Jamii ya wahadzabe ilindwe, baada ya miaka 8 hawatokuwepo tena

Jamii ya wahadzabe ilindwe, baada ya miaka 8 hawatokuwepo tena

Hizo ndo jamii bora na Asilia mkitaka kuwaletea usasa mtaharibu Sana.
Kuna mijitu ni mijuaji sana wao wanadhani ulimwengu unazunguka katika mawazo yao tu, kwamba kunywa mirinda, kutumia smartphone na kuitukana CCM hayo ndo maisha na wenyewe wanaita civilization
 
Wako so primitive sana! Sometimes kuwepo muingiliano na watu wengine ili kuwapa kujua kinachoendelea duniani.
Angalau wawe kama Wamasai hivi ambao pamoja na muingiliano na watu wengine lakini bado wamepreserve utamaduni wao.
Hiyo primitivism yao wewe inapunguza mshahara kiasi gani kwako
 
Hiyo primitivism yao wewe inapunguza mshahara kiasi gani kwako
Tuko kwenye modern world ambapo kwa utandawazi uliopo dunia ni kijiji wanatakiwa kuinteract na wengine bila kupoteza culture yao.
 
Huu uzi ni wa ajabu na watu waliocomment before this ni watu anbao sijui ni wa kundi gani

Sisi sote tulikuwa uncivilised sasa tuko civilized. Hakuna sifa kuwa au kuishi kama hazabe, watoto hawasomi na wala hawapati mahitaji muhimu za kibinadamu.

Hatuwezi kufagilia au kufurahia wahazabe waishi kama wanyama

Si kweli wana haki ya utandawazi, usasa. Ni haki yao

Dunia ni kijiji sasa, tunajenga madaraja kuunganisha watu, alafu kuna watu wanataka kujenga ukuta kufunga watu

Siafiki
Sisi tunabadirika...tunapiga pamba tunataka wao waendelee kuvaa ngozi!!
 
Tuko kwenye modern world ambapo kwa utandawazi uliopo dunia ni kijiji wanatakiwa kuinteract na wengine bila kupoteza culture yao.
Huo ulazima ni nani kauweka? Mabepali, kwanini ili kuneemesha matumbo yao

Tanzania matajiri ( on terms of dollars) chini ya 3000
Watu wa kipato cha kati hawazidi milioni 4 na wanaobakia wote ni masikini. Yaani asilimia 76 ya watanzania ni masikini na asilimia 43 ya watanzania wanaishi kwa chini ya dola moja, wapo below poverty line, na hao wote kwa kiwango kikubwa wanaishi kwenye hiyo modern civilization.

Kwahiyo lengo lenu muwaharibie wahadzabe mfumo wao wa maisha ili wawe manpower ya kuongeza utajiri kwa mabwenyebye, sijui unanielewa?.
Lengo la maisha ni kufurahia kile unachokipata, wao wako happy na maisha yao, hawana kansa, hawana hepatitis b virus, hawana HIV, hawana gonorrhea, hawakupata uviko, hawana shida ya chanjo, wanakula, wanalala, wanaoana, Wanafanya shereehe, wanaburudika enhee unataka wawe "civilized" ili!!? Halafu iweje yani?
 
Sisi tunabadirika...tunapiga pamba tunataka wao waendelee kuvaa ngozi!!
"Kupiga pamba" na "kubadilika" siyo kwa hiyari yako Babu yake Babu yako Babu yake alitukanwa na wafanyabiashara za utumwa, wakampeleka kwenye zoo za maonesho kama mfugo halafu hao watwana wakamwambia maisha aliyoishi siyo maisha ndiyo maana leo tuna civilization nyingi hadi za kubadili jinsia
 
Niliona wakihojiwa Clouds ile lifestyle yataka moyo sana ila kama umezoea ni maisha poa pesa inakuwa sio kipaumbele
 
"Kupiga pamba" na "kubadilika" siyo kwa hiyari yako Babu yake Babu yako Babu yake alitukanwa na wafanyabiashara za utumwa, wakampeleka kwenye zoo za maonesho kama mfugo halafu hao watwana wakamwambia maisha aliyoishi siyo maisha ndiyo maana leo tuna civilization nyingi hadi za kubadili jinsia
Acha kuishi kama nyani wewe dunia imebadilika unaweza kuona sifa kumbe watu wanakushangaa wanakuona hujakamilika kuwa binadamu miaka hii unavaa ngozi muda wote unanuka hii akili Gani yaani unaishi dunia ambayo unasubiri kifo ulikuja duniani kufanya nini sasa
 
Kama washaanza kuunga nyama na karoti/hoho/vitunguu na kuweka mafuta lazima wapotee.
 
Acha kuishi kama nyani wewe dunia imebadilika unaweza kuona sifa kumbe watu wanakushangaa wanakuona hujakamilika kuwa binadamu miak hii unavaa ngozi muda wote unanuka hii akili Gani yaani unaishi dunia ambayo unasubiri kifo ulikuja duniani kufanya nini sasa
Kipi kinachokufanyaa ujione wa pekee dhidi yao?
 
Back
Top Bottom