Mkalibari
JF-Expert Member
- Mar 20, 2012
- 659
- 399
mkalibari. Do you know what is satan?
Yes i know boss, u?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mkalibari. Do you know what is satan?
Satanic version of creation,
Mimi mwanadamu sikutoka huko unapo pasema wewe, mimi nimetokana na baba ADAM alie umbwa directly na Mungu mwenyewe, sasa unaponiletea hizo blah blah zako sikusomi kabisa!
BTW sisi tumuaminio mungu tumeshataadhalishwa na watu kama nyinyi kua mtakuja na singeli zenu nyingi tu kuhusu kutaa Uumbaji wa mungu, pia tuliambiwa kua huwa amridhiki mpaka muoneshwe facts kwa kuona au kugusa...
Najua utakuja na hoja za kwamba dhibitisha kama mungu yupo, sijui nani alimuumba mungu, sijui mwambie mungu abadilishe uelekeo wa jua n.k
Kabla hujauliza ntakwambia kua Mungu hua alekezwi cha kufanya na stupid lizard kama wewe, he does at his will!
Najua mta/utanishangaa kua mbona kama nimeandika nje ya mada na hata kujibu maswali ambayo bado hayajaulizwa!
Trust me, hii mada ndiko inakoelekea...
Naomba unisaidie kuoanisha hiyo stori yako na "Human Races". Kwanini duniani kuna races nyingi za wanadamu...mfano, Blacks(Africans), Arabs, Whites, Indians, Asians(Eastern Asians), etc
Also, story yako inazungumzia wanadamu tu but ina-ignore viumbe wengine kama Tembo, Simba, Penguin, Ndege wa aina mbalimbali, samaki wa aina mbalimbali, etc.
Mbona niliweka yote imekuwaje ipo nusu?
Any way.... Ngoja niiendeleze hapa hapaa
Ni ndani ya mfululizo huu alimozaliwa binadamu....
Uhai hapa duniani uliletwa kutoka katika Constellation ya Lyra. Hawa viumbe wa Lyran Humanoids ni Wenye bidii sana katika kueneza uhai ulimwenguni miongoni mwa Jamii za Humanoids. Viumbe hao ndio waliuhamisha uhai wa kimazingira (environment ecosystem) kutoka sayari yao kwa maana ya mimea, wanyama, hewa yenye bacteria nk kupitia vyombo vyao vya anga za juu vilivyojulikana kama Makerubi. Waliandaa mazingira vizuri na kuotesha uhai wote wa kiikolojia. Kama desturi ya nyakati zote waliwafanyia cloning watoto wawili wadogo mmoja wa kiume na mwingine wa kike kutokana na jamii yao ili waweze kuwiana vya kutosha na mazingira yao mapya ya maisha.
Viumbe hawa waliwaandalia mazingira mazuri ya kuishi ndani ya bustani na kuwaweka humo. Watoto hawa wadogo walihitaji usimamizi mwingi kutoka kwa Wazazi wao na kwa hiyo, viumbe hawa wa Lyrans waliwatembelea hapa na pale ili kuangalia makuzi yao. Hatimaye waliridhika kwamba ni watu wazima na hivyo wakawakabidhi rasmi utawala wa dunia kama sayari yao.
Ugomvi mkuu waibuka baina ya Humanoids na Reptoids.
Muda mchache kabla ya Lyrans kupanda uhai duniani ugomvi mkubwa ulikuwa umetokea baina ya Jamii hizi mbili yaani Humanoids wa Lyrans na Reptoids wa Alpha draconians. Ugomvi huu uliletwa na Reptoids wa Alpha draconians waliotaka kuzimiliki baadhi ya sayari za Humanoids wa Lyrans ziwe makao yao ya kuishi. Viumbe hawa walikuwa katika galaxy moja japo nyota mbali mbali. Reptoids hawa wa Alpha walipoiona sayari ya Bila walivutiwa kabisa na mazingira yake nao wakawa wamenuia kabisa kuichukua sayari hiyo. Humanoids hawa wa Lyrans waliomba kwanza kuwajua vizuri kabla ya kukubali ombi lao kwa kuwauliza swali kwamba tungependa kwanza tuwajue vizuri, je ninyi ni watu wa aina gani?
Swali hili lilipokelewa kama kauli ya kukataliwa na matokeo yake ndani ya muda mfupi walizusha vita kubwa dhidi ya sayari hiyo ya Bila sayari ambayo ilikuwa imewavutia sana Reptoids hawa. Ndani ya muda mfupi sayari tatu miongoni mwa sayari kumi na nne za Humanoids wa Lyrans zilikuwa zimeharibiwa vibaya sana. Sayari zilizokuwa zimeharibiwa ni Bila, Teka na Merok. Humanoids wa Lyrans walikuwa ni wakulima, hawakuwahi kujishughulisha na silaha za maangamizi, walikuwa ni viumbe wapole sana,hawakuwahi kujishughulisha na vita ya aina yoyote. Kwa hiyo waliangamizwa sana. Msaada mkubwa wa katika vita hiyo uliletwa na Humanoids wanaojulikana kama Arcturians. Humanoids hawa wa Arcturus wana upendo sana, wameboresha sana teknolojia yao kwa ajili yao lakini zaidi sana kwa ajili ya jamii zingine. Kwa hiyo pia hujulikana kama Walinzi wa mbingu. Humanoids hawa wa Arcturians walipoingia katika vita hiyo waliwaangamiza vibaya sana wale Reptoids hao wa Alpha draconians na kuwafanya wakimbie kurudi kwao wakiziachia sayari hizo walizokuwa wamezishikilia. Ni katikati ya uhasama huo Reptoid mmoja alipojipenyeza hadi bustanini walimokuwa binadamu wa kwanza na kuamua kuwachochea kinyume cha Wazazi wao hao wa kimbingu. Ni kweli kwamba mambo mengi bado Wazazi hawa wa kimbingu wa wanadamu walikuwa hawajawaeleza bado, hii ni busara kabisa kutowaeleza mambo yote nje ya kiwango chao cha kustahimili. Lakini hili likatumiwa vibaya na draconian huyu kwamba Wazazi wao hao wa kimbingu hawakuwapenda wala kuwatakia mafanikio makubwa. Muunganiko huu wa binadamu na adui zao uliahirisha zawadi nyingi nzuri walizokuwa wapendelewe na Wazazi wao, mojawapo ni zawadi ya uhai wa milele. Zawadi hii ilitokana na jamii ya miti yenye kuleta uzima usio na kikomo. Kama nilivyoandika Jamii hii ya Humanoid Lyrans ni Jamii ya wakulima kwa hiyo muda mrefu walishagundua miti yenye kuboresha uhai wa mtu ambaye hajafanyiwa cloning ya uhai. Kwa hiyo walimuondolea zawadi hii kusudi asije kuutumia uzima wa milele vibaya kinyume na Wazazi wake. Na hivyo uhai wa milele wakaamua kuuweka miongoni mwa gharama za Mamlaka ya Nafsi, badala ya kuwa zawadi isiyogharimiwa.
Draconian huyu alipogundua kuwa amegundulika alitoroka na kurudi kwenye himaya yao ya Alpha draconians na kuwaeleza kile kinachoendelezwa hapa duniani na humanoid wa Lyrans na ubora wa sayari hii kama makao ya kuishi. Hivyo viumbe hao wa Reptoids wakaja kwa wingi wao pamoja na watumwa wao wa Zeta Reticulians ili kuwaangamiza Lyrans hao waliokuwa duniani na kuwaangamiza pia na binadamu ili kulipiza kisasi na kuichukua sayari hii. Lakini zoezi lao hilo halikufanikiwa kwa sababu kumbe viumbe wa Arcturians walishaweka kituo chao kisichoonekana cha ulinzi wa anga hizi za chini. Kituo hiki kisichoonekana kinachojulikana kama Athena, kipo Kati ya anga ya sayari ya Saturn na Jupiter. Reptoids hao wa draconians bila kujua uwepo wa kituo hicho waliangamizwa kabisa. Hivyo mpango wao wa maangamizi haukufanikiwa. Hata hivyo Reptoids hao waliobakia bila madhara walikimbilia duniani na kuwaambia Arcturians kwamba endapo watawafuatilia zaidi basi wao watawaeleza binadamu siri nyingi zaidi za ulimwengu, jambo ambalo binadamu alikuwa hajakomaa kuelezwa. Kwa hiyo Arcturians wakaamua kuwaacha wakae duniani bila kubughudhiwa tena. Arcturians wakawaacha maadamu hawana tena madhara ya kuangamiza Jamii ya binadamu. Hata hivyo Reptoids hao wala nyama walianza kuleta ghasia duniani kwa kutawala wanadamu kwa ukatili na mateso na kula nyama za wanadamu. Kipindi hicho katika historia ya wanadamu ndio chanzo cha masimulizi kuhusiana na Manefili pamoja na Mazimwi wala watu. Huo ukawa mwanzo wa binadamu kula nyama na kutoa Sadaka za binadamu
Ujio wa Humanoids wa Pleiades hapa duniani
Miaka mingi baadaye, wanadamu wakiwa wameongezeka duniani. Yapata miaka elf kumi iliyopita, kulitokea ujio wa viumbe wengineo wa Jamii ya Humanoids kutoka galaxy ya Pleiades. Viumbe hao ni watoto wa Lyrans kama ilivyo kwa binadamu. Kwa hiyo ni kana kwamba walisafiri hadi duniani ili kuona hao ndugu zao wa kibinadamu ni watu wa namna gani. Humanoids hawa waliishi duniani kwa muda mrefu kabisa na hata wakaamua kuishi kinyumba na mabinti za wanadamu na kuzaa nao watoto. Kwa vile ingawa viumbe hao ni kutoka sayari tofauti lakini ni specie moja tu ile ile ya anga nyingine, ndio maana waliweza kuzaa watoto. Hadi leo wanasayansi wanakubali kwamba kuna genetics mpya iliingia ghafla miongoni mwa binadamu. Genetics hiyo inapatikana wa ukanda wa Kaskazini mwa dunia. Kwa wenyeji wa Scandinavia, Sweden Na Norway. Wana wanakubali kwamba genetics hiyo iliingia ghafla katika Jamii ya binadamu miaka elfu kumi iliyopita. Wazazi wao kutoka Lyrans wakaamua kuwaangamiza wote watatu, kwa gharika ya maji yaani Terrans, Pleiades, na draconians. Kasoro tu kuhifadhi mbegu chache za wanadamu na wanyama.
Elimu maridhawa hii nimechagua kuiamini.
Mkuu kama kunachakuongezea endelea kutupa darasa.
Satanic version of creation,
Mimi mwanadamu sikutoka huko unapo pasema wewe, mimi nimetokana na baba ADAM alie umbwa directly na Mungu mwenyewe, sasa unaponiletea hizo blah blah zako sikusomi kabisa!
BTW sisi tumuaminio mungu tumeshataadhalishwa na watu kama nyinyi kua mtakuja na singeli zenu nyingi tu kuhusu kutaa Uumbaji wa mungu, pia tuliambiwa kua huwa amridhiki mpaka muoneshwe facts kwa kuona au kugusa...
Najua utakuja na hoja za kwamba dhibitisha kama mungu yupo, sijui nani alimuumba mungu, sijui mwambie mungu abadilishe uelekeo wa jua n.k
Kabla hujauliza ntakwambia kua Mungu hua alekezwi cha kufanya na stupid lizard kama wewe, he does at his will!
Najua mta/utanishangaa kua mbona kama nimeandika nje ya mada na hata kujibu maswali ambayo bado hayajaulizwa!
Trust me, hii mada ndiko inakoelekea...
Hadi Nahisi Kichwa Kina Uma Najiulza Mambo Ambayo Majibu Yanakuwa Magumu,
Kitu Gan Kilifanya Binadamu Kumwabudu Mungu? Ama Kwanin Kizaz Kimoja Kiabudu Kingine,
Pia Kumbuka Jacob Hakushnda Alipigwa Paja Na Huyo Kiumbe ,na Je Hawa Viumbe Wana Kiongoz Wao Kama Yupo Ni Nan?
Nisaidie Haya Kwanza Alafu Uendlee
Ok.
Tumalizie hiki kipande kidogo.... Cloning biological engineering ni teknolojia ya kurekebisha mifumo mbali mbali katika mwili wa kiumbe hai ili kiweze kuwiana na mazingira ya sayari husika. Hii ndiyo kazi tunayoiona katika masimulizi ya kitabu cha Mwanzo katika Biblia. Anayetajwa pale kuwa Mungu tofauti na fungu la kwanza, siye hasa Mungu bali viumbe kutoka anga za mbali, yaani Jamii ya Lyran Humanoids. Viumbe hawa wenye ujuzi mkubwa wa teknolojia mbali mbali ndio waliootesha uhai hapa duniani kutokea sayari yao. Kilichofanyika pale sio uumbaji hasa wa viumbe wasiowahi kuwepo bali ni uoteshaji wa viumbe waliopo katika sayari nyingine ya mbali. Michakato yote iliyofanyika pale ni jinsi ya kupangilia mambo katika mpango sawia unaowiana na sayari dunia. Majira na nyakati duniani , hali mbali mbali za hewa zingeweza kuwa ni tofauti kwa kiasi fulani na hivyo kuwa na athari kadhaa kwa viumbe hao endapo wangepandikizwa hapa duniani bila kupitia cloning biological engineering. Kwa hiyo cloning biological engineering ni teknolojia inayosaidia kiumbe hai kutoka sayari moja kufanya sayari rafiki kuwa sayari ya nyumbani. Tafsiri ya baadaye ya kitabu cha Mwanzo ndiyo iliyobadilisha uelewa huu wa michakato iliyoendelea katika sura hiyo. Kwa mfano neno "Bara" katika lugha ya kiebrania yaani "kuumba " lina maana ya kutokeza kitu kipya kisichowahi kuwepo kabisa. Lakini neno la kiebrania "Asah" yaani "kufanya" maana yake ni kupangilia kitu kilichopo ili kiwe katika muundo unaohitajika. Maneno ya kiebrania kama Elohimu jina lenye wingi wa neno El, kuonesha viumbe wahusika kwamba walikuwa wengi Maneno kama, tufanye mtu kwa sura na mfano wetu - Mwanzo 1:26,na maneno, Mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya-Mwanzo 3:22, kauli inayoonesha kwamba walikuwa wengi na wenye kuhesabika mmoja mmoja. Maana wakasema amekuwa kama mmoja wetu. Aidha binadamu akawa kama mmoja wao kwa kujua yaani ujuzi, kuonesha kwamba tofauti yao na binadamu ilikuwa katika ujuzi. Kwamba viumbe hawa walikuwa ni Wenye miili kama sisi kwa maana ile kauli iliyoahidi hukumu ya gharika kuu inasema, sitashindana na binadamu milele maana yeye naye ni nyama Mwanzo 6:33. Sasa angalia maneno , " Yeye naye ni nyama " kuonesha kwamba hata msemaji wa maneno hayo naye alikuwa ni nyama. Na kwa sababu ni nyama ndiyo maana viumbe hawa waliwahi kumtembelea Ibrahim akawachinjia wakala - Mwanzo 18:1-9. Tunaambiwa kwamba Yakobo alishindana na mmoja wa viumbe hawa mieleka na Yakobo ndiye aliyeshinda Mwanzo 32 :24 - 30. Viumbe hawa pia kama viumbe walikuwa na mipaka, kwa mfano Adamu alipojificha kiumbe aliyemtembelea hangeweza kumuona kwa hiyo aliuliza Adamu uko wapi? Mwanzo 3:8-11. Je unakumbuka wanadamu walipojenga mnara viumbe hawa walisema na tushuke tuwachafulie msemo wasielewane maana pengine jengo lao hilo refu lingeweza kusababisha madhara makubwa endapo lingeanguka kwa sababu ya kuwepo kwa mapungufu katika ubora. - Mwanzo 11:7 Jimena njoo huku na benie360
Hadi Nahisi Kichwa Kina Uma Najiulza Mambo Ambayo Majibu Yanakuwa Magumu,
Kitu Gan Kilifanya Binadamu Kumwabudu Mungu? Ama Kwanin Kizaz Kimoja Kiabudu Kingine,
Pia Kumbuka Jacob Hakushnda Alipigwa Paja Na Huyo Kiumbe ,na Je Hawa Viumbe Wana Kiongoz Wao Kama Yupo Ni Nan?
Nisaidie Haya Kwanza Alafu Uendlee