Godbless Lema awali aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kabla ya uteuzi wake
kutenguliwa na Msajili wa vyama vya siasa, na kisha baadaye kuteuliwa tena kwa ajili ya kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Madai kuhusu Lema kustaafu siasa
Kumekuwepo na taaarifa inayosambazwa mtandaoni kwa kutumia grafiki zenye utambulisho wa Jambo TV, Wasafi Media, Mwanahalisi na ITV kuwa Godbless Lema anatumia jina la Lissu na CHADEMA kutafuta misaada Canada.
Uhalisia wa taarifa hiyo.
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani, haijachapishwa na vyombo hivyo (
Mwanahalisi,
ITV,
Jambo TV pamoja na
Wasafi Media)
bali ni ya kutengenezwa na wapotoshaji.
Hata hivyo grafiki hizo zimebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo matumizi ya mwandiko (Fonti) ambazo hautumiwi na vyombo hivyo jambo linalodhihirisha kuwa ni za kutengenezwa na wapotoshaji.