Ni wendawazimu tu kufikiri eti KUNA ZAMU ZA KUSHIRIK AFCON. hii akili sijui ni ya wapi? Afcon inataka maandalizi na mapambano ya dhati ya nia dhabiti na malengo mahsusi. Specific Objectives.
Sasa mnaposema NI ZAMU YETU hii kauli mbiu ya kichovu imeasisiwa na nani?kudhani kuwa kuna kupeana zamu katika kushiriki AFCON? kuwa sasa tunaanza kudai zamu yetu ili kushiriki na si kwenda kupambana?
Hatua tuliyofika tumejitakia baada ya kupoteza mechi ambayo kwa taifa letu hatukupaswa kupoteza. Leo tunajikuta tunategemea hisani ya Uganda ili kupita. Na kuanza kuwaomba kuwa ni zamu yetu.
Tulijiandaaa vipi toka mwanzo katika hili? Miaka hii bado maandalizi yetu ni ya zima moto.hatuna kikosi kinachojielewa cha Taifa Stars. Je kocha amefuatilia viwango vya wachezaji katika mechi zao kwa ukaribu?
Zamu yenu watanzania inakuja vipi? Mnataka kugeuza mpira nao kuwa siasa? Mpira ni mapambano hakuna zamu.kwa team iliyojipanga hata watazamaji wasipoenda itashinda tu.
Uganda njooni mje mcheze mpira wa kutafuta ushindi.msije dhubutu kutubeba tukaenda kuaibisha huko mbele.tupate ushindi stahili.zamu watapeana huko huko kwenye siasa kuwa sasa ni zamu yetu kula au zamu yetu kutawala.
Mpira hauna zamu. Ni mapambano uwanjani dk 90 zinaamua mshindi na si mwenye zamu. Tunataka kuona mpira wa ushindani TANZANIA VS UGANDA. hakuna kubebana.