Jamii mbili za viumbe wenye akili ulimwenguni

Naomba unisaidie kuoanisha hiyo stori yako na "Human Races". Kwanini duniani kuna races nyingi za wanadamu...mfano, Blacks(Africans), Arabs, Whites, Indians, Asians(Eastern Asians), etc

Also, story yako inazungumzia wanadamu tu but ina-ignore viumbe wengine kama Tembo, Simba, Penguin, Ndege wa aina mbalimbali, samaki wa aina mbalimbali, etc.
 

Jazba za nini sasa?
 
du! kama naangalia sinema fulani za roboti kwenye ma galaxi, sijui nasoma jf au naangalia sinema au naota! ! ! !
 

Ni kama nyumbani kwenu utakuta kuna mtoto hana rangi ya baba wala ya mama. Na hiyo haimaanishi kwamba mtoto sio wao

Kuhusu Tembo, Simba, Penguin nk haihusiani na mada. Mada ni (jamii mbili za viumbe wenye akili ulimwenguni)
 

Elimu maridhawa hii nimechagua kuiamini.
Mkuu kama kunachakuongezea endelea kutupa darasa.
 
Muda wote nasubiri muendelezo wa hii mada sbb imenivutia sana. Mwaga fasta part III ili tuendelee na kujua tusiyoyajua. Ila nasubiri kujua kwa kuwa tulinyimwa uzima wa milele, je tunapokufa nini kinaendelea sbb nahisi hii mada inataka kuleta majibu fulani ivi ...!!!
Lete nondo mtoa mada
 
Mungu wangu. Akili ulizowapa wanadamu ndo wameamua kuzitumia hivi.....
 
Elimu maridhawa hii nimechagua kuiamini.
Mkuu kama kunachakuongezea endelea kutupa darasa.

Jamii binadamu nayo ipo njiani kuendeleza technology yake ili siku ikifika/ambayo ipo. Nasi pia tutaendelea na hii kazi ya kusambaza uhai ulimwenguni kama ilivyo kwa wazazi wetu.
Ikumbukwe kuwa kila tatizo lina jawabu lake ndani ya ulimwengu huu huu. Iwe kifo, ajali, nk... Yote hayo yana jawabu lake katika maarifa fulani.

Ngoja nimtage pia Apollo japo najua aweza kutofautiana na mimi kidogo. Wapo wengi ambao ningeweza kuwatage tatizo wao hawaamini kuwa mungu yupo
 
Last edited by a moderator:
Ok.
Tumalizie hiki kipande kidogo.... Cloning biological engineering ni teknolojia ya kurekebisha mifumo mbali mbali katika mwili wa kiumbe hai ili kiweze kuwiana na mazingira ya sayari husika. Hii ndiyo kazi tunayoiona katika masimulizi ya kitabu cha Mwanzo katika Biblia. Anayetajwa pale kuwa Mungu tofauti na fungu la kwanza, siye hasa Mungu bali viumbe kutoka anga za mbali, yaani Jamii ya Lyran Humanoids.

Viumbe hawa wenye ujuzi mkubwa wa teknolojia mbali mbali ndio waliootesha uhai hapa duniani kutokea sayari yao. Kilichofanyika pale sio uumbaji hasa wa viumbe wasiowahi kuwepo bali ni uoteshaji wa viumbe waliopo katika sayari nyingine ya mbali. Michakato yote iliyofanyika pale ni jinsi ya kupangilia mambo katika mpango sawia unaowiana na sayari dunia. Majira na nyakati duniani , hali mbali mbali za hewa zingeweza kuwa ni tofauti kwa kiasi fulani na hivyo kuwa na athari kadhaa kwa viumbe hao endapo wangepandikizwa hapa duniani bila kupitia cloning biological engineering.

Kwa hiyo cloning biological engineering ni teknolojia inayosaidia kiumbe hai kutoka sayari moja kufanya sayari rafiki kuwa sayari ya nyumbani. Tafsiri ya baadaye ya kitabu cha Mwanzo ndiyo iliyobadilisha uelewa huu wa michakato iliyoendelea katika sura hiyo. Kwa mfano neno "Bara" katika lugha ya kiebrania yaani "kuumba " lina maana ya kutokeza kitu kipya kisichowahi kuwepo kabisa. Lakini neno la kiebrania "Asah" yaani "kufanya" maana yake ni kupangilia kitu kilichopo ili kiwe katika muundo unaohitajika.

Maneno ya kiebrania kama Elohimu jina lenye wingi wa neno El, kuonesha viumbe wahusika kwamba walikuwa wengi Maneno kama, tufanye mtu kwa sura na mfano wetu - Mwanzo 1:26,na maneno, Mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya-Mwanzo 3:22, kauli inayoonesha kwamba walikuwa wengi na wenye kuhesabika mmoja mmoja. Maana wakasema amekuwa kama mmoja wetu.

Aidha binadamu akawa kama mmoja wao kwa kujua yaani ujuzi, kuonesha kwamba tofauti yao na binadamu ilikuwa katika ujuzi. Kwamba viumbe hawa walikuwa ni Wenye miili kama sisi kwa maana ile kauli iliyoahidi hukumu ya gharika kuu inasema, sitashindana na binadamu milele maana yeye naye ni nyama Mwanzo 6:33. Sasa angalia maneno , " Yeye naye ni nyama " kuonesha kwamba hata msemaji wa maneno hayo naye alikuwa ni nyama. Na kwa sababu ni nyama ndiyo maana viumbe hawa waliwahi kumtembelea Ibrahim akawachinjia wakala - Mwanzo 18:1-9. Tunaambiwa kwamba Yakobo alishindana na mmoja wa viumbe hawa mieleka na Yakobo ndiye aliyeshinda Mwanzo 32 :24 - 30.

Viumbe hawa pia kama viumbe walikuwa na mipaka, kwa mfano Adamu alipojificha kiumbe aliyemtembelea hangeweza kumuona kwa hiyo aliuliza Adamu uko wapi? Mwanzo 3:8-11. Je unakumbuka wanadamu walipojenga mnara viumbe hawa walisema na tushuke tuwachafulie msemo wasielewane maana pengine jengo lao hilo refu lingeweza kusababisha madhara makubwa endapo lingeanguka kwa sababu ya kuwepo kwa mapungufu katika ubora. - Mwanzo 11:7 Jimena njoo huku na benie360
 
Last edited by a moderator:
Hadi Nahisi Kichwa Kina Uma Najiulza Mambo Ambayo Majibu Yanakuwa Magumu,
Kitu Gan Kilifanya Binadamu Kumwabudu Mungu? Ama Kwanin Kizaz Kimoja Kiabudu Kingine,
Pia Kumbuka Jacob Hakushnda Alipigwa Paja Na Huyo Kiumbe ,na Je Hawa Viumbe Wana Kiongoz Wao Kama Yupo Ni Nan?

Nisaidie Haya Kwanza Alafu Uendlee
 

Uelewa wako naona ndo ulipoishia hapo


Hakuna mwenye shida yoyote na maswala ya jua kubadilika.

Na wala hii mada haina uhusiano na hayo uliyoandika hata kidogo.

Asante kwa mchango wako.
 
Hii yako ni new creation theory au na kama ni source ya watu wa kale aina mbili walipata wapi huo uwezo wa kujibadilisha wenyewe.
 

Haya mambo ni magumu aisee mleta mada naomba uweke source ya vitabu ulivotumia ili na Mimi nikisome nijue zaidi. Kwangu Mimi hii kitu ni new
 
Na miti nayo ilitokea wapi?

Mambo ya uumbaji hamna ayajuayo kwa sasa lbd mpaka miaka 2000 mingine ijayo ndio binaadam ataweza kutegua kitendawili hicho.
 

Hapa naomba nimtag tomjelly kama sikosei ni yeye alikuwa na andiko linalomtatiza kutoka biblia huwa ni viumbe gani waliokuwa wanaongelewa nadhani hapa atapata mwanga kiasi.

Asante sana kwa elimu mkuu
Cc Bennie 360
 
Last edited by a moderator:

Huku duniani ndio tu bado tunahangaika kusema mara mungu yuko hivi mara vile kwa sababu kuna maarifa ambayo bado hatujayajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…