Kwenye ukurasa wa 9 inapozungumzia suala la "Finance" kuna kauli ambayo kwa mchumi yeyote au hata aliyepitia kwa juu juu ina uzito mkubwa sana. Mpango unasema hivi:
The world bank has pointed out that financial stringency and budgetary limitations will be determining factors in any planning for the future. These budgetary limitation are due to the very small taxable capacity of Tanganyika's low-income economy.
Hii ina maana gani? Ina maana ya kwamba kwa miaka 40 ambayo wakoloni walikuwa wanaendesha uchumi wa Tanzania hawakutengeneza uchumi ambao ni sustainable enough kuweza kujiendesha wenyewe. Sehemu ya uchumi iliyolipa kodi ilikuwa ni ndogo sana. Kwa maneno mengine mafanikio yoyote ya maendeleo wakati ule yangetegemea sana kile kinachoitwa kama "tax base" yaani sehemu ya uchumi inayotozwa kodi (iwe ni watu, au sekta fulani).
Mpango huu pia kwenye sehemu hiyo hiyo unatuonesha kuwa Nyerere mwenyewe kama mchumi - tukumbuke kasoma uchumi - anatoa somo la msingi sana kwa mchumi wowote - unatumia kulingana na mapato yako. Mpango unasema hivi:
The size of recurrent expenditure (matumizi ya kawaida-MM) which is limited by recurrent revenue , i.e by the amount of money that Government collects each year in various taxes places in turn a limit on the size of development expenditure.
kwa maneno mengine, mapato ya kawaida tunayoyapata kutoka katika kodi mbalimbali yanatumika zaidi kugharimia matumizi ya kawaida ya serikali (mishahara, malipo mbalimbali ya kuendeleza vilivyopo n.k) kabla ya kiasi kinachobakia kwenda kwenye matumizi mapya -yaani ya maendeleo. Kama tax base yako ni kidogo na kama matumizi uliyonayo tayari ni makubwa, ni wazi kuwa ni fedha kidogo sana ya kodi yako itakayoenda kwenye maendeleo. Hili haliitaji shahada ya kwanza ya uchumi toka UDSM kuweza kulielewa. Mtu yeyote aliyejifunza classical economy - lile likitabu fulani likubwa hivi - anaweza kuelewa siku ya kwanza darasani.
Na kutoka hapo mpango unaeleza kitu kingine cha wazi sana, kwamba hata ukiingiza fedha kwenye mpango fulani wa maendeleo kwa mfano kujenga hospitali au shule, mpango ule ukikamilika unageuka kuwa ni mpango wa kudumu na hivyo utatakiwa uingizwe kwenye bajeti ya matumizi ya kawaida; kwa maneno mengine, mipango ya maendeleo inazidi kubebesha mzigo katika bajeti ya kawaida ya matumizi kila mwaka.
For example, capital expenditure on hospitals and schools provided for in development plan will generate after their completion recurrent expenditure on staff, nurses, and doctors and on teachers and students respectively. Such a recurrent expenditure has to be accommodated in recurrent budgets long after its origin - the building of hospitals and schools has been completed.
Ni kutokana na ukweli huo ilionekana wazi kuwa uchumi wetu usingeweza kukuwa kwa zaidi ya asilimia 5 kwa mwaka. Siyo maoni ya Nyerere hayo bali ya Benki ya Dunia ambao walishiriki sana katika kuandaa mpango huu. Leo hii watu wanazungumzia kukua kwa asilimia 7 kama lengo! Wakati wana tax base kubwa zaidi, wasomi wengi zaidi, na sababu nyingi zaidi za kufanya vizuri.
Kutokana na uelewa huu mpango wa maendeleo unasema hivi (Uk.12):
The total increast of some 3-4M poundsin recurrent expenditure will no doubt represent a heavy burden on Tanganyika's budget. It is thie recurrent commitment which limits the size of the Development Plan itself and within the Plan restricts the development of those services that give rise to particularly heavy recurrent expenditure such as Education and Medical services. These two services alone account for more than half of the total increase in recurrent expenditure arising from the plan.
Sasa hapa hatuna budi kuwauliza wale wanaomkosa Nyerere, what is wrong with reasoning background of this plan? Kauli hizo zina uongo gani wa kiuchumi. Watu wanasema Nyerere angeweza kujenga mashule mengi na mahospitali bwelele kila kijiji labda na kila mji tena ya kisasa kabisa.. well.. angetoa wapi hela? Angechagua nini? Kati ya shule mpya na barabara mpya au hospitali mpya serikali ya mwanzo ingechagua nini hasa kama bajeti yake iko limited hivyo?
Kama hawa wakosoaji wangekuwa na ukweli huo wao wangechagua kufanya nini?
Sasa juzi wamepitisha mpango wao wa maendeleo; angalia mgawanyo wa jumla wa mpango wa Nyerere (Uk. 13) :
Asilimia 60 ya fedha zote zilizokuwa zinaombwa kwa ajili ya mpango huu ilikuwa ni kwa ajili ya maendeleo
Asilimia 20 Huduma za jamii
Asilimia 20 kwenda Jeshi, Polisi, Mambo ya Nje, Majengo ya serikali na mengineyo.
Je katika bajeti ya mwaka huu peke yake asilimia ngapi inapelekwa kwenye maendeleo kulinganisha na fedha zinazoenda kuhudumia matumizi ya kawaida?
Kuhusu suala la barabara Nyerere na mpango wa serikali yake wanatuonesha walivyokuwa wanaona mbali!
The Mission's view that the main trunk road system is virtually complete is not accepted by the Government. The present main road system looks outwards, particularly in the noth and facilititaes the flow of purchasing power from the rich provinces in teh north to Kenya and Uganda rather than inwards to Tanganyika. Also, there is no direct road connecting the prosperous Lake and West Lake provinces (Mwanza, Kigoma, Shinyanga of the time- MM) with the Northern Province and with Tanganyika searports so that the main flow of imports and exports has to make a detour via kenya and Uganda. Similarly, there is no convenient link with teh potentially rich Southern Highlands and the Kilombero valley.
The government's view is that the new main road system should connect the areas of agricultural and mineral production (taking into sonderation their future potential) with the main outlets in Tanganyika. Also, there is little point in starting an ambitious feeder roads programme if there are no railheads and main roads to feed to. However, the Government accepts the Mission's view, that gradually the emphasis should shift to feeder roads and this factor will be taken into consideration in the next plan.
Ndugu zangu, hii ndio reasoning ya great leader. Hakuitaji kuuma maneno bali kuita vitu jinsi villivyo. Kuna watu wanataka tuamini kuwa wakoloni walitutandikia barabara kila kona ya nchi na Nyerere akaja akaziharibu; wanataka tuamini kuwa mtu uliweza kutoka Tanga hadi Mahenge au Ilula hadi Magu kwenye barabara za lami! Wanataka tuamini kuwa ilikuwa rahisi kutoka Ifakara kwenda Morogoro mjini kwenye barabara za kuvutia zilizoachwa na wakoloni. Ukweli uko wazi kwa Mtanzania mwenye fikra huru kuamua; yule ambaye yuko tayari kufungua macho yake baada ya kupewa hiki kidonge kama alichopewa Neo kwenye "The Matrix".
Ili kuweza kutoa hukumu ya haki ya uongozi wa Nyerere ni lazima kwanza mtu afungue hisia zake, kukataa aliyoimbishwa na watu wengine na kwa macho meupe asome yeye mwenyewe kama mwanadamu mwenye fikra huru na kuanza kuangalia ushahidi ulioko mbele yake. Ni katika kufanya hivyo tu mtu ataanza kujenga ile balance ya kweli na siyo extremes view za "uovu, ubaya" wa Nyerere ambazo zinamuondoa Nyerere kutoka katika context of historical paradigm of which he was part of.