Jamii ya Kimasai yaanzisha mfumo wa Uongozi wa Kimila wa Wanawake

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Jamii ya Kimasai ni Moja ya jamii ambayo hadi sasa inaishi kwa kufuata mila na tamaduni zake, tofauti na jamii nyingine ya kiafrika ambapo sasa hivi zinakwenda kusahau kabisa mila yake.

Katika jamii ya kimasai, kuna Viongozi wa kimila Wanaojulikana kama Leigwanan, hawa ni viongozi ambao wamekuwepo kwa miaka mingi waskishughulika na majukumu mbalimbali ya kijamii.

Kama ilivyo kwa jamii ya kimasai,Bado nafasi ya Mwanamke imekuwa ni ndogo sana katika uongozi na mara nyingi Mwanaume ndie amekuwa akionekana kushika nafasi ya uongozi.

Kwa mara ya kwanza katika jamii ya kimasai, pameonekana muhamko wa Wanajamii kutaka na Wanawake na wao waanze kushika nafasi za Uongozi wa Kimila.

Mnamo tareh 18 Juni 2024,historia imeandikwa katika jamii ya kimasai pale ambapo wanawake sita waliweza kutawazwa kwa mara ya kwanza kama viongozi wa Kwanza wa KImila ambao wanajulikana Engaigwanan.

Viongozi hawa watakuwa na majukumu ya kusimamia shughuli zote za kijamii na hasa katika kufanya utetezi wa haki za wanawake.

Tukio la kuapishwa kwa wanawake hawa lilifanyika katika Tarafa ya Loliondo,wilaya ya Ngorongoro na kuweza kuhudhuriwa na viongozi tofauti ikiwemo wa kisiasa pamoja na serikali.

Uhamasishaji wa kuanzishwa kwa Engaigwana ulianza kwa kufanziwa uchechemuzi na shirika la MImutie Women Organization lenye makao yake makuu katika eneo la Ngorongoro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…