Unailindaje jamii na haya mapinduzi ya kijamii yanayoendelea, maeneo ya mapori yana rasimishwa, binadamu wanaondolewa na kubakiza wanyama kulinda ecologia ya wanyama pori na misitu, binadamu tumeonekana ni waharibifu wa misitu na,ecologia ya wanyama.Brasili na India Kuna jamii adhimu zinalindwa kwa nguvu zote
Hazabe wao wanahama hama kulingana na mahitaji na msimu, hawatulii, sio wafugaji siyo wakulima wanazagaa kutafuta wanyama kula, asali kula, matinda kula, hawaoteshi hawafugi, ni ngumu ila inawezekana kuwalinda, ila kwa sera za utalii kwa sasa watatoweka.
Serikali inawataka watulie iwajengee makazi, wao hawakatai chochote, ila kufanya hivyo ni kuwabadirisha kuwataka wawe tofauti na asili yao.