Jamii ya wahadzabe ilindwe, baada ya miaka 8 hawatokuwepo tena

Jamii ya wahadzabe ilindwe, baada ya miaka 8 hawatokuwepo tena

Dudukwe ndiyo nini?
Huyo ndo celebrity kwa wahdzabe ! Ndo ameonekana sana kwenye mitandao ya kijamii ! Yaan ukienda kuwatembelea wahadzabe usionane na Dudukwe huku uraiani tunaona kama umeigiza hukufika pori uliishia njiani ukaokoteza wahadzabe
 
Ndani ya hii miaka miwili Kuna muingiliano mkubwa sana wa jamii wa watu wa hadza na watu wa ulimwengu wa kwanza kitu ambacho binafsi naona kama kitachangia sana kuharibu mfumo wa mzuri wa kiasili waliouzoea kuishi na kuondoa kabisa ule utambulishi wao kama wahadzabe

Wageni wengi wanaokuja kuwaona na hata wenyeji wanaowaongoza hao wageni kutokea mijini hutambulisha vitu visivyo vya msingi kabisa kama vinywaji vya kusindika vyenye kemikali na mivyakula yenye sumu za viwandani kadhalika na mavazi ambayo hayana tija kwa jamii hiyo. Ninachoona si kwamba jamii hii haijui chochote kuhusu ulimwengu wa kisasa maana wao pia huku manyara huonekana kwenye minada mingi sana wakiuza zana za kuwindia na wao kupata bidhaa zingine, ila ninachoamini ni kuwa waliamua kwa dhati kujitenga na ulimwengu huu wa kisasa ili waishi kwa namna watakavyopendezwa wao

Muingiliano huu wa jamii ya hadza na watu kisasa unahatarisha hata kingamwili zao na harakati zao za kawaida kwa kuwa ni kama wanabugudhiwa na hawa watu wanaowatembelea na kuwapa vitu vigeni bila utaratibu maana hawa jamaa kwa kiasi kikubwa wako huru nje ya magonjwa tunayopambana nayo huku mjini kwa hiyo Wana kingamwili zao binafsi hivyo kuruhusu watu wawatembelee kiholela kunaweza kuhatarisha ustawi wai na mtindo mzima wa maisha yao

Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya maliasili na hata wizara ya mambo ya ndani ninaomba waweke marufuku au taratibu Kali au ikiwezekana kutoruhusu kabisa kuwasumbua wahadzabe kwa kuwa hawa jamaa ni moja ya jamii adhimu sana duniani ambazo zineamua kuishi utaratibu wao binafsi

Leo hii Afrika kusini amebakia mtu mmoja tu ambaye anatenda tamaduni za Khoisan naye ni mzee sana kwa kuwa jamii yao hao watu imeshamezwa na usasa. Hakuna faida yoyote wanayopata wahadzabe kwa kuingiliana na watu mjini au wa nje ya nchi zaidi ya hao watu kuwatumia kwa maudhui yao ya mtandaoni na kujitengenezea umaarufu na kipato huku wakiwaharibia mazingira na tamaduni zao

SERIKALI IWAPIGE MARUFUKU WATU WOTE WANAWAKARIBIA WAHADZABE
Hii jamii haitakiwi kulindwa kwani wenyewe hawataki kusaidiwa, wanataka waishi maisha wakifanana na wanyama na kutooga. Waachwe tu waangamie.
 
Hii jamii haitakiwi kulindwa kwani wenyewe hawataki kusaidiwa, wanataka waishi maisha wakifanana na wanyama na kutooga. Waachwe tu waangamie.
Eeh ndo muwaache kuwashobokea we wasipooga inapunguza chakula kiasi gani nyumbani kwako
 
Hizo ndo jamii bora na Asilia mkitaka kuwaletea usasa mtaharibu Sana.
 
Wako so primitive sana! Sometimes kuwepo muingiliano na watu wengine ili kuwapa kujua kinachoendelea duniani.
Angalau wawe kama Wamasai hivi ambao pamoja na muingiliano na watu wengine lakini bado wamepreserve utamaduni wao.
 
Back
Top Bottom