Elections 2010 James Mbatia apata shida kupiga kura Kawe

Elections 2010 James Mbatia apata shida kupiga kura Kawe

Endeleaaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
1,485
Reaction score
739
Live from ITV Mbatia ameonekana akilalamikia kuzuiwa kupiga kura baada ya jina lake kukosekana kwenye orodha ya wapiga kura.

Hili linaonekana ni tatizo kubwa sana maana wanaonekana wengi kukumbwa na tatizo kama hilo la mbatia.
 
Hivi hata Mbatia hakuhakiki kwanza kama jina lake lipo?
 
Live from ITV Mbatia ameonekana akilalamikia kuzuiwa kupiga kura baada ya jina lake kukosekana kwenye orodha ya wapiga kura.

Hili linaonekana ni tatizo kubwa sana maana wanaonekana wengi kukumbwa na tatizo kama hilo la mbatia.
sasa kama hajajiandikisha alitegemea nini? Aende kushikishwa ukut* huko!
 
Live from ITV Mbatia ameonekana akilalamikia kuzuiwa kupiga kura baada ya jina lake kukosekana kwenye orodha ya wapiga kura.
Siku zote nane alikuwa wapi kuhakiki jina lake?
 
katika hali ya kushangaza, jina la mgombea ubunge jimbo la kawe kupitia nccr mageuzi, mh. James Mbatia hatapiga kura mpaka sasa kwa sababu jina lake halijaonekana kwenye orodha.

Kwa kweli NEC wamechemsha sana kwenye maandalizi ya uchaguzi. Pia mh. Mbatia amewaonesha waandishi wa habari kadi feki ya kupigia kura iliyo amatwa yenye jina bila picha ya mwenye kitambulisho.
 
Mkulima unasema nini wewe! majina yameondolewa kwa makusudi, watu walihakiki na wakaona majina yao. Angalia sasa mpaka vitambulisho hewa vya kupigia kura, ameletewa na mpenda haki ameonyesha kama ushahidi.
 
Uyu nae anaonekana hayuko makini
Sasa anatupa picha gani wananchi wa kawaida ebuu aache usanii apa
 
Tuache kulalamika na tuchukue hatua. Hivi kweli itakuwa rahisi jina la Mbatia liwepo siku mbili zilizopita halafu lieondolewe leo?

Kama wanatoa majina, hawawezi ku risk kwa kutoa jina la kigogo kama Mbatia.

Atakuwa hakuhakiki jina lake.
 
Tena bila aibu analalamika!Huyu kama ameshindwa kufuatilia jina lake kabla ya uchaguzi,akiwa mbunge ataweza kweli kufuatilia matatizo ya wana Kawe?
 
Hizo kadi zinatumika kupiga kura kwenye vituo vyao feki
 
Kwani hata kama halipo si itakuwa halipo tu. Usajili haufanyiki. Hujuma wazi wazi.

Watu wengi tu majina yao hayakuwepo na baada ya kulalamika, ufumbuzi ukapatikana.

Sasa Mbatia anaomba kura za wengine huku anashindwa kulinda kura yake? Mtu kama huyu anapoteza tu muda wa NEC kulalamika sasa.
 
Kama hii inatokea kwa mgombea ubunge na mwenyekiti wa chama taifa, ni maelfu mangapi ya wapiga kura ambao kwa makusudi NEC ya mafisadi imewanyang'anya haki yao ya kupiga kura?
 
Usually Majina Yapo. Watu wanashindwa tu kufuatilia kwa Uzuri.
 
Back
Top Bottom