Jamhuri ya Paraguay | República del Paraguay

Jamhuri ya Paraguay | República del Paraguay

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,143
Reaction score
6,560
| Jamhuri ya Paraguay, Republic of Paraguay, República del Paraguay au Tetã Paraguái ni taifa linalopatikana Amerika ya Kusini, likiwa na ukubwa wa eneo zipatazo 406,705 Square Kilometers sawa na 157,047 Square Mile's.

Paraguay Flag.jpg

Bendera ya Jamhuri ya Paraguay

Paraguay yenye idadi ya watu takribani millioni 7,252,700 kufikia Machi 20, 2020 mji wake mkuu ni Asunción, mji wenye kuhodhi shughuli za kiserikali na masuala baadhi ya kimataifa. Miji mingine mikubwa na iliyoendelea ni Luque, ni mji wa biashara wenye kuhodhi uwanja wa ndege wa kimataifa Silvio Pettirossi International Airport, makao makuu ya shirikisho la mpira wa miguu Amerika ya Kusini (CONMEBOL) na kambi kuu ya jeshi la Paraguay, Luque ndio mji wenye wageni wengi ndani ya Paraguay. Miji mingine bora ni San Lorenzo, Encarnación, Concepción, Villarrica, Pedro Juan Caballero na Ciudad del Este.

Paraguay Presidential Palace.jpg

Ikulu ya Rais wa Paraguay | © Paraguay Presidential Palace

Pesa rasmi ni Guarani (PYG). Guarani moja ni sawa na Centimos 100. Lugha rasmi ni Kihispaniora na KiGuarani (Guarani). Kauli kuu ya taifa hili (Motto); ni "Paz y Justicia" | "Amani na Haki".

| Uchumi, Biashara, Kilimo, Maendeleo na Uwekezaji.

Paraguay yenye kupakana na Argentina upande wa Kusini na Kusini Magharibi, Brazil - Mashariki na Kaskazini mashariki, Bolivia - Kaskazini Magharibi ni taifa lenye kuzalisha umeme upatao KWh billioni 63 kwa mwaka kupitia bwawa nambari mbili duniani Itaipu Dam.

River Rio Fly Over.jpg

Daraja la juu (Fly Over) la Mto Rio - Itapu Dam ©Muñoz Felipe

Pamoja na kuzalisha umeme mkubwa Paraguay imekuwa ikitumia KWh billioni 15 kwa mwaka pekee, kupelekea kufanya biashara ya usambazaji wa umeme katika mataifa ya Brazil, Argentina na Uruguay.

Asunción.jpg

Jijini Asunción | ©Visit Paraguay

Paraguay inashikilia nafasi kumi za juu katika kilimo cha soya, mbaazi, mahindi, ngano, sukari na uchakataji nyama.

Paraguayan Spurge.jpg

Mbaazi | ©Vianca Guarani Farms

Kupitia azimio la "Maquila Law" lililoweka sera bora za uwekezaji ndani ya Paraguay, imepelekea ukuaji wa kiuchumi kwa asilimia 7.2% kutokana na uanzishwaji wa viwanda vya Cement, Mavazi, Vifaa vya magari na vyombo vya moto na upembuaji madini.

Asuncion Patys Paraguay.jpg

Asunción Patys | ©Franz Ali

Taifa hili linalokuwa kwa kasi katika bara la Amerika ya Kusini ni nyumbani kwa soko huria na huru nambari tatu Ciudad del Este nyuma ya Hong Kong na Miami, FL.

Paraguay ni taifa lenye pwani, fukwe na bandari zinazopatikana katika mito mikubwa ya Paraná na Paraguay. Paraná - Paraguay ni mito inayotambulika kama "Corazón de Sudaméricana" | "Moyo wa Amerika ya Kusini".

| Elimu

Elimu ndani ya Paraguay ni bure na lazima. Asilimia 98% ya watoto kati ya miaka 6 hadi 12 wanafika shule, huku asilimia 93.6% ya raia wa Paraguay ni wasomi na asilimia 87.7% wanayo elimu bora ya kiwango cha sekondari.

Elimu ya juu ndani ya Paraguay inatolewa na vyuo, baadhi ya vyuo vyenye ubora ni;- National University of Asunción, Autonomous University of Asunción, Universidad Américana, Columbia University of Paraguay na The Federal University for Latin América Integration.

Basilica of Virgin Mary of Caacupé.jpg

Basilica of Caacupé | ©Visit Paraguay

The Federal University for Latin América Integration ni chuo cha mataifa kilicho katika mpaka wa Paraguay, Brazil na Argentina, kinachoendeshwa na mataifa matatu kwa ushirikiano.

| Michezo, Burudani na Muziki

Mchezo namba moja ndani ya Paraguay ni mpira wa miguu. Paraguay imekuwa ikishiriki vyema mashindano ya CONMEBOL, Copa América na Kombe la dunia.

Paraguay inayoshika nafasi ya 41 katika viwango vya mpira wa miguu duniani inawakilishwa vyema na Club Olimpia timu bora kutoka ndani ya taifa hili. Huku ikiwa nyumbani kwa mchezaji wa kimataifa Roque Luis Santa Cruz Cantero aliyetikisa ulimwengu mzima akiwa na vilabu vya FC Bayern München, Malaga, Blackburn Rovers na Manchester City, mchezaji mwenye historia ya aina yake ni Óscar Cardozo.

Roque.jpg

Roque Santa Cruz - Akiwa na Club Olimpia. ©Claró Sports

Wachezaji wa hivi sasa wanaoiwakilisha vyema Paraguay ni Blás Riveros - FC Basel, Fabian Balbuena - Westham United na gwiji wa kujiangusha na kujirusha kiwanjani Miguel Almirón wa Newcastle United.

Miguel Almirón.jpg

Miguel Almirón - Newcastle United © Cecilia Xara / Forbes

Katika Muziki Paraguay inawakilishwa vyema na mkongwe wa miondoko ya pop ya kilatini, bachata, mziki wa elektroniki mwanamama Giuli Mendoza maarufu kama Perla aliyefanya matamasha katika mataifa yapatayo 41 duniani kote, huku akiwa mwanamuziki pekee ulimwengu kufanya matamasha katika miji yote mikubwa ndani ya Brazil.

Ana Lucrecía Taglioretti alikuwa mpiga violini wa kimataifa kutoka Paraguay, atakumbukwa vyema kwa kupiga vilioni katika michezo ya Copa América 2015, Copa América Centanario na Fainali za Kombe la dunia ndani ya Urusi. Mwanadada huyu aliyetangulia mbele za haki, aliuacha ulimwengu wa tatu angali mdogo (Dec 25, 1995 - Jan 7, 2020).

Hii ndio Jamhuri ya Paraguay 🇵🇾
 
Shukran MKUU nimekoment nakulike nakusubscribe Akijaalia Muumba Ntaupitia Kesho Namalizia Kula Eid Kwanza Karibu na karibuni[emoji4]

Sent using My COVID-19
Shukrani! Eid Mubarak, kuwa na wakati mwema 😊
 
Du! mbona si mchezo
63,000,000÷2,100=30,000
Ina maana bwawa letu la kimkakati(la nyerere) linaingia Mara 30,000 kwa hili?au

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Itaipu Dam ni bwawa namba mbili duniani nyuma ya Three Gorges ya Hubei, China.

Itaipu Dam inahadi Production Studio maana bwawa hili huwaka rangi mbalimbali na maumbo mbalimbali, huku production team ikiendesha suala zima.

Lilijengwa kwa $19.6 billioni sawa na $48.2 billioni ya leo. Mwaka 2016 lilizalisha 103,098,366 megawatt kwa saa na kuweka record ya dunia ambayo haijavunjwa hadi leo.
 
Back
Top Bottom