SoC01 Jamii Forums: Habari Katika Kurasa Salama

SoC01 Jamii Forums: Habari Katika Kurasa Salama

Stories of Change - 2021 Competition

MWAG

Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
7
Reaction score
5
Unajua nini kuna mitandao ya kijamii ukiifuatilia utacheka sana wakati mwingine inasikitisha kwasababu waandishi hawana tena uweledi yaani hawaandiki tena uhalisia wa maisha wanaandika kile bosi anataka hii ni hatari kwani kwani waandishi ndo watu pekee wanao weza kubadili uongo uonekane kweli na ukweli uonekane uongo.

Lakini unajua nini, Jamii Forums ni mtandao pekee unaothubutu kuandika ukweli halisi wa maisha yaani kusema kweli katika kila hali. Yaani Jamii Forums sio kama page zile za YANGA NA SIMBA yaani ukiingia huko utacheka sana sema utahuzunika pale utapojionea uhalisia wa mambo. Yaani hizi page zipo bize kujisifia wanajisifia hadi wanakosea wakibadili stori ni kuwaponda watani zao wa jadi yaani kila mtu anasubili mwenzake akosee hapate cha kuandika yaani simba akizingua hii ni stori kubwa huko katika kurasa za Yanga na hata Yanga akizingua kwenye kurasa za Simba ni bonge la stori. Lakini Simba akifanikiwa utadhani Yanga haoni na hata Yanga akitusua utakuta Simba hana habari zaidi zaidi yuko tayari kuficha takwimu ili tu mwenzake aonekane yuko hovyo kama alivyo fanya yule msemaji wa Simba enzi (Haji Manara) alipotoa takwimu za makombe ambayo Simba amechukua na idadi ya makombe ambayo Yanga amechukua zikionyesha Simba amechukua idadi kubwa ya makombe kuliko Yanga lakini leo yupo Yanga anadai zile takwimu sio sahihi na kwamba yeye ndio alihusika kuziandaa na kwa msisitizo anadai alikuwa amelewaa.Yaani kama wewe ni mgeni Tanzania utabaki mdomo wazi lakini kwa wenyeji ndo kwanza watagonga like na kukuambia Bongo siami raha sana.

Yaani hawa jamaa katika mafanikio utadhani hawapo hapa.Lakini mmoja wao hawe na hali ngumu utabaki unashangaa hawa jamaa wametokea wapi ni wengi balaa na stadi wa kuwacheka wenzao. Hii ni nzuri maana inasaidia mwanayanga halali anajua akizembea tu atachekwa na Simba hivyo hivyo wanafanya kazi usiku na mchana wakihofia kuchekwa na mtani ni afya kwa maendeleo ya mpira wetu.

Ni mbaya pale tu wanapotakiwa kushirikiana yaani hawawezi kabisa hata kusogeleana mara ya mwisho nakumbuka walishirikiana ilikuwa ni katika kombe la kagame(CECAFA)ilikuwa ni katika jitihaada za kudai maslai zaidi baada ya simba na yanga kukutana nusu fainali wakapanga kugoma kushinikiza kupewa pesa zaidi na CECAFA ya enzi hizo katibu wake akiwa Nicholaus Msonye nadhani unamkumbuka huyu jamaa walidai hivyo maana mechi yao ingeingiza pesa nyingi sana.Basi bwana wakapanga mipango pamoja wakutane hotelini kugomea nusu fainali hiyo Yanga akajikuta amegoma pekee yake na kilicho mkuta mimi sikusimulii Simba yeye akatimba uwanjani akapewa ushindi wa mezani enzi hizo Hassan Dalali akiwa mwenye kiti wa SIMBA .

Siku hizi hamna unafiki kabisa wapinzani wa Yanga wanapokelewa vizuri na Simba kama wale River United nasikia walipokelewa na Simba kwa madai kuwa wanalipa kisasi cha Yanga kuwapokea Plateu united nayo ya uko Nigeria ingawa mimi sikuona ila nilicho shuhudia ni yule mshambuliaji wa aliyevaa jezi ya Simba akidai ana ndoto za kuja kuchezea simba siku moja lakini na fikiri unaikumbuka pia ile ya kiongoziwa Yanga Hersi Saidi kuvaa jezi ya Kaizer Chief ya huko Afrika Kusini sio hiyo tu kuna hile ya kocha wa Yanga enzi hizo Mwinyi Zahera kutoa ushirikiano wa kutosha kwa As Vita ya kwao Congo pindi wamekuja kucheza na Simba.

Sio mbaya wakirudi kwao wanasimulia mapokezi yetu na kudai kuwa kwa Tanzania ni wakarimu na mpira kwao sio vita ina tutambulisha hivyo bongo bana raha sana ndo hakuna anaye takakuhama
Hachana na hao sasa kuna hawa wana siasa kurasa za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kule Bungeni hadi mitandaoni kazi yao ni kuunga MKONYO hoja hadi nakosea huku wakiimba ule wimbo wao maarufu wa tuna imani na Rais na siku hizi wana msemo wao wa kazi iendelee raha sana.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wao kazi yao eti ni kuikosoa serikali kwa kigezo cha mbadala si Bungeni sio mitandaoni hawana mda wa kusema ukweli. Mara ya mwisho nisikie CHADEMA wanaiunga mkono serikali ilikuwa ni kipindi UVIKO19 inaingia Tanzania wakahaidi kushirikiana na serikali bega kwa bega katika vita ya kupambana na ugonjwa huo ilikuwa enzi za Hayati Magufuli lakini hata hivyo walishirikiana basi walitofautiana mazima.

Ingawa kuna faida zake inasaidia serikali kuwa makini maana wakiteleza watawabariki CHADEMA cha kuongea inakuwa na afya mara mia kwa Demokrasia ya nchi yetu. Lakini shida ni pale unapo hitajika umoja wa kitaifa katika shughuli za maendeleo ngumu sana kushirikiana yaani tunapingana hadi katika mambo ya msingi maana lile somo la maendeleo hayana chama lilitupita mbali sana.

JAMIIFORUMS sio kama zile page za motivation speaker ambayo mara nyingi wanawaaminisha watu mambo makubwa tofauti na uhalisia kawaida sana kusikia eti mtu alianza na mtaji wa elfu tatu (3000) kwa kuuza ubuyu na kwa sasa hana mtaji wa milioni kumi na tano na zaidi yaani ili mradi tu watu wahamasike. Ni nzuri maana inasaidia watu wahamasike na kuthubutu hata katika nyakati ambazo sio rahisi wao kufanya hivyo na wakiwa na malengo makubwa wanafanikiwa japo kupiga hatiua ingawa sio kwa kiasi kile walicho kusudia. Yaani akiwa na mtaji huo wa elfu tatu anaweka malengo ya milioni kumi tano lakini walau anafika kwenye laki moja hapo tunasema tayari kapiga hatua.

Tatizo ni pale tu mtu usipo mwambia ukweli yaani uhalisia juu ya jambo fulani anapoingia katika uhalisia anashindwa kupambana na inakuwa ni rahisi sana kukata tamaa na kujiona yeye kama mtu asiye na uwezo "hopeless" na ndipo anapo pata somo jipya la maisha ya kwenye makaratasi na maisha halisi yapo tofauti.

Kwa ushauri wangu hili ni swala la kulitazama upya kwa waongeaji wa kuhamasisha SIJAJUA WANAFUNDISHWA NINI DARASANI lakini ni vizuri kuongea uhalisia zaidi kuliko kufarijiana zaidi yaani wanawapa watu maono makubwa sana tofauti na uhalisia wa maisha kwahiyo unapopata matokeo hafifu unajidharau sana kwamba wewe ni mzembe sana au kudharau wengine kiuwa wao ni wazembe kumbe maisha ni kitu tofauti kabisa kama walivyosema wahenga mipango sio matumizi ni kweli maana wakati nipo kidato cha tatu nilikutana na motivation speaker aliye tupa hadithi yake ya maisha alikuwa stadi wa kusimulia jambo lililo tufanya tuhamasike kumsikiliza alisema kipindi anamaliza chuo ajira zilikuwa za shida sana hali iliyo mfanya abuni njia ya kupata pesa kwahiyo akati anasubiri ajira alitafuta mkokoteni (toroli) akalitumia kukusanya taka mtaani na kuwalipisha wenye taka zao kwa shilingi mia mbili hadi mia tano aliendelea hivyo hadi akafanikiwa kununua gari dogo la kubebea taka badae akanunua gari kubwa na akatuambia kwa sasa ana magari matatu makubwa na anaendelea pia na hiyo biashara achilia mbali gari yake ya kutembelea tulibahatika kuiona nayo pia akadai ni zao la hiyo biashara yake aliyo ibuni na kwa sasa yeye ataki tena kuajiriwa. Tulijifunza mengi katika hadithiyake aliyo hipa jina zuri la from ZERO TO HERO

MOSI; Kuwa elimu haina umuhimu wowote katika maisha maana ni ukweli kuwa akutuonyesha umuhimu wowote wa elimu ilivyomsaidia kuwa mtu mkubwa mwenye mafanikio zaidi alituambia kwasasa hataki kuajiriwa yaani maana yake ni sawa na kutuambia alichoma vyeti vyake moto na sisi anatushauri tusisome hilo nalo neno.

MBILI; Katika maisha kikubwa ni ubunifu ukiwa mbunifu basi utafika mbali sana kwa kuanzia chini kabisa na kufika juu kileleni.

TATU; Alituonyesha namna maisha yalivyo mepesi sana na jinsi hela zilivyo nje nje na ni kama ametushauri tuache shule tuzifuate jambo la ajabu sana

LA MWISHO;nililojifunza ni wale wote wasukuma mikokoteni kule mjini niwazembe na hawana akiliya maisha maana wengi wao wanaishi nyumba za kupanga wakati mwenzao ni mtu mkubwa sana mwenye mafanikio makubwa sana kwa kipindi kifupi tu.

Tuache hayo tuje hapa nikuambie kwanini nasema KALAMU YA JAMII FORUMS KATIKA MIKONO SALAMA yaani hapa ni mahali nilipo hisi utofauti sana katika nyanja ya habari ni mahali ambapo wamefanikiwa sana katika nyanja ya habari

MOJA; Hapa amna ushabiki ule wa simba na yanga wao wanatoa habari sahihi kwa wakati sahihi hawaachi kuripoti jambo zuri walilo fanya SIMBA wala hawaachi kuripoti jambo zuri walilo fanya YANGA WAPO KATIKA USAWA kwa hili naomba niwapongeze sana labda ushauri wangu tu kitu wanachotakiwa kuongeza hapa ni uchambuzi wa mechi mbali mbali hii itasaidia sisi wanamichezo kujisikia nyumbani pale tunapo pata moja mbili tatu kutoka kwa wachambuzi mbalimbali na hili sina shaka na uongozi wa jamii forum kuwa wakiamua kulifanya watafanya kwa ustadi mkubwa na kutafuta mtu sahihi sio mwenye mapenzi na timu furani bali ni kupata mtu sahihi ,mwenye kufuata weledi katika kazi yake.

MBILI; Huu mtandao hautumiki kisiasa na sisi katika hili ni mashaidi JAMIIFORUMS inaripoti habari zote za kisisa kwa haki na usawa sio zile za chama tawala wala za vyama vya upinzani wameriporti kwa usawa kabisa bila kuacha kitu kongole nyingi kwao maana wametutendea haki katika ili wametujari sana yaani wametupa habari sahihi na sio za upendeleo wala za uonevu hongolreni sana kwa kuwa muhimili mzuri wa kitaifa hata pale wanapo yumbishwa wao usimama katika weledijambo la kujivunia hili kwa kuwa hadhina ya taifa labda katika hili ninalo la kuwashauri pia tukipata wachambuzi wa kisiasa pia waliobobea litakuwa jambo zuri na lenye tija cha msingi tu wasiwe wanaegemea upande mmoja itapendeza kama tu watatumia weledi wao vizuripi mngetuwekea mahojiano ya kisiasa.Haya mambo yangesaidia kuimarisha demokrasia.

TATU; Elimu inayotolewa hapa juu ya mambo mbali mbali nijambo la kuipongeza page yetu pendwa,uongozi na wahalili wa jamii forums kwa ujumla wamekuwa wakitoa elimu juu ya mambo mbalimbali yanayotufanya tukue zaidi kiakili na kuwa salama kiafya.Elimu juu ya sheria mbalimbali za nchi inasaidia uma wa watanzania kujua sheria na haki zao za msingi katika mambo mbali mbali na kujua jinsi gani wanaweza kuyatetea na kutafuta haki zao za msingi.Pia elimu juu ya maswala mbalimbali ya kitechnolojia inasaidia sana watumiaji wengi wa mtandao kujua namna ambavyo wanaweza kutumia mtandao kiusalama zaidi na kuepuka utapeli wa mtandaoni na mambo mengine maana mtandaoni kuna mengi aisee sio tu wizi wa mtandaoni lakini unyanyasaji wa mtandaoni sio jambo dogo.Elimu pia ya afya jinsi ya kujikinga na UVIKO19 ni jambo linalo omyesha fika uongozi huna nia ya dhati kutuweka salama watanzania na janga hili hatari na kuakikisha jamii nzima inabaki salama

HITIMISHO; LABDA niitimishe tu kwa upongeza uongozi mzima wa JAMIIFORUMS kwa namna wanavyopambana kutuhabarisha katika nyanja mbalimbali katika siasa,Demokrasia,michezo na burudani na pia katika swala zima la utoaji wa elimu lakini pia nashukuru kwa uanzishwaji wa shindano hili japo jambo nililo liona ni gumu kwangu walau idadi ya maneno ipungue maneno 1500 ni mengi sana ukizingatia pia watanzania wengi ni wa vivu wakusoma LAKINI KWAKO MDAU NAOMBA KURA ILI NIWEZE KUSHINDA SHINDANO HILI LAKINI PIA NINA MENGI YA KUJIFUNZA KUTOKA NIPO TAYARI KUSOMA USHAURI WENU KATIKA COMMENT AHSANTENI NA USISAHAU KUNIPIGIA KURA
 
Upvote 1
NAOMBA KURA YAKO MPENDWA JAPO SISTAHILI
 
Back
Top Bottom