Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

Mkuu hii salamu Haina msingi wa kuitegemea.

Huyo Jamhuri hafahamiki ni nani.

Kwanini Rais anahofia kusalimia wananchi Kwa kuzitambua dini zao au tamaduni zao??

Kama anaona soni kusema Asalam Aleykum au Bwana Yesu Asifiwe basi aseme tu Habarini za saa hizi ma bibi na mabwana.

Huyo Jamhuri ndio nani??
Mkuu hii salamu inafikirisha sana.
 
Sio lazima asalimie jinsi mtanguliz wake alivyokuwa anasalimia, anaweza kusalimia kama Mkapa pia.
Asalimie kwa salamu za dini za Watanzania kama alivyofanya mtangulizi wake na hiyo iwe ndiyo sala ya kufungua mkutano. Hakuna haja ya kuwaita viongozi wa dini wasali tena. Tunapoteza muda kwani wanatoa hotuba badala ya sala fupi.
 
Eti kazi iendelee Hiki nini Hiki?

Wakiwa na mwendazake katika kunadi sera zao walitumia neno hapa Kaz tuh, mwendazake kashaenda zake,yeye anasisitiza muendelezo wa Kaz,Kaz iendelee,sasa ww unaumia kitu gan hapo?
 
Una point hapo. Sasa Rais lazima kupenda na kuheshimu dini za wananchi wote. Basi anagalau abadilishe kidogo aseme ""Msifuni Yesu Kristu!"
Aseme msifuni yesu Kristu Kwan yupo kanisani yeye?

Ukimsifu wewe Kristu wako inatosha,na samia asipomsifu Kristu Kwan anapungukiwa kitu gan huyo kristu
 
Aseme msifuni yesu Kristu Kwan yupo kanisani yeye?

Ukimsifu wewe Kristu wako inatosha,na samia asipomsifu Kristu Kwan anapungukiwa kitu gan huyo kristu
Kwani Magufuli alipokuwa akisalimia Asalaam Aleikhum! Bwana asifiwe! Tumsifu Yesu Kristu! alikuwa kanisani? Ni salamu walizozoea Watanzania, na hazina ukakasi. Tumeshauri Mama azitumie badala ya secular salutation that is followed by lengthy prayers.
 
Hii nchi ni secular na salamu zake zinapaswa kuwa secular.Sijui kwa nini huwa wanawake mambo ya maombi kwenye shughuli za serikali

Mkuu, nchi ni secular ila wananchi wake wana dini. Ukiwasalimia kwa salamu za dini zao huondoi ule ukweli kwamba nchi ni secular. Nchi kuwa secular maana yake ni kwamba haiendeshwi kwa sheria za dini yoyote. Basi.
 
Daaaaah!.hii kitu ungejaribu kuliongelea vijiweni.humu unatukosea heshima ya JF.

Hukuwahi kuulizia utekwaji,mauwaji ya waandishi wa habari,ukamatwaji wa viongozi wa upinzani,na katiba kusiginwa.
Nijue tu unaelimu kiasi gani tuanzie hapo.
 
Hii nchi ni secular na salamu zake zinapaswa kuwa secular.Sijui kwa nini huwa wanawake mambo ya maombi kwenye shughuli za serikali

Hiyo habari ya nchi kuwa secular ni zuga tu.

Tangu enzi na enzi viongozi wa dini wamekuwa wadau muhimu wa watawala na ndio maana wana baraka zote za dola kuwatoza waumini wao kodi kwa mfumo wa zaka na wanasamehwa kodi nyingi za serikali.

Dola nyingi zinawatizama viongozi wa dini kwa jicho la ziada kwasababu ya ushawishi mkubwa walio nao katika jamii.
Penginepo, dini inakandamizwa moja kwa moja na nchi nyingine
sheria za dini zinatawala.

Huko kwetu, watawala wasio makini hawajaweza kuwa na msimamo wa kudumu juu ya nafasi ya taasisi za kiimani katika taifa.
 
Aseme msifuni yesu Kristu Kwan yupo kanisani yeye?

Ukimsifu wewe Kristu wako inatosha,na samia asipomsifu Kristu Kwan anapungukiwa kitu gan huyo kristu
Lakini Rais huyo huyo anashiriki sala za kumsifu Kristu baada ya salamu. Nimependekeza salamu za dini zote kubwa Tanzania zingekuwa sala ya kutosha. Baada ya hapo hakuna sababu viongozi wa kidini waitwe kusali tena.
 
Back
Top Bottom