James Sinclair: A Friend or Foe?

James Sinclair: A Friend or Foe?

I have a problem with a leader, a minister of President, who will go into partnership with an outside investor, like Barrick, while still in power. A minister or president is first and foremost the first and last line of protecting the interests of the people of Tanzania. Sasa anapotumia wadhifa wake kuingia katika miradi na akina Barrick, etc. itakapobainika kuwa maslahi ya umma yamedhulumiwa ni nani atakayetetea umma?

What should he do if he happens to have shares in a company and that company invests in his country? Should he sell all his shares then?
OR
Lets put it this way, a company that has a president or minister of certain country is not allowed to do any work in that particular country?
 
Insurgent,
Unajua mkuu wangu kuna wakati tunavuka mpaka na huu mpango wa ushahidi hasa ktk hoja tunazozianzisha sisi wenyewe.
Wewe unapodai ama kumaanisha kuwa rais wetu alikuwa na hisa Barricks kabla hajashika madaraka! Sasa wewe unao ushahidi wowote maanake tusiwe tunadai ushahidi toka nje ktk issue uliyoianzisha wewe.
JK hakuwa na hisa Barricks kabla hawa jamaa hawajaingia nchini kununua Bulyanhulu na kama unao ushahidi wa kupinga hoja hii ulete hapa ukiambatana na hoja yako.. hapo utakuwa umefunga midomo ya watu!
 
Insurgent,
Unajua mkuu wangu kuna wakati tunavuka mpaka nahasa ktk hoja hii.
Wewe unapodai ama kumaanisha kuwa rais wetu alikuwa na hisa Barricks kabla hajashika madaraka! Una ushahidi wowote maanake tusiwe tunadai ushahidi ktk issue uliyoianzisha wewe.
JK hakuwa na hisa Barricks kabla hawa jamaa hawajaingia nchini kununua Bulyanhulu na kama unao ushahidi wa kupinga hoja hii ulete hapa!

Nafikiri ukisoma post yangu utaona, sijaribu kumtetea wala kumzungumzia JK. Ninaongelea ANY president or minister.
Najaribu kuangalia in wider context...Je tukiwa na situations nilizotaja hawa viongozi wafanye nini?
Jana alikuwepo BWM, leo yupo JK na kesho unaweza ukawepo wewe. Sasa najaribu kuangalia situation kama ile iki"arise" wewe utakuwa na makosa?
 
Insurgent,

Yes ukitazama ktk Upana wa swala hili huwezi kupata jibu kwa sababu kila nchi ina sheria zake. Hapa tunazungumzia swala hili Tanzania na kwa upana wa hii hoja ni pale tu tutakapoweza kumwondoa rais wetu pamoja na viongozi wake ktk kujaribu kutuibia sisi kulingana na sheria walizozitunga wao.
Azimio la Zanzibar ni moja ya wizi huo ambao umeweka tobo kibao kuwawezesha wao kuwa wafanyabiashara ktk nafasi tulizowakabidhi. Leo hii tunasikia maswala ya hisa ktk vitega uchumi vya kitaifa tena basi sio ktk soko letu ila la nje!.. haya ni maslahi ya nani?.. hawa si wanatembea na dola mfukoni!
Sasa ushahidi peke yake unaotakiwa toka upande wetu wa mashtaka yaani sisi wananchi ni uwezo wa kuona kwamba viongozi wetu wametumia wadhifa wao kwa faida zao binafsi.. period!
Now, unaweza kuuliza kwa vipi na ndipo tunaweka matumizi kama haya ya ununuzi wa hisa ktk kampuni ya madini ukiwa waziri wa madini ama rais wa nchi kama moja ya kivutio cha kitaifa.
Kuna nchi kama Zaire am,bako Mobutu aliwaibia wananchi wake mabillioni hadi kuwa mmoja kati ya matajiri wakubwa duniani lakini madai yake yaliwezeshwa na sheria ambazo aliweka yeye mwenyewe kwa faida ya tumbo lake. Na ndio maana akapinduliwa, Hitler na kutaka Kuitawala dunia, sheria za nchi yake zilimweshesha yeye kutimiza lengo lile lakini hii haina maana ni haki hata kidogo.
Kila Mtawala ahata yule Dikteta huwa amewekja sheria zinazompa nguvu kikatiba kuendeleza maovu yake lakini haina maana kuwa huyu ni kiongozi bora, mwenye kulipenda taifa na watu wake.
sasa ikiwa kweli JK ama Karamagi wanazo hisa ndani ya Barricks ipo kila haja ya sisi kulitazama swala hilo na mwanzo wake kwa makini zaidi ili tupate kufahamu kuwa Uongozi uliopo madarakani sasa hivi ni kundi la mijizi wanaopinda sheria kutunisha matumbo yao.
Mimi na wewe hata siku moja hatuwezi simama kubadilisha katiba wala sheria yeyote ila ni hao tuna waamini ambao wamewakabidhi zana zote. Hawa ndio Majemedali wa jeshi letu ambao kwao ni LAZIMA wawakilishe taifa letu kwanza na sio matumbo yao!...

Mwisho ebu jiulize hili deal la Buzwagi umewahi kusikia Tender yake?
 
NI kwa vile hatuna sheria inayopinga mgongano wa kimaslahi ndio maana tunajikuta hatujui tuamue vipi. Rais na Waziri wake wanapokuwa na hisa kwenye kampuni ya madini, kampuni ambayo mmoja wa wanahisa kubwa ni Barrick Gold lazima wananchi wajiulize. Inapotokea kuwa rafiki wa karibu wa Rais ambaye ni mmiliki wa kampuni ambayo Rais ana hisa anapoleta pendekezo la kampuni gani ipewe mkataba, na kampuni hiyo ni ile ambayo imenunua hisa nyingi kwenye kampuni ya rafiki huyo wa Rais, wananchi hawana budi kujiuliza.

Inapotokea kuwa mgunduzi wa madini iliyouziwa kampuni ya Barrick ni afisa katika kampuni ya Rafiki wa rais (ambayo Rais ana hisa) na Waziri wake wa zamani wa madini ana hisa.. wananchi ni lazima wajiulize.

Sasa, iweje ni wananchi peke yao wajiulize?
 
Hizo hisa amenunua au amehongwa? Je kama amenunua pesa aliyonunulia ameilipia kodi kihalali? Na kama hivyo ndivyo tunaruhusu rais kufanya biashara anapokuwa madarakani?

Nakuunga mkono kwa hili ki msingi! Kuna uwezekano kuwa kweli hizo hisa wamepewa tu kwa nafasi zao ili waweze kutumiwa kunyoosha mambo ya kampuni serikalini. Lakini inabidi kuthibitishwa kama ni hivyo!
Cha pili sina uhakika kama kweli kuna sheria inayokataza Rais kuwa mfanyabiashara madarakani ila maadili ya uongozi yanakataza ili. Na jee, hizo hisa walizinunua lini????
 
Nafikiri ukisoma post yangu utaona, sijaribu kumtetea wala kumzungumzia JK. Ninaongelea ANY president or minister.
Najaribu kuangalia in wider context...Je tukiwa na situations nilizotaja hawa viongozi wafanye nini?
Jana alikuwepo BWM, leo yupo JK na kesho unaweza ukawepo wewe. Sasa najaribu kuangalia situation kama ile iki"arise" wewe utakuwa na makosa?

....unaonekana na wewe ni mwizi tuu na kama sio mwizi ni mnazi tuu asiye na akili,unajaribu bogus spin zako ambazo ni za kitoto sana na watu kama nyie ni hatari sana kwa nchi kuliko hao wanao sign huo wizi wa mali zetu.
 
What should he do if he happens to have shares in a company and that company invests in his country? Should he sell all his shares then?
OR
Lets put it this way, a company that has a president or minister of certain country is not allowed to do any work in that particular country?

He should declare his interest like the Bunge's have to do in parliament.The very act of doing so will make him extra caustious,knowing he will be closely watched.The secreacy with which these guys do things is what creates suspicion/doubt of corrupt practices.By nature, they are dishonest.They are now competing with each other for the Richest man in CCM.
 
kichuguu,mwanakijiji,dua,....
...jamani naomba mnielekeze ni wapi imeonyeshwa kwamba JK na Msabaha wana hisa ktk kampuni ya Barick.

nimejaribu kuisoma document iliyoambatanishwa hapa na sijaona mahali JK na Msabaha wakitajwa kama shareholders wa Barick.

...niliwahi kutumiwa katika PM kwamba Bwana Sinclair amekuwa akijigamba kwamba "anawajua" wanasiasa na civil servants, previous and current administrations, wote "muhimu" wa Tanzania.

...vilevile ujumbe katika PM hiyo unadai kwamba Sinclair amefikia mpaka kujigamba kwamba anamjua hata Mtanzania atakayemrithi JK!!

..watanzania tunajua kwamba rafiki wa JK ni Mheshimiwa Ditopile, lakini huko nje Sinclair anajitamba kwamba yeye ndiye swahiba mkubwa wa Kikwete.

...NAOMBA NIELEKEZWE SEHEMU INAYOWATAJA JK NA MSABAHA KAMA SHAREHOLDERS WA BARICK.
 
Joka Kuu.. mwenye jibu hilo ni mimi. Doc uliyoiona wewe hapa siyo ninayoizungumzia mimi. Siyo tu kwamba wana hisa, bali wanatajwa pia kuwa ni maafisa wa Tanzania Royalty. Halafu usichanganye, Kikwete na Msabaha siyo wana hisa wa Barrick Gold, bali Tanzania Royalty Exploration (formerly, Tan Range) ambayo inaongozwa na Sinclair.
 
kichuguu,mwanakijiji,dua,....
...jamani naomba mnielekeze ni wapi imeonyeshwa kwamba JK na Msabaha wana hisa ktk kampuni ya Barick.

nimejaribu kuisoma document iliyoambatanishwa hapa na sijaona mahali JK na Msabaha wakitajwa kama shareholders wa Barick.

Jokakuu

Doc hiyo uliyoisoma wewe ni ipi, naomba nidondoshee link tafadhali.
 
Mwanakijiji said:
Joka Kuu.. mwenye jibu hilo ni mimi. Doc uliyoiona wewe hapa siyo ninayoizungumzia mimi. Siyo tu kwamba wana hisa, bali wanatajwa pia kuwa ni maafisa wa Tanzania Royalty. Halafu usichanganye, Kikwete na Msabaha siyo wana hisa wa Barrick Gold, bali Tanzania Royalty Exploration (formerly, Tan Range) ambayo inaongozwa na Sinclair.

Yebo Yebo,
Mkjj amenijibu vizuri hapo juu....nilifikiri document iliyokuwa posted hapa inawataja JK na Msabaha kama wanahisa. I was wrong.
 
the twist ni kuwa Barrick God waliingia mkataba na Tanzania Royalty wa kununua hisa karibu laki saba na ushee za Tanzania Royalty, na hivyo Barrick ni mojawapo ya wenye hisa wakubwa wa Tanzania Royalty. Hivyo, wanapopata leseni nyingi za kuchimba madini (sasa hivi wanasubiri ya Kabanga) unafikiri nani naye anapata njuluku zaidi?
 
....unaonekana na wewe ni mwizi tuu na kama sio mwizi ni mnazi tuu asiye na akili,unajaribu bogus spin zako ambazo ni za kitoto sana na watu kama nyie ni hatari sana kwa nchi kuliko hao wanao sign huo wizi wa mali zetu.

Naonekana mwizi?! Naonekana mnazi?! Na mimi naspin?
Shida hii inatokea pale watu kama nyinyi wanapokuwa hawana mawazo na kuishia kutukana. Wewe kila mtu anayeongea usichopenda wewe basi mwizi au mnazi.

Namshukuru COMRADE44 for this input:

He should declare his interest like the Bunge's have to do in parliament.The very act of doing so will make him extra caustious,knowing he will be closely watched.The secreacy with which these guys do things is what creates suspicion/doubt of corrupt practices.By nature, they are dishonest.They are now competing with each other for the Richest man in CCM.

Koba, Dua and the like need to learn how to discuss issues. Tatizo la wajinga, hawawezi kubishana na HOJA .Ikianzishwa thread ya matusi nina uhakika hawa mchango wao utakuwa mzuri sana!!
 
the twist ni kuwa Barrick God waliingia mkataba na Tanzania Royalty wa kununua hisa karibu laki saba na ushee za Tanzania Royalty, na hivyo Barrick ni mojawapo ya wenye hisa wakubwa wa Tanzania Royalty. Hivyo, wanapopata leseni nyingi za kuchimba madini (sasa hivi wanasubiri ya Kabanga) unafikiri nani naye anapata njuluku zaidi?

Barick wanakula huku na huku; wao wanapata faida kama independent (wao ndio wachimbaji/wauzaji)na pia wanapata faida kama wanahisa wa Tanzania Royalty...Damn..looks like a good business thinking.

je, kuna makampuni mengine zaidi ya Barick ambao nao wanakula kupitia Tanzania Royalty?
 
Koba, Dua and the like need to learn how to discuss issues. Tatizo la wajinga, hawawezi kubishana na HOJA .Ikianzishwa thread ya matusi nina uhakika hawa mchango wao utakuwa mzuri sana!!

...Yeah, feels like flooding this post with cursing words.
 
Ziuzwe Dar ili nani afaidike? Jambo la maana ni kutunga sheria kuwa makampuni ya madini (labda na ya sekta nyingine kubwa) ni lazima yawe incoporated na registered hapo Tanzania badala ya kuwa matawi ya kampuni mama iliyoko Ulaya. Kwa kufanya hivyo, mambo mengi yataendana na sheria za Tanzania. HIvi sasa kampuni iitwayo "Tanzania Royalty Exploration" is NOT a Tanzania company! Na inaongozwa na sheria za Canada.
 
Back
Top Bottom