Nani kakwambia shahada inatoka katika vitabu vya Mashia ? Quran ndio imemkiri Allah na Mtume wake sasa unataka shahada kutoka vitabu vya kishia huu ni ukichaa mkubwa , Shahada ni Allah na mtume wake iwe shia iwe wahabi iwe nani usipende kupikia watu maneno
Nacheka sana,hiki kina kirefu,pili nakukumbusha tu ukiona kuna sehemu yoyote nimekujibu "Poa" ujue nimekupuuza sababu nikiendelea kujadiliana na wewe lazima utaaibika.
Nakukumbusha tu,hapa unatakiwa uthibitishe Ushia kwamba ni Uislamu,sababu Mashia wapo na tunaishi nao waulize wao wana itikadi gani na kweli ni waislamu.
Maana hata makadiani wana dai wao ni waislamu,mashia kadhalika,hii ni kama kisa cha Laila,kila mtu anadai Laila ni mchumba wake lakini tukimuuliza Laila anakana.
Kijana,nilitaka nikupuuze ukadhani naogopa,nilitaka kukuacha sababu hujui lolote. Sasa nataka unionyeshe Uislamu wa Mashia toka kwenye vitabu,kabla sijakuwekea vitabu vyao nikuonyeshe wanajipambanua vipi.
Qur'aan haijataja jina Ushia wala Usuni na kila kitu kina asili yake na lazima turudi kwa wenye hizo nisba.
Nataka unionyeshe hiyo shahada katika vitabu na mashia wanasemaje ? Si umejinadi una ushahidi kijana ? Nataka unionyeshe wapi mshia anashuhudia kwa shahada hiyo ?
Nipo ..