Hiyo sasa ndiyo mistake yake kubwa kisiasa aliyofanya! Inawezekana kwa kujua, kwamba wamekubaliana na wanamtandao au pengine kutokujua. Amejitengenezea upinzani (ndani ya chama, nje ya CCM hamna upinzani) mapema mno, tena kwa kutaja kabisa kwamba anafanya mabadiliko ya Baraza baada ya kuona watu wanafocus 2025! Mnamkumbuka "shati la kijani mwenzio"
Wale watu watampa shida na ukizingatia muda bado sana. Suala la watu kumchafua JPM bila serikali au chama kukemea nalo ni bomu litakuja kupasika tukikaribia uchaguzi. Wananchi hawajalipokea vizuri, inaonekana tunatakiwa tuende 2025 bila kutaja jina la JPM lakini kuna kila dalili kampeni imefeli.