isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,143
- 6,560
| Jamhuri ya Nicaragua, Republic of Nicaragua au República de Nicaragua ni taifa linalopatikana Amerika ya Kaskazini. Nicaragua yenye ukubwa wa 129,494 Square Kilometers sawa na 49,998 Square Mile's ni nyumbani kwa watu wapatao takribani millioni 6,625,560 kufikia 1 April 2020.
Bendera ya Jamhuri ya Nicaragua
Mji mkuu wa taifa hili ni Managua mji wenye kuhodhi shughuli za kiserikali, miji mingine iliyoendelea ni León, Granada, Matagalpa, Puerto Cabezas na Rivas. Granada ni mji wa biashara na mji wenye historia ya enzi za ukoloni wa Uhispania.
Lugha rasmi ya Nicaragua ni Kihispaniora, pesa rasmi ikiwa Nicaragua Córdoba / Gold Córdoba (NIO), Córdoba 1 ni sawa na Centavos 100.
Wito wa taifa hili (Motto) ni "En dios Confiamos" | "Tunaamini katika Mungu". Raia wa Nicaragua unaweza kumuita Nicoya, Nica au Pinolero.
Mji wa Managua
Nicaragua imepakana na Honduras kaskazini magharibi, Caribbean upande wa mashariki, Costa Rica upande wa kusini na bahari ya Pacific upande wa kusini magharibi.
Plaza de la Revolución
| Biashara, Uchumi, Maendeleo na Uwekezaji. Taifa hili linatambulika kama taifa maskini nyuma ya Haiti ndani ya Amerika ya Kati. Shughuli kuu za kiuchumi ni kilimo, biashara na utalii.
Cologne City, Granada
Shughuli za Kilimo na biashara hasa ya kahawa, nyama, sukari, karanga, mpira, pamba, dhahabu, tumbaku, vitambaa na malighafi za kuvalisha nyaya za vyombo vya moto zimekuwa zikisafirishwa nje kuelekea Marekani kwa asilimia 44.2%, El Salvador 6.4%, Venezuela 5.5% na Costa Rica 5.5%.
Kampuni za Nestlé na Starbucks zimekuwa chachu ya uchumi wa Nicaragua kutokana na kufuata kahawa moja kwa moja.
Karanga ya Nicaragua
Utalii ni moja ya sekta muhimu kwa taifa hili, utalii unachagizwa na uwepo wa milima ya volcano, miji ya kale, pwani na fukwe maridhawa, milima na maziwa yenye maji safi na tulivu. Maeneo makuu ya utalii ni Visiwa vya Corn, Masaya, Volcano Islet's of Granada, Mombacho, Momotombo Volcano, Ziwa Nicaragua na Managua.
Ziwa Nicaragua ni ziwa pekee lenye maji safi na tulivu (Fresh water lake) kuwa na papa ndani yake.
Otto Beach - Kisiwa kidogo cha Corn
Sehemu nyingine za kitalii ni León Viejo mji mkongwe ndani ya Amerika ya Kati. Uwapo Nicaragua utaweza kushuhudia nyota nyingi zaidi kuliko sehemu yeyote ile duniani.
Granada Grand Colón
| Elimu ndani ya Nicaragua ni bure! Kwa shule za awali, msingi na secondary huku elimu ya juu ikitolewa mikopo na bodi maalumu. Elimu ndani ya Nicaragua ina sheria na taratibu zake, elimu ya awali na msingi sio lazima kwa mwanafunzi kuvaa sare za shule, huku elimu ya upili (Sekondari) ikiwa lazima kuvaa sare za shule.
Palacio Nacional
Elimu ya juu inatolewa baada ya wanafunzi kuhitimu shule ya upili, mfano wa vyuo bora vinatoa elimu inayolenga zaidi elektroniki, mifumo ya tarakirishi, sayansi, sanaa, uchumi, sheria na kilimo ni Central American University (UCA), Central University of Nicaragua, Universidad Internacional de Agricultura na Universidad de la Integración de América Latina (UNIVAL).
| Burudani, Sanaa, Michezo na Habari. Taifa hili linavituo vya Radio na Runinga zaidi ya 100 (Vituo vya runinga vikisambazwa kwa mfumo wa Cable-TV). Nicaragua inayo magezeti yafuatayo La Prensa, El Nueva Diario, Confidencial na gazeti la mtandao The Nicaragua Dispatch.
Ndani ya Nicaragua mchezo maarufu ni baseball, ndondi na mpira wa miguu. Katika mchezo wa boxing Nicaragua ilitambulishwa vyema na Alexis Argüello aliyempiga bondia Max Hess wa Ujerumani kwa Knockout hali inayopelekea Mjerumani huyo kutolewa na gari ya dharura ukimbini.
Granada Castia VI
Muziki ndani ya Nicaragua ni suala la kitaifa huku ikiwepo dansi ya Nicaragua - Palo de Mayo inayochezwa na kila rika. Aina nyingine ya muziki ni salsa, bachata, merengue, cumbia na mziki wa asili unaochakatwa kwa kutumia marimba.
Nicaragua ni nyumbani kwa waandishi nguli Sergio Ramirez, Gíoconda Belli na Claribel Alegría.
Hii ndio Jamhuri ya Nicaragua 🇳🇮
Nakala: Rubawa mtu chake Bwanautam Farolito