James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

Kwa namna alivyonogewa na hicho cheo, sijui kama ataupokea huu ushauri wako kwa mikono miwili! Nadhani atachagua tu kufa na tai yake shingoni. πŸ˜‡
 
Kutembea na escort ya king'ora ndani ya kiyoyozi kuna raha yake, asikwambie mtu. Mzee atakaa mpaka dakika ya mwisho kuomba Majaaliwa (kama jina lake) ya Mungu.
 
Hapo patamu maana alishasahau bei umeme, maji, petrol, chakula, mavazi n.k shida anaziona kwenye tv pekee
 
Tufuate Katiba. Si vizuri kwa nafasi zote za juu kuwa na Watu wapya. Nimesikia Rais Samia SH akisifiwa leo alivyo tuongoza vizuri kipindi cha Msiba. Hivi hizi sifa ni za Mh Rais peke yake au ni team mzima. Mh Rais na Makamu wake kama wanafikiri ni afya kwa kumtoa PM na kuvunja Baraza la Mawaziri na Wafanye hivyo. Ila ingekuwa vizuri wakajaza nafasi kwa Umakini ya Wizara ya Fedha. Na wakaendelea na Baraza lililopo halafu wakawapa matarajio yao. Atakaye shindwa kutumbua kuhusike.

Nchi hii imetikiswa vya kutosha na msiba wa Hayati JPM tusiitikise tena kwa taama za watu kutafuta vyeo.

Mbatia anataka ubunge wa viti maalumu kwa hiyo naye kasema asikike.
 
Majaliwa amekaa kishari sana utafikiri amepewa hati miliki ya kuwa waziri mkuu milele wakati cha maana anachokifanya hata hakionekani
 
Mnampotosha huyu mama, mnatafutia vita huyu mama CCM ni hile hile na watu ni wale wale au mnataka akalete mawaziri Zanzibar kwao?

yeye ni Vp Hilo balaza la mawaziri wakati linaundwa si alikuepo kwenye huo utawala
Hujawajua hawa watu wanataka nini? Wanajalibu kubahatisha kama mama atapovunja baraza la mawaziri labda mama anaweza kuwakubuka kwenye teuzi
 
ACHA WIVU NA CHUKI UTAKUFA MASIKINI
 
Naona Sasa wafanya kazi wanaanza kupangia boss cha kufanya au mnataka avunje baraza nanyi awakumbuke kwenye teuzi?
 
pambana atakukumbuka kwenye teuzi!
 
Wakati unampigia kura magufuli,ni wakati huo huo ulimchagua na Makamu wake.
basi sawa Kama mambo yapo vile PM Hana ulazima wa kujiuzulu,tulishajua mnachotaka baraza livunje ili nanyi awakumbuke kwenye teuzi
Si ndio hicho mnachotaka?
 
Ushauri ni mzuri japo lishafanya nao kazi hakuwa na uwezo wa kuwaondoa.
 
Naona Sasa wafanya kazi wanaanza kupangia boss cha kufanya au mnataka avunje baraza nanyi awakumbuke kwenye teuzi?
Naona ww ndie afisa habari wezi wa kujibu hoja za watu wote JF.
 
ACHA WIVU NA CHUKI UTAKUFA MASIKINI

Sema nitakufa bila kuwa milionea, lakini sio umasikini maana huko nimesharuka na siwezi kurudi, labda itokee janga la asili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…