Son of Gamba kwa mfano wewe unadhani njia gari bora itumike wakati njia zote za kidemokrasia zimeshindikana? hili ni jukwaa huru labda utuambie kwa mtazamom wako wewe ni njia gani inafaa? usikimbilie kwenye kutishia vita tu na ukadhani watu wanatishika kaka, weka hapa ni njia gani unadhani wewe zinafaa?
mr mkiki nadhani umetumia maneno ya sitiari kidogo kuficha ukakasi wa bandiko lako, lakini kauli nzuri ni kuwa CHADEMA na muungano wote wa vyama watafute mbadala wa njia gani za kukabiliana na Jeshi la polisi. Hio hasa ndio ilikuwa kauli sahihi kutumia. Uchaguzi wa juzi Buyungu mgombea anasema walipelekwa Field Force 400 tena usiku mnene na Katibu mkuu CCM anasema vita ni wakati wote, sasa hapo unadhani kuna nini tena? kwenye bandiko lako ondoa neno intelijensia weka neno "Techniques za kupambana na jeshi la polisi na tume yake"