Write your reply...si utaje hapahapa huo ubaya wa washia?,na huyo mwandishi we fanya kupaste hapa paragraph chache kama amechemka ama anasema kweli tuone,kwanini ufanye siri?
ITIKADI ZA KISHIA
ZITUATAZO NI ITIKADI ZA KISHIA ZINAZOKHITALIFIANA KABISA NA ITIKADI ZA MASUNNI NA KUHITALIFIANA PIA NA WAISLAMU WENGINE
Itikadi hizi ni nyingi sana, lakini nitajaribu kuzitaja baadhi chache tu.
ITIKADI YA KWANZA
Itikadi ya ‘Ar-Raja-ah - nayo ni itikadi ya kufufuliwa na kurudi tena duniani baada ya kufa kabla ya siku ya Qiyaamah.
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika Kitabu Chake kitukufu ameikanusha itikadi hii ya kurudi tena duniani baada ya mtu kufa, aliposema:
“Na yatapomfikia mmoja wao mauti, husema: “Mola wangu! Nirudishe (ulimwenguni) Ili nifanye mema sasa badala ya yale niliyoyaacha.” (Hujibiwa) “Hapana!” Hakika hili ni neno tu analolisema yeye: na mbele yao kuna maisha ya baada ya kufa (Barzakh) mpaka siku watakapofufuliwa.” [ Al-Muminuun: 100]
Kwa hivyo kufufuliwa na kurudi tena duniani kabla ya siku ya Qiyaamah kumekanushwa na Allaah Subhahanu wa Taala ndani ya kitabu chake kitukufu, lakini mafundisho ya Kishia yanaitakidi kuwa Kufufuliwa huko kupo.
Imeandikwa na Al-Kulayniy katika kitabu cha Al-Kaafiy kutoka kwa Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa amesema: “Sunnah imetupa elimu ya vifo na elimu ya matatizo, na (pia imetupa sisi) neno la mwisho, na mimi ndiye Mwenye kurejea tena na tena na mweneye dola, na mimi ndiye mwenye fimbo na mwenye mnyama atakayezungumza na watu.”
Haya yamo ndani ya kitabu cha Al-Kaafiy Juzuu ya mwanzo ukurasa wa 198.
Alieyekifanyia tahakiki kitabu hiki Ali Akbar Al Ghafari anasema:
“Neno ‘Mwenye kurejea tena na tena’, maana yake mwenye kufufuliwa tena na tena, yaani atarudi duniani mara nyingi baada ya kufa kwake.
Hapa tutataja majina ya Maimamu wa Madhehebu ya KiIthnaa ‘Ashariyah:
1. ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu)
2. Al-Hasan bin ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu)
3. Al-Husayn bin ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu)
4. ‘Aliy bin Al-Husayn bin ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu)
5. Muhammad bin ‘Aliy (maarufu kwa jina la ‘Al Baaqir’) (Radhiya Allaahu ‘anhu)
6. Ja’afar bin Muhammad (maarufu kwa jina la ‘Asw-Swaadiq’) (Radhiya Allaahu ‘anhu)
7. Musa bin Ja’afar (maarufu kwa jina ‘Al Kadhim’) (Radhiya Allaahu ‘anhu)
8. ‘Aliy (maarufu kwa jina la ‘Ar-Ridha’ yaani ‘Aliy Ar-Ridhaa’) (Radhiya Allaahu ‘anhu)
9. Muhammad (maarufu kwa jina la Muhammad Al Jawad) (Radhiya Allaahu ‘anhu)
10. ‘Aliy (maarufu kwa jina la ‘Ali Al Hadi’) (Radhiya Allaahu ‘anhu)
11. Al-Hasan bin ‘Aliy (maarufu kwa jina la Al Askari) (Radhiya Allaahu ‘anhu)
12. Al Muntadhir (Mahd) ‘anayesubiriwa’ (na huyu ana majina mengi sana yakiwemo: Al Ghaib (asiyekuwepo), Al Muntadhir (anayesubiriwa), Al Khaif (mwenye kuogopa), na majina mengi mengine aliyebandikwa.
Na kabla ya kuendelea mbele kwa kuzitaja riwaya zilizopokelewa na Al-Kulayniy katika kitabu chake maarufu cha Al-Kaafiy, ningependa kukutanabahisheni jambo moja muhimu sana: nalo ni kuwa riwaya zote nitakazozitaja zilizoandikwa ndani ya vitabu vyao hivyo ni uongo waliosingiziwa Maimamu hawa ukwa wamesema. Kwani sisi tunawatakasa ‘Aliy bin Abi Twaalib na Al-Hasan na Al-Husayn na Ja’afar na Muhammad na Musa na Ali na Muhammad Al Jawad na wote hawa (RAnhum) kuwa haiwezekani wao kuyatamka haya.
Sisi tunawatakasa wote hawa kuwa hawawezi kusema uongo kama huu waliowazulia, lakini ninachokusudia ni kuwa haya ndiyo yaliyomo ndani ya vitabu vyao.
Kwa hivyo anaeleza Al-Kulayniy katika kitabu cha Al-Kaafiy kutoka kwa Ja’afar bin Muhammad anayejulikana kwa jina la Ja’afar Asw-Swaadiq (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa amesema:
“Hakika Allaah aliwaambia Malaika: ‘Mubaki penye kaburi la Al-Husayn mpaka mtakapomuona akitoka (kutoka kaburini pake) hapo mumnusuru na mulie kwa ajili yake na kwa ajili ya yaliyokupiteni katika ushindi wake, kwani nyinyi mumehusishwa kwa ajili ya kumnusuru yeye na kumliliia.”
Kisha anaendelea kusema:
“Malaika wakalia kwa huzuni kubwa kwa yale yaliyowapita kwa kukosa kumnusuru. Na atakapotoka (kaburini pake) watamnusuru (watapigana kwa ajili yake).”
Na ‘atakapotoka’, wanakusudia pale atakapotoka Al Mahdi Al Muntadhir wanayemsubiri maana itikadi yao ni kuwa wakati huo na Al-Husayn atafufuka na kurudi tena duniani, na hapo ndipo Malaika watakapomnusuru.
Wao wanaitakidi kuwa pale atakapokuja huyo wanayemsubiri, na Maimamu wote waliotangulia watatoka na kuwa pamoja naye.
Haya yamo ndani ya kitabu cha Al-Kulayniy kiitwacho Al-Kaafiy Juzuu ya kwanza ukurasa wa 284.
Na Itikadi yao hii ya mtu kufufuliwa tena hapa duniani ni itikadi tukufu sana kwao inayokwenda kinyume na maneno ya Allaah kama mlivyoona.
ITIKADI YA PILI
Kauli zao kuwa Masahaba wote walirtaddi (walitoka katika dini ya Kiislamu isipokuwa wachache sana)
Imesimuliwa na Al-Kulayniy katika kitabu cha Al-Kaafiy kutoka kwa Muhammad bin ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na umaarufu wake ni Muhammad Al Baqer kuwa amesema: “Watu wote walirtaddi baada ya kufariki kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa watatu (tu).”
Ar-Rawdhah katika kitabu cha Al-Kaafiy ukurasa wa 246
Na imeandikwa humo pia kuwa Muhammad bin ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:
“(Al Muhajirin) Watu wa Makka na (Al Ansar) watu wa Madina (wote) walitoka katika dini isipokuwa watatu (tu).”
Al-Kaafiy – Juzuu ya 2 ukurasa wa 244
Amesimulia huyo huyo Al-Kulayniy katika kitabu cha Al-Kaafiy kutoka kwa Muhammad bin Ja’afar kuwa amesema:
“Watatu Allaah hatosema nao siku ya Qiyaamah na wala hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo
1- Kila anayeukataa uimamu wetu unaotoka kwa Allaah,
2- na kila anayemkanusha Imamu aliyeletwa na Allaah
3- na kila anayesema kuwa watu wawili hawa ni Waislamu.”
Watu wawili wanaokusudiwa katika hadithi hii ni Abu Bakr na ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu). Na maana yake ni kuwa kila anayesema kuwa Abu Bakr na ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) ni Waislamu basi Allaah hatosema naye wala hatomtakasa siku ya Qiyaamah na atapata adhabu iumizayo.
Hadithi hii imo katika kitabu cha Al-KaafiyJuzuuu ya kwanza ukurasa 373
ITIKADI YA TATU
Kauli yao kuwa kila asiyekuwa Shia ni kafiri – watu wote ni makafiri isipokuwa Mashia. Na yareti kama wangenyamaza hapo, bali wameendelea kusema kuwa: Kila asiyekuwa Shia ni kafiri na ni mtoto wa zina .
Amesema Bin Babawayh, na huyu ni katika maulamaa wao wakubwa wa elimu ya hadithi kuwa:
‘Kila anayemkanusha Imam anayesubiriwa, ukafiri wake ni mkubwa kupita hata wa Ibilisi – Yeyote anayemkanusha imamu ‘asiyeonekana’, ukafiri wake mkubwa kupita wa Ibilisi.”
Ikmalu ddin – Ukurasa 13
Ameeleza Al-Kulayniy katika Al-Kaafiykutoka kwa Muhammad al Baqer kuwa:
‘Watu wote ni watoto wa zina isipokuwa Mashia wetu.”
Na haya yamo katika Ar-Rawdhah - Al-Kaafiy ukurasa wa 239
Imesimuliwa na Al-Kulayniy katika Al-Kaafiy kutoka kwa Ar-Ridha kuwa amesema:
“Hakuna Muislamu isipokuwa sisi na Mashia wetu.”
Juzuu ya 1 ukurasa wa 233
Anasimulia Al-Kulayniy katika Al-Kaafiy pia kutoka kwa Ja’afar bin Muhammad Asw-Swaadiq kuwa amesema:
“Shetani huja na kukaa juu ya mwanamke sawa kama anavyokaliwa na mumewe, na hutenda kama anavyotendewa na mumewe na kumuingilia kama anavyoingiliwa.”
Muulizaji akauliza:
“Vipi tutaweza kutofautisha?”
Yaani vipi mwanamke anaweza kujulikana iwapo ameingiliwa na shetani au ameingiliwa na mumewe?
Akajibu:
“Kwa kutupenda na kutuchukia. Kila anayetupenda basi tone yake imetokana na binadamu, na kila anayetuchukia basi tone yake imetokana na shetani.”
Juzuu ya 5 katika kitabu cha Al-Kaafiy ukurasa wa 502
Amesema Ni’imatullah al-Jazaairiy – na huyu ni katika maulamaa wao wakubwa wa elimu ya hadithi katika wakati wake kuwa:
“Sisi hatuko pamoja nao – (anakusudia Masunni) hatuko pamoja nao katika Mungu wala katika Mtume wala katika Imamu, na hii ni kwa sababu wanasema kuwa Mungu wao ni yule ambaye Muhammad ni Mtume wake na Abu Bakr ni Khalifa baada yake – na sisi tunasema: sisi hatumuabudu Mungu huyo wala Mtume huyo, bali tunasema kuwa Mungu aliyemuumba Abu Bakr kuwa ni Khalifa wa Mtume wake, huyo si Mungu wetu, na wala Mtume huyo si Mtume wetu.”
Amesema haya katika kitabu kiitwacho: ‘Al Anwar Al Nuamaniyah – Juzuu ya 2 ukurasa wa 278
Anasema Al-Huuru Al-’Aamiliy kuwa:
‘Ni’imatullah al-Jazaairiy ni mtu mwema, mwanachuoni, na mfanya tahakiki mkubwa sana.’
Amesema Al Khansariy:
‘Niamatullah alikuwa miongoni mwa wanachuoni wetu wakubwa sana na alikuwa bahari ya elimu katika wakati wake katika lugha ya kiarabu, na katika elimu ya Fiqhi na ya Hadith.’
Na Al Tijani ambaye ni mwanachuoni wao mkubwa katika zama hizi anasema:
‘Mungu aliyeridhika kumfanya Abu Bakr kuwa Khalifa baada ya Mtume, sisi hatumtaki Mungu huyo.”
Ameyasema haya katika mhadhara alioufanya huko London na kaseti yake tumeihifadhi