Jamii ya watu weusi inaangamia kwa kupenda miujiza, maajabu na mazingaombwe badala ya kupenda kuwajibika kwa juhudi na maarifa

Jamii ya watu weusi inaangamia kwa kupenda miujiza, maajabu na mazingaombwe badala ya kupenda kuwajibika kwa juhudi na maarifa

Wenzetu waishaachana na huu ujinga kitambo sana. Hawa manabii, mitume nk walikuwa ni watu wa kudhibitiwa, wanatumia ukosefu wa elimu na umasikini wa jamii yetu kuiangamiza kabisa.

Umewasahau imani za kishirikina, uchawi na waganga wa kienyeji wote hao ni kundi moja.
Umesema jambo la muhimu sana,uchawi na ushirikina nao ndio wale wale tu,

Cha ajabu eti yule anayeeneza propaganda za kichawi na kishirikina humu JF eti nae anayasema hayo makanisa!

😀😀😀😀
 
Hivi unafikiri wanaosema waafrika ni wajinga unadhani ni utani.Vichwa vyetu sio vizima kabisa.Ujinga tunaoufanya uku afrika ni mkubwa zaidi kuliko unaofanyika uko walikotuletea hizi dini.Kwa mfano angalia hili jambo la mapenzi ya jinsia moja,nakuhakikishia japokua kwasasa linaonekana ni jambo dogo na liko chini chini ila kwa vichwa vyetu baada ya miaka 10 litakua kubwa sana uku kwetu kuliko uko liliko toka.Dini zilianza hivi hivi polepole ila sasa hivi kuna wanaojifanya niwadogo zake na yesu kabisa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Nishakustukia... Wewe mfuasi.. maana nimetafakari huo ujumbe wako hata hauendani na mada
 
Upande wa pili kumejaa mbumbumbu
Screenshot_20230421-141547.jpg
 
Hebu imagine ndo anakanyaga gia, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], nacheka km mwehu hapa.
[emoji23][emoji23]alafu linafanya kama mdako vile huku wakisema I receive papa[emoji23][emoji23]
 
Longtime niliepelekagwa kwa mama rwakatare,kipengele hicho cha kutaka gari sasa ,mnakaa mkao wa kushika usukukani na kukanyaga break
Huku mnaombewa [emoji1]

Ova
Alikupeleka Mama? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ilikuwaje ukatoka katoliki?
Sijawahi kuwa Mkatoliki.

Hizo habari ni za wazushi tu wanaoona fahari kujifanya wananijua kuliko ninavyojijua mimi mwenyewe.

Kuhusu Ukristo, polepole niliona tu kwamba, kimantiki, habari za uwepo wa Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote zinapingana na uhalisia.

Baadaye, nikawa nasoma sana dini tofauti na falsafa, nikakutana na kitu kinaitwa "the problem of evil" hususan version ya "Epicurean Paradox", nikaona kumbe kile nilichokuwa nakifikiri wanafalsafa walishakiona na kukiandika vizuri miaka mingi sana.

Ukiangalia "the problem of evil" na "The Epicurean Paradox" kimantiki, utaona huyu Mungu hayupo, ni hadithi ya kutungwa na watu tu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Dah [emoji23][emoji23]yaani nimewavutia picha nikajikuta nacheka mbaya kabisa. Mara mmama na mimba yake, mbaba na likitambi wanapichana kama robot.

Hawa wahubiri Mungu anawaona[emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna waumini watakufa miguu inachucha maji wallah, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Enyi wagalatia mliokoswa Akili ni Nani aliyewaroga?
Ewe unayejitoa ufahamu kwa kuhisi wagalatia wamerogwa jiulize kwanza wanaojitoa mhanga wamelogwa na nani?Usichukulie kwa ujumla ujinga wa watu wachache ukafanya kundi lote wajinga
 
Duh: kuna hawa wanaojiita wakarisimatic ndani ya kanisa letu Katoliki.kuna siku nimeenda parokiani kuonana na paroko.Baba paroko akanitonya nimsubirie kidogo kama nusu saa hivi maana alikua na issue anamalizia.

Basi nikao kwa muda ule niingie kanisani maana kulikua kumechangamka kwa kelele za hapa na pale.kuingia ndani nikakuta hao wakarisimatic wanafanya yao.nikaketi benchi la nyuma kabisa kuona kinachofanyika.ghafla akaja mmoja wao na kunihoji kwa nini nimekaa ili hali wao wanapepetana na shetani na pia nitoke pale niende mbele.nikamwambia aisee hebu niache ww kaendelee na mambo yenu.kilichofuatia alienda kuita mwenzake ambapo waliniambia nitoke nje haraka..hapo ikawa ndio mbwai sasa maana nilichowajibu ni kwamba hili kanisa amejenga nani mpaka mniambie nitoke nje?

Wakasisitiza nitoke hapo ndio ikawa tafrani mpaka baba paroko akaenda kuitwa kuamulia kimuhemuhe kile.alipokuja nilimuuliza swali lile lile ya kwamba ni nani amejenga hili kanisa.Paroko kwa ueledi wake akajibu kanisa hili limejengwa na waumini na sio mali ya mtu binafsi.Hapo wale wakulungwa wakaishiwa pozi wakaamriwa watoke nje kwa maana wanaleta fujo...Binafsi hawa watu wenye vinasaba vya miujiza nawachukkulia kama wagonjwa wa akili.
Ukiwa Roma ishi kama Waroma.Kama hukuwa na sababu ya kuwasikiliza wewe kwa nn ubishane nao si ungeondoka?
 
Back
Top Bottom