Yaani ww ndo jinga kuliko wote
Pumba tupu
Habari yako brother,
kama mwanzo nilivyotangulia kusema kwa kuandika sipo hapa kwa lengo la kukuza ikhtilaf au hawa ni bora kuliko hawa la hasha! Sipo kwa muktadha huo. Bali nipo hapa kueleza kwa kile kilichoibuka kuhusu Ushia na Ussuni.
Unamfahamu Abdillah bin Saabah? Sahaba aliyesilimu kwa Mtume? Lakini alisilimu kiunafaki? Vipi kuhusiana na Hudhayfah ibn Al' Yaman, unamfahamu huyu,ambaye alikuwa ni msiri wa Mtume s.a.w alipewa orodha ya majina ya wanafiq wote kutoka kwa Muhammad s.a.w.
Mtume s.a.w anasema masahaba wake hawa wakuu wa 4 ( Abuu bakr, Umar, Othman na Ally) ni kama nyota hawa. Yeyoye atakaye wafuata ameongoka. Je, unafahamu juu ya hawa Masahaba Shia wanawapokeaje? Kuanzia Abu bakr, Umar na bila shaka Uthman, Shia hawa wanasema ni Laanutullah tena huwa wanadhimisha mpaka na masiku ya kuwalaani. Unafahamu haya?
Unafahamu Shia wanasemaje juu ya mke wa Mtume naye ni mama Aisha wao wanamuita Malaya. Unafahamu hili?
Suratul Baqarah aya ya ii Mungu anasema " Dhalikal kitabu la rayba fiiiih" kwa maana Qur'an haina shaka ndani yake na anayesema hivyo ni Mungu mwenyewe lakini kwa ndugu zetu Shia wanasema Qur'an wanayoitumia watu hii siyo, hii ina mashaka iliyosahii ni yao inaitwa mas' haf fatmah, unajua hili.
Muhammad wahuwa nabiyyan warasuulah naye ni mtume wa mwisho na katika juu ya hilo shahada zipo mbili tu " Ash' hadu anlaa ilaha illa llah" hiyo ni ya kwanza " Wa' ash' hadu annamuhammad rrasuulullah" hii ni ya pili na ndivyo zipo hivyo. Upande wa Shia zipo tatu katika hizo shahada kwa kinachoongezeka ni Ally( karamallahu wajha) Naye kwao ni Mtume huyu. Unafahamu hili?
Je, unajua Maimam 4, Imam Muhammad ibn Idrissatu Shafii, Imam Malik, Imam Muhammad ibn Hambali na Imam Abuu Hanifah wamewazungumziaje hawa Shia, unajua walichokizungumza? Na hawa Maimam hawajaja hivi hivi wametabiriwa hawa na Mtume.
Kwa kukuhabarisha kitabu cha ndugu zetu Shia Mimi nimebahatika kukisoma ni kimoja tu cha kwao wenyewe kama wenyewe na hayo niliyokuambia ni baadhi tu lakini hawa ndugu zetu vitabu vyao kuvipata na vigumu sana. Huwa vinapatikana katika maktaba za kwao na huruhusiwi kuingia mpaka uwe Shia, siyo uwe Muislam Bali uwe Shia tofauti na hapo hupati chochote na wanajuana hawa wana utaratibu wa wao kufahamiana.
Bado sijaja katika ikhtilaf za salafiyyu kuhusu bidaa na madh' hebu mengine. Ndugu yangu tusome.