Jamhuri ya Watu wa Kenya yaendelea kuwa Taa ya Demokrasia kwa majirani zake ikiwemo Tanzania

Jamhuri ya Watu wa Kenya yaendelea kuwa Taa ya Demokrasia kwa majirani zake ikiwemo Tanzania

Kwa mfano kwenye kampeni za Uchaguzi wa Tanzania wa 2020 , mabango ya barabarani yaliyoruhusiwa kubandikwa hata maeneo yasiyoruhusiwa , yalikuwa yale ya Mgombea Urais wa CCM tu.

Waliojaribu kubandika mabango ya Mgombea wa Chadema walikiona cha moto na zipo taarifa kwamba wako wengine wamepotea hadi leo hawajulikani walipo .

LAKINI KWA KENYA HALI NI TOFAUTI SANA , kila mgombea wa Urais ana haki sawa kabisa .

Mungu ibariki Jamhuri ya watu wa Kenya

View attachment 2277006
Uchaguzi hii mtajuta. Ngoja mmchague ruto muone kilele za madharau au makamu wa raisi awe martha karua muone sura yake halisi.
 
Yani umwage damu ili mwingine awe Rais? Ni kichaa ndo anaweza fanya

Sent using Jamii Forums mobile app

Acha mawazo ya kioga na hofu. Mbona Tanzania ilimwaga damu ili Obote awe Rais wa Uganda?. Akina samora Machel, Mondlane, Augustino Neto, Mugabe etc fought to gain power.

CCM inadharau wananchi wake kisa ni kondoo. Wananchi kondoo huzaa Viongozi Fisi na mbweha.
 
CCM Kuna kipindi watu walikuwa hawaachiani glass ya maji. Juzi almanusra mzee Mangula Makamu Mwenyekiti wa chama afariki kiss kawekewa sumu. CCM ya hovyo Sana na Bibi yao.
 
Aliyeharibu Uchaguzi wa 2020 ni Magufuli na tayari alikwishapata anachostahili. Mungu hakumuacha na amani kwa siku zote 114 kuanzia Oktoba 25, 2020 hadi Machi 17, 2021.

Siku zote alikuwa mtu wa kujikuna ngozi, kuishi kwenye mashine ya kupumulia, kutembea na catheter mkononi, kuropoka ovyo na kutukana. Na mwishowe maiti yake ikatembezwa barabarani mikoa 5 huku ikinuka

Bora aliondoka. Mimi nilivyoona dhiaka anayofanya kipindi anaapishwa pale Jamhuri dodoma nikajua huyu lazima atapata pigo ambalo linatokana na karma.

Huwezi kufanya ujinga wa namna ile ukaishi, Tanzania sio mali ya mtu uipeleke unavyotaka. That hate monger had to go.
 
Kwahiyo Demokrasia kwenu maana yake inaishia katika uchaguzi tu, vipi kuhusu kabila tatu pekee kuwa na haki ya kuongoza nchi?, vipi kuhusu 75% ya ajira serikalini kuchukuliwa na kabilaba mbili pekee, vipi kuhusu ardhi kumilikiwa na familia za wanasiasa?. UN inasema Tanzania imeipita Kenya ktk Demokrasia, wewe na UN nani zaidi?
Tony254

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app

Acha uongo na utapeli. Yani UN ndio anaijua Tanzania kuliko mimi ninayeishi Tanzania?. Yani umemfumania mkeo gesti, halafu Kuna shehe au mchungaji anakwambia mkeo ametulia na wewe unakubali, kiss kasema mchungaji. Tanzania hatuna demokrasia ndio spika wa bunge na mahakama zipo compromised.

Bunge baadala ya kuisimamia serikali ipo kwa ajili ya kujikomba kwa serikali. Ndio maana spika aliyepita alitoa maoni yake tu akafurumushwa.

Kuhusu ajira na kumiliki Mali Hilo halihusiani na demokrasia huko ni utawala Bora ambako CCM ilishafeli kila siku ufisadi na kujuana. Mkwe waziri, mke mbunge na mtoto mbunge. Kuna kipindi baba na mtoto walikuwa wabunge.
 
Uhuru gani wa kujiamulia upo Kenya?, Kama ubaguzi wa ajira serikalini unawatenga wakenya walio wengi?, Mbona tume iliyoundwa kuchunguza dhuluma katika kumiliki ardhi ilishauri kurudisha ardhi yote walijimilikisha wanasiasa kurudishwa serikalini ili igawiwe kwa wananchi lakini imeshindikana, huo uhuru wa kujiamulia ni upi?

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app

Kuwa na Tume ya kutoa mapendekezo Kama hayo hapa Tanzania ipo?. Tume zote zipo kuifurahisha CCM . Watu walipeana mablioni ya pesa wakaitwa kwenye kamati ya maadili wakajibu kwa dharau billioni mbili Ni pesa ya mboga.

Mafisadi wa escrow, kagoda, Richmond, EPA, wmefanywa Nini?. Tanzania haina demokrasia na ufisadi ndio upo juu. Tumekosa vyote
 
Je unaweza kuwa Jobless , alafu ukawa na furaha?
Russia ajira nje nje kwa wazaliwa

Umefika Russia au unaongea tu. Ajira zipi zipo Russia. Nenda chechnya waulize magumu waliopitia Chini ya Putin.
 
Gadaffi alikuwa Dikteta Ila nchi ikawa Ina maendeleo.
Vyama vya upinzani wanaotaka demokrasia kwa mgongo mabeberu walipoweza kuipata hio demokrasia hakuna maendeleo tena huko Libya

Huwezi kuongoza wanadamu Kama inaongoza mbwa kwa kumpa chakula huku umemfunga mnyororo.

Ghadafi ndio aliiharibu Libya. Aliiongoza Kama Mali binafsi na kuita wakosoaji mbwa. Mwisho wa siku yanayotokea Leo ndio aliyataka. Ghadafi alitakiwa alete Mapinduzi ya kisiasa na kuandaa mtu wa kumridhi na kuruhusu Uhuru wa kuchagua. Leo tungeongea mengine.
 
Siyo kweli hata kenya kuna kaupendeleo kwa wagombea hawa wawili tu. Hata vijiwe vya kubashiri mshindi (kama akina redet) wanawataja hawa wawili tu, wagombea wengine kama profesa bangi (wajackoyah) hawatajwi.

Kwa uchaguzi wa mwaka huu wagombea wenye nguvu ni wawili tu. Hao waengine wawili hawana nguvu Sana, labda kidogo wajakoyah ingawa ushawishi wake unapungua kidogo.

Tanzania hamna kitu sisi tuendelee kuendeshwa na CCM mpaka siku ya mwisho maana tunaibudu CCM acha itutawale.
 
Wewe Acha ujinga, ilikuwa ukabila sio kutafta hdaki.

Uwe mwelewa Yale mapigano chanzo kIlikuwa kutafuta haki baada ya uchaguzi wa 2007 kuibiwa. ODM na PNU. Bila vile serikali ya Umoja wa kitaifa isingekuwepo. Mapigano Yale msingi wake ulikuwa uchaguzi. Kalenjin ODM Ruto v Kikuyu PNU Kibaki na Uhuru
 
Haki ipi wewe kila matokeo ya kitoka utasikia vilio kura zimeibiwa, wewe una sahau haraka uchaguzi uliopita huyu Odinda aliapishwa kuwa rais wa watu akijitangazia ushindi, huku Kenyatta akiwa rais wa dola akitangazwa na tume ya uchaguzi , acha uvivu wewe

Hiyo ndio demokrasia Sasa unajitangaza Rais, na bado unapeta uraiani. Sio huku Tanzania kuwa mfusi wa CHADEMA Ni kosa la jinai. Mikutano imepigwa marufuku miaka Saba Sasa kisa kuiua CHADEMA.

Huku Tanzania watu wanaiogopa CCM wakati Kenya Vyama vinne tofauti vimewahi kukamata serikali. KANU, NARC, PNU na Sasa Jubillee na Kuna uwezekano kingine kikaongezeka Azimio au UDA Kenya kwanza.

Demokrasia inadhihirisha kwa kubadilisha vyama madarakani.
 
Hiyo ndio demokrasia Sasa unajitangaza Rais, na bado unapeta uraiani. Sio huku Tanzania kuwa mfusi wa CHADEMA Ni kosa la jinai. Mikutano imepigwa marufuku miaka Saba Sasa kisa kuiua CHADEMA.

Huku Tanzania watu wanaiogopa CCM wakati Kenya Vyama vinne tofauti vimewahi kukamata serikali. KANU, NARC, PNU na Sasa Jubillee na Kuna uwezekano kingine kikaongezeka Azimio au UDA Kenya kwanza.

Demokrasia inadhihirisha kwa kubadilisha vyama madarakani.
Mtu ana vunja katiba wewe unaita demokrasia? unajitangazia Urais kisha una jiapisha wakati mamlaka hayo ni ya tume ya uchaguzi, huu upuuzi hauwezi kuwa demokrasia, lazima ushughulikiwe ufundishwe katiba ndio muongozo
 
Uwe mwelewa Yale mapigano chanzo kIlikuwa kutafuta haki baada ya uchaguzi wa 2007 kuibiwa. ODM na PNU. Bila vile serikali ya Umoja wa kitaifa isingekuwepo. Mapigano Yale msingi wake ulikuwa uchaguzi. Kalenjin ODM Ruto v Kikuyu PNU Kibaki na Uhuru
Demokrasia na usawa upo sasa mnauana kutafuta haki ipi? ndio maana ni kasema hakuna cha maana Kenya , ndio maana kila uchaguzi utasikia kura zimeibiwa, hata huu wa mwaka huu lazima Ruto au Odinga alie hadharani kuibiwa kura
 
Wakenya mlimwaga damu sio sababu ya demokrasia bali ukabila uliwatawala..
Tanzania itakuwangumu kumwaga damu sababu ya demokrasia maana tunatabia ya kupotezea mambo.
We don't care.

Pili hatuana siasa za kikabila.
 
Back
Top Bottom