Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Baadae kampuni ya Pacific seafood ya nchini Marekani iliposikia habari za kuvuliwa kwa samaki huyo adimu duniani ilitangaza offer ya 30,000$ kwa kila kilo sawa na TZS 69M kwa kilo, ambapo ingelipa jumla ya 2.6 US$ million sawa na Tshs bilioni 6 kwa kilo zote 87. Lakini wakati kampuni hiyo inatangaza offer hiyo tayari samaki huyo alikua ameshaliwa na kuisha.
Frank Dulcich Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Pacific Seafood amesema kitu ambacho mvuvi huyo hakujua ni kwamba wakati anafurahia kutafuna minofu ya samaki huyo, alitafuna pia urithi wa familia yake vizazi na vizazi.
"As he was eating together with his villagers, he didn't know that he has eaten the wealth for his generations to come" amesema Dulcich!
Blue Marlin ni moja ya samaki adimu sana duniani na wenye thamani kubwa sana baada ya Bluefin Tuna na White Marlin. Wanapatikana bahari ya Pacific tu, na kabla ya huyu aliyepatikana Nigeria, mwingine alipatikana nchini Nicaragua mwaka 2014!