James Mbatia amkingia kifua Spika Ndugai, kwenda mahakamani kuzuia mchakato wa kutafuta Spika mpya

Sijui ni umbumbumbu wangu wa sheria!!? Naona kama kesi ya Mbatia imekosa mashiko na Mbatia anakosa uhalali wa kuifungua.

Hapa ni sawa na mke/mume aamue kumuacha mume/mke wake halafu jirani akapinge mchakato wa kuachana.

Au mfanyakazi aamue kuacha kazi na mwajiri wake akaridhia, halafu anatokea kidudu mtu apinge mchakato.

Pascal Mayalla na Petro E. Mselewa
naombeni msaada ktk hili.
 
Anaweza kuwa na hoja lakini kwa mfumo ulivyo hiyo imeshatoka hatutegemei cha tofauti
 
Ukisikia mwanaume anaingiliwa na wanaume wenzie usitarajie atakuwa na akili nzuri. Msimchukulie Mbatia James seious
 
Kwa wanamuziki ili wabaki kwenye game wanahitaji wawe na kiki zitakazo wafanya wawe kwenye head line.

Hivyo hivyo kwa wanasiasa inatakiwa waweke chokochoko ili wapate air time kubaki katika reli ya siasa na kuzungumziwa.
 
Unataka kusema Katiba ya nchi hii hamhusu Mbatia na NCCR? Watanzania tumekuwa wajinga sana na nchi itaendelea kuwa masikini mpaka mwisho wa dunia.
 
Pascal Mayalla na Petro E. Mselewa
naombeni msaada ktk hili.
Mkuu Sexless , japo sijabahatika kuiona charge sheet, lakini Mbatia has a point.
1. Katiba imetoa maelekezo Spika akijiuzulu barua anapeleka kwa nani?. Hili halijufanyika!. Why?. Mahakama itajibu.

2. CCM ndio imeliarifu Bunge, na Bunge likakubali!. Who is mightier kati ya Bunge na CCM?. I thought enzi za party supremacy are over!.

3. Kuna watu wamezuiwa kugombea Uspika, wametajwa mawaziri, manaibu mawaziri na viongozi wengine wanaotajwa na katiba. Tulia kagombea bila kwanza kujiuzulu unaibu Spika, kasema Naibu Spika hatatajwa!.
Mahakama itajibu.
P
 
Ndugu,
Wakati wa kesi ya Lissu kuvuliwa ubunge walituthibitishia kuwa kwenye mambo ya msingi, mahakama yetu haiko tayari kugombana na Bunge. Mbunge wa kumrithi Lissu alipokelewa na kuapishwa Bungeni wakati kesi ya kupinga bado iko mahakamani.
Mbatia aendelee na kesi kwa madhumuni ya kuuanika tena muhimili huo uliyokosa aibu. Labda waTz wataanza kufumbuka macho. Amen
 
Aliye kuambia Tanzania kuna mahakama kakudanganya!
Ni kweli. Ona katika kesi ile ya "MCHONGO"
Jaji= mteule wa rais ambaye alishasema
Mbowe gaidi.
Mashahidi= karibu wote ni askari polisi, waajiriwa wa serikali inayoongozwa na huyo huyo raisi ambaye amemteua jaji na tayari kesha sema Mbowe ni gaidi. Hapo hatutegemei haki, kwani @mbwakalambwa.
 
Ukisikia mwanaume anaingiliwa na wanaume wenzie usitarajie atakuwa na akili nzuri. Msimchukulie Mbatia James seious
Matusi si uungwana. Tuangalie hoja ya Mbatia. Je katiba yetu inasemaje juu ya kujiuzulu kwa spika. Ni lazima atangaze hivyo ndani ya bunge mbele ya wabunge na Siwa au anaweza kujiuzulu hata kwenye banda lake la kufugia kuku?
 
Ni case nzuri Sana ambayo inaweza kuisaidia Nchi kwa kuweka Misngi mizuri kwa Jambo Kama hili la Ndungai haswa kwa wakati ujao. Lakini kwa Mahakama hizii, sijui. Tena itapigwa chini kwa vitechnical grounds vya kutafuta kwa tochi.
 
Sitegemei maajabu kwa nchi isiyojali katiba kama hii. Angalia wanavyowakumbatia wale covid 19 pale bungeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…