudai zamu yetu ili kushiriki na si kwenda kupambana?

Hatua tuliyofika tumejitakia baada ya kupoteza mechi ambayo kwa taifa letu hatukupaswa kupoteza. Leo tunajikuta tunategemea hisani ya Uganda ili kupita. Na kuanza kuwaomba kuwa ni zamu yetu.

Tulijiandaaa vipi toka mwanzo katika hili? Miaka hii bado maandalizi yetu ni ya zima moto.hatuna kikosi kinachojielewa cha Taifa Stars. Je kocha amefuatilia viwango vya wachezaji katika mechi zao kwa ukaribu?

Zamu yenu watanzania inakuja vipi? Mnataka kugeuza mpira nao kuwa siasa? Mpira ni mapambano hakuna zamu.kwa team iliyojipanga hata watazamaji wasipoenda itashinda tu.

Uganda njooni mje mcheze mpira wa kutafuta ushindi.msije dhubutu kutubeba tukaenda kuaibisha huko mbele.tupate ushindi stahili.zamu watapeana huko huko kwenye siasa kuwa sasa ni zamu yetu kula au zamu yetu kutawala.

Mpira hauna zamu. Ni mapambano uwanjani dk 90 zinaamua mshindi na si mwenye zamu. Tunataka kuona mpira wa ushindani TANZANIA VS UGANDA. hakuna kubebana.
Mkuu,umeelewa ulivyotaka wewe lakini sio kwa mtizamo waliokuja na hiyo kauli mbiu, labda ni upungufu wa ujazo wa kiswahili umepelekea hilo lakini ktk lugha ya Kiingereza kauli mbiu hiyo ingesomeka "Its Our Time" (to qualify for AFCON).Kwahiyo elewa hivyo sio hivyo unavyoelewa wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania inabidi tufanye sensa..wahamiaji wamezidi..kuna nchi kibao wameshindwa kufuzu Na mpira wanaupiga mwingi...
 
Nauliza tu, hivi hawa wasanii wa Bongo Movie wanamchango gani kwenye kamati ya kuhamasisha Taifa Stars?
 
Nauliza tu, hivi hawa wasanii wa Bongo Movie wanamchango gani kwenye kamati ya kuhamasisha Taifa Stars?
Wee ulitaka watoe mchango gani??ulitaka Wema amfundishe Bocco jinsi ya kuji position uwanjani??Bila shaka jibu ni hapana,hao wametumika kuleta hamasa ya kuishangilia Taifa Stars miongoni mwa mashabiki wao na bila shaka umejionea mwenyewe hamshahamsha la juzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom