Jambo limezua Jambo.

Mkuu DC nadhani huyo 'jamaa' yuko morally wrong na amekumislead kabisa! maana hapa tunaanza kuingia kwenye issue za kwamba kwa nini watu wana have sex in the first place, kama sio kwa ajili ya recreation,?

Mkuu una hakika na hayo unayoyasema? Mbona juzi hapa walishakubaliana kuwa infidelity is here to stay?

nadhani kwa mtu mwenye kuwa na maadili hawezi kutegemewa akatae mtoto ambaye ana uhakika ni wa kwake....wanaokataa hivyo ni kwa sababu nyingine za kimaisha tu na ndio maana baadaye hurudi 'kuwatafuta' hao watoto waliowakataa in the first place!

Unawezaje kuongelea maadili wakati jamaa alikubali kuzaa na mke wa mtu? Unadhani kuna wema wa wowote aliotenda katika issue hii zaidi ya kufanya uzinzi na ex GF wake? Mkuu bado sikubaliani na wewe. Jamaa akatafute mahali pengine pa kulelea mtoto wake badala ya kumsumbua mke wake!!
 
Kwa mwendo huu sasa tutawafanya wakatili zaidi ya Hitler!!:smile-big::smile-big:
 
its true mkuu infidelity is there to stay.,....ndo maana nilicaution kuwa tusiende ndani sana kwenye suala la kwamba not every ejaculation deserves a name.

That said, siye kwenye infidelity hatukatai mtoto hata siku moja! never!

Wema aliutenda tu mkuu tena alikubaliana na mume wake kabla. na hili wala sio yeye wa kwanza..wapo tangu enzi za mababu zetu za 'kuinuliana' uzao..so wema upo tu kwamba walau kamsitiri jamaa!
 
Kwa mwendo huu sasa tutawafanya wakatili zaidi ya Hitler!!:smile-big::smile-big:

kama 'tukiwaaachia', watakuwa wakatili kweli kweli...kwa wenzetu tayari wanaionja joto ya jiwe......manake wameshatoka ule 'uanawake' wao wameuvaa 'uanaume'
 
Huko kote sina shida mkuu wangu na hata mtoto sina tatizo naye. Huyo baba (kama mama amekataa mtoto) atumie akili yake kutafuta mahali salama atakapolea mtoto wake bila kumsumbua mke wake. Kwani kuna ugumu gani hapo?

Sikubaliani na suala la kumletea mtoto dada wa watu aanze kulea (something she was never made aware of) wakati ndo baaado anasubiri wake. Tunahitaji kumshauri huyu jamaa ili asije kuhatarisha afya ya akili zake na ndoa pia! Kwa jinsi anavyolia lia na tatizo dogo la kulea mtoto, he will soon go crazy!
 
Kwa mtanzamo wangu hapa unatakiwa kufuta historia yote kuhusu upatikanaji wa mtoto huyo. Tena wala usijisumbue kulifikilia jambo juu ya ndugu wa mume wa mama mtoto wako kwakuwa hiyo ni damu yako.
Toa huduma kwa mtoto wako huyo tena umchukue make ni jukumu lako kulea vema. hakuna hata sababu ya mama yake kumchukua tena hasa ikiwa hayuko tayari kufanya hivo. Kama ni maamuzi ulishayafanya toka siku uliyokubali kumpa mimba..... Malizia sasa sehemu iliyobakia

Mungu na akuuumbie moyo wa huruma....akufumbue macho pia ili uweze kuona kuwa ni wajibu wako kuokoa maisha ya huyo malaika (hakuhusika kwa lolote ktk starehe yenu)
 
mpende sana mkeo......ni ngumu kwa mwanamke kuelewa hii hali, tena ndoa yenyewe bado changa hivi ni wakati mgumu kwake.
 
Kwanza, nakupa pole sana kwa yaliyokusibu maana hukuyatarajia kabisa.

Pili, nampongeza sana wife wako kwa kuwa mwelewa maana hii ishu ni ngumu kidogo.

Tatu, mtihani unaoukabili, utawafunza na wengine kuwa kabla ya kukubali kufanya kitu, tafakari sana kwa marefu na mapana.

Mwisho, kama walivyoshauri wengine, jizatiti kumtunza "mwanao" kibinadamu maana unajua kabisa kuwa huyo mwana ni wako. Isingekuwa hivyo, kisheria huyo mwana ni wa mume wa huyo mdada na lisingekuwa jukumu lako kumtunza maana alizaliwa kwenye ndoa ya huyo mdada na marehemu mumewe.
 
Uporoto sasa hivi ndio nimekusoma vizuri baada ya kujibu maswali yetu! kumbe ilikuwa kabla haujaoa...lakini bado mama mtoto anatakiwa amlee mwanae.
 
mpende sana mkeo......ni ngumu kwa mwanamke kuelewa hii hali, tena ndoa yenyewe bado changa hivi ni wakati mgumu kwake.

Huyo mwanamke lazima autatue huo mtihani wa kukaa na mtoto wa kambo akishindwa bora aanze atampendaje Mr. tu?
 
Uporoto sasa hivi ndio nimekusoma vizuri baada ya kujibu maswali yetu! kumbe ilikuwa kabla haujaoa...lakini bado mama mtoto anatakiwa amlee mwanae.

Hapo sasa umenena ni jukumu la huyo mama kulea...
 
Hapo sasa umenena ni jukumu la huyo mama kulea...

mbona nilimaanisha hivyo kuanzia mwanzo? au hujanimanya...jukumu la mama mzazi amlee mwanae! umeshajazia umri kule tupeleke posa?
 
Uporoto sasa hivi ndio nimekusoma vizuri baada ya kujibu maswali yetu! kumbe ilikuwa kabla haujaoa...lakini bado mama mtoto anatakiwa amlee mwanae.
Nyamayao...bottomline ni kwamba huyo mama mzazi anaonekano kutokua tayari kumlea mwanao...sasa uporoto afanyeje??? Hawezi kumwacha mwanae akae na mama asiyekua tayari kulea!
Si unajua kuna wanawake wasio na uwezo wa kulea??
 
Wewe ni baba, mtoto huyo hana na hatapata baba mwingine duniani. Chukua mtoto, muweke popote, mhudumie. Ila utapokabidhiwa huyo mtoto mwende kwa lawyer athibitishe kuwa wewe ndo mzazi kusije kukatokea tatizo lingine la kisheria.

After all wakati mnamtafuta(mimba) ilikuwa starehe kwenu tena tamu, leo chukua jukumu.
 
Nimeishi maisha ya kumkosa mzazi mmoja, mama yangu alifariki nikiwa na miaka 3, nikiona situation km hizi namfikiria mtoto zaidi na uchungu wa kukosa mzazi. nazijua shida zake in and out. TAFADHALI uporoto01 mtoto anahitaji msaada wako, wife aelezwe hilo, hiyo ni damu yako, asthma isiwe kikwazo kwako kumhudumia, mimi nilisumuliwa sana na huo ugonjwa nikiwa mdogo, lkn mama yangu(wa kambo) alinibeba saa nane ya usiku na kunipeleka hospitali. hakujali km mie si mwanae, mungu ailaze roho yake mahala pema peponi(na yeye alifariki).
 
Nyamayao...bottomline ni kwamba huyo mama mzazi anaonekano kutokua tayari kumlea mwanao...sasa uporoto afanyeje??? Hawezi kumwacha mwanae akae na mama asiyekua tayari kulea!
Si unajua kuna wanawake wasio na uwezo wa kulea??

hili jambo ndio mie ckubaliani nalo, alivyomtafuta huyo mtoto kwa maarifa yote mpaka akafanikiwa alijua nani atamlelela?...anatakiwa amlee mwanae kwa bidii zote kama alivyotumia bidii kumpata.
 
pole sana Chimunguru.
 
Pole sana mkuu Chimunguru! hujafa hujaumbika ndugu yangu! Hapo kwenye bold, that has been my argument throughout this thread
 
hili jambo ndio mie ckubaliani nalo, alivyomtafuta huyo mtoto kwa maarifa yote mpaka akafanikiwa alijua nani atamlelela?...anatakiwa amlee mwanae kwa bidii zote kama alivyotumia bidii kumpata.

Hebu chukulia huu mfano...
Tufanye umezaa mtoto na bahati mbaya huishi na baba wa mtoto, mtoto anaishi na babake....ukisikia mtoto wako halelewi vizuri utakaa kimya?
 
Hebu chukulia huu mfano...
Tufanye umezaa mtoto na bahati mbaya huishi na baba wa mtoto, mtoto anaishi na babake....ukisikia mtoto wako halelewi vizuri utakaa kimya?

ni hivi mtoto wangi ningemlea mwenyewe bab yake angeleta matunzo tu.....na huyu mtoto sio wa bahati mbaya walipanga yakapangika, bac na mama ackwepe jukumu la kumlea mwanae akisaidiana na mzazi mwenzie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…