Mtia saini namba 55 katika waraka wa watia nia wa ubunge 55 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 2025, maarufu kama G55 James Kabepele, amekana kuhusika katika waraka huo akiwataja wahusika kuwa ni wasaliti wa Chama.
Kabepele ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Tabora amekanusha kuhusika na waraka huo wa vuguvugu la G55 linalodaiwa kupinga kampeni ya 'No Reforms No Election', na kusema kuwa hakuwahi kuweka saini kwenye waraka huo wala kuonesha nia ya kugombea jimbo lolote.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kabepele amesema kuwa waraka huo unaotaja jina lake kama mtia nia wa Jimbo la Igalula, pamoja na saini inayodaiwa kuwa yake, si wa kweli na haukuwahi kupata ridhaa yake.
“Mimi si mtia nia wa jimbo lolote, na sikuwahi kuweka saini kwenye waraka huo. Siwezi kujua nani aliweka saini hiyo kwani ni rahisi kughushi kwa sababu ya nafasi yangu na ushiriki wangu katika vikao mbalimbali vikubwa,” amesema Kabepele.