Hii ni kashfa. hapo kwenye bold, unataka kutusadikisha kwamba huo ndio ulikuwa mpango kamili wa Nyerere kuhusu Agriculture? inaonekana unatumia zaidi hisia badala ya kuchambua hoja. suala la kupeleka watu katika vijiji ni kwamba tokea hapo concept ya vijiji imejikita na zunguka Tanzania pote watu wanaishi katika vijiji ambapo huduma za elimu, afya, maji nk. zinaweza kupelekwa huko. watu wanatumia maeneo ya mbali na vijiji kwa shughuli maalum tu na wanakwenda huko kwa muda na kurejea katika kijiji. hata mijini kuna mitaa, kata, wilaya, nk. zamani kila watu walikaa katika sehemu zilizotapakaa huku na kule. Nyerere, being a people-focused person, alitaka hawa watu waonje maendeleo, washiriki kula keki ya taifa lao. sioni njia nyingine zaidi ya kuweka mfumo wa watu kukaa katika vijiji. policy was right, unaweza kuzungumzia kuhusu utekelezaji wa hapa na pale. lakini kama nilivyosema, tunafaidi matunda ya hiyo policy mpaka sasa. na ndio maana tunaweza kuzungumzia shule za kata, nk., ijapokuwa hapo ndio kabisaa tumevuruga. ona hiyo tofauti: shule za kata lengo ni kupata umaarufu wa haraka haraka, with disastrous results. vijiji, lengo ni kuwapatia watu huduma, na mpaka sasa concept ndio tunaitumia na kumtukana mwanzilishi.
kuhusu Kilimo, ukitaka kuzungumzia mpango wa Nyerere katika kilimo, inabidi uzingatie mfumo mzima alioujenga. ni kweli alikuta some research stations za kilimo, lakini aliziendeleza sana. mabwana shamba aliwakuta, akawaendeleza sana na kuwapa resources za kufanyia kazi, walikuwa pia na hadhi kubwa sana. aliimarisha institutes, na akaendelea mpaka tertiary level. siasa kwa upana wake ilikuwa inapumua kilimo tu. sasa ili kuweka vizuri coordination kati ya research centre, mkulima, kwa kutumia bridge ya bwana shamba, concept ya vijiji ilikuwa muhimu. ukitaka kuwa fair katika kumjadili Nyerere, do your homework. otherwise ni hate religion