Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimekusamehe...Machadema banna!! ujinga tu umewajaa ndio maana Lwakatare amesema mna maplastic ndani ya vichwa vyenu
Boss, hapa siyo suala la CHADEMA na CCM. Vyama ni vingi siyo viwili. Wengi tunapenda kuwe na checks and balances. CCM ni wema kwa sababu ya upinzani kuwazoza. Lakini upinzani unatakiwa usioneshe uhuni pia.Tuinue ubora wa upinzani kwa vigezo vya kiccm!
Hatimaye utaelewa maana ya kuinua ubora wa upinzani. Mkiti wa chama anahangaika mitaani usiku wa manane wakati yuko shughuli za Bunge zinazohitaji mtu kuwa makini na kazi zake, na nyendo zake.Tuinue ubora wa upinzani kwa vigezo vya kiccm!
Hatimaye utaelewa maana ya kuinua ubora wa upinzani. Mkiti wa chama anahangaika mitaani usiku wa manane wakati yuko shughuli za Bunge zinazohitaji mtu kuwa makini na kazi zake, na nyendo zake.
Jibu hoja ya Mbatia siyo kuandika kile ulichokaririshwaHuyo Mbatia anajushuku tu. Anatakiwa afanye kazi aliyotumwa na CCM kwa ufanisi, vinginevyo arudishe hela.
Hujaelewa! Sijadili chama kukuwa wala kuungwa mkono, wala kupendwa na marafiki zake wala kuacha ulevi. Nionacho hana sifa ya kuwa kiongozi wa nchi. Aongoze anaowaongoza hilo siyo kosa. Hata Nyumbu na quelea-quelea na njiwa wana viongozi.Mbowe sio mtoto wa shule useme hakuwa domitory wakati wa usiku, na kama ni pombe hakuanza kunywa jana, na hatakaa aache. Kama ni kukutana na majanga tatizo halikuwa usiku, maana Lisu alishambuliwa mchana kweupe. Hicho chama kimefikia hapo kilipo akiwa na tabia hiyo hiyo, kama hiyo tabia hiyo ndio kikwazo cha chama kukuwa, basi ndani ya miaka 16 yake ya uenyekiti, hakikupaswa kuwa hapo. Ni hivi, huenda una point za msingi, lakini unakosa maneno sahihi ya kuwakilisha pointi zako, hivyo kajipange upya.
Hujaelewa! Sijadili chama kukuwa wala kuungwa mkono, wala kupendwa na marafiki zake wala kuacha ulevi. Nionacho hana sifa ya kuwa kiongozi wa nchi. Aongoze anaowaongoza hilo siyo kosa. Hata Nyumbu na quelea-quelea na njia wana viongozi.
Nincompoop!Ni wapi Mbowe kautaka urais? Au unaanza kuokoteza hoja?
Umeanza kupata akili sasa. Hahaaaaa.Bora sahvi tujikalie kimya tu
Wanasiasa siyo wa kuwa amini
Ova
Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Saa kadhaa kabla ya ngazi kugoma kubeba waleviHujaelewa! Sijadili chama kukuwa wala kuungwa mkono, wala kupendwa na marafiki zake wala kuacha ulevi. Nionacho hana sifa ya kuwa kiongozi wa nchi. Aongoze anaowaongoza hilo siyo kosa. Hata Nyumbu na quelea-quelea na njia wana viongozi.
Mrema mwingine huyo..Mbatia hana maisha kisiasa na kimwili (Dead man walking). Ndio navyomuona.
Lakini Mbatia apa ulienda ikulu kufuata Nini? Apa Tena kama kama huna ukamerooon Hivi wewe na Bashite mna ukewenza?Salaam Wakuu,
Kuna kipande kidogo cha video kinasambaa Mtandaoni, James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi akielezea kusikitishwa kwake na wanaomuona kwamba anavunja nguvu upinzania.
Hapa chini nmenukuu kile alichokiongea na kukiandika hapa chini.
Ameanza kwa kusema:
View attachment 1469145
"Mimi ni Mbunge wa Vunjo, umewahi kunisikia nalalamikia labda CHADEMA kwanini wameweka Mgombea kule Vunjo?
Niwe mkweli tu. Uchaguzi mkuu mwaka 2015 vyama Vingine viliweka Wagombea na wao tumo ndani ya UKAWA tukagawana zile kura za Madiwani CCM ikashinda, ulisikia nmelalamika?
Mwaka juzi nlimwambia Naibu Katibu Mkuu Bara Elizabeth kawaulize Washirika Wenzetu kwanini wanafanya fujo kule Vunjo? Alipowauliza wakasema Mbatia amezoea kudekadeka sana. Ulisikia nalalamika popote?
Ni haki yao na ni haki ya chama kilicho sajiliwa kina haki ya kufanya kazi mahali popote pale.
Mwasisi namba moja wa NCCR Mageuzi mwenye chama Mabere Nyaucho Marando alihamia CHADEMA ulisikia nalalamika popote? Kwanza nliulizwa nikawambia namtakia kila la heri, ni haki yake. Mwesigwa Baregu, ni haki yake.
Nakuhakikishia ukweli wa Mungu Chacha Wangwe akiwa Diwani wa NCCR Mageuzi Tarime Mjini 2003, walienda Viongozi wa CHADEMA wakamchukua wakamfanya Mwenyekiti wa Mkoa wa CHADEMA na wakati yupo NCCR Mageuzi na hatukumfukuza chama. aliendelea kuwa DIWANI"
Mwisho wa kumnukuu.
MY TAKE:
Vya vya siasa vya Tanzania vimetawaliwa na UBINAFSI, KIBURI, KUJIONA BORA na JICHO KWENYE FEDHA ZA BURE.