SoC02 Jamii yenye huzuni iliyojaa picha za furaha na ufahari katika mitandao ya kijamii

Stories of Change - 2022 Competition

Leonard24

New Member
Joined
Aug 23, 2022
Posts
1
Reaction score
3
Utambulisho
Habari Wana jamii Forum,kwa majina naitwa Lenny Godfrey mkazi wa wilaya ya kinondoni jijini Dar-Es-Salaam.Na pia Mimi ni mwanachuo wa chuo kikuu Cha Sayansi na Teknologia Cha mtakatifu Joseph Mbezi jijini Dar-Es-Salaam katika ngazi ya Uhandisi.

Kutokana na ukuaji wa Sayansi na Teknolojia kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya mitandao ya kijamii na hii inaotokana na ongezeko la utumiaji wa vifaa vya kisasa vya mawasiliano kama simujanja na komputa mpakato,vishikwambi n.k hii imepelekea kuwa na mabadiliko makubwaa ya maisha ya vijana katika jamii ya Leo .

IMG_20220823_224737.jpg

Athari za mitandao ya kijamii kwa vijana wa Leo.
Hapa tagusia zaidi vijana walio katika ngazi ya elimu ya juu nikimaanisha vijana wengi walio machuoni.Tofauti na maisha ya zamani vijana wengi wa Leo wameathiriwa na mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter, Snapchat n.k katika mitandao hiyo vijana wengi wamekuwa wakijionyesha wenye furaha,maisha ya kifahari na yenye kupendeza lakini nyuma ya pazia ni tofauti na kile kinachoonekana katika mitandao.Jamii imekuwa na watu wenye picha za furaha lakini nyuma ya kioo wamejaa maisha ya kusikitisha na msongo mkubwaa wa mawazo.

Hii imepelekea vijana wengi kujihusisha na shughuli haramu Ili wapate ela waweze kuonekana wenye mafanikio katika mitandao hiyo.mfano mkubwa ni dada zetu ambao asilimia kubwa wamejihusisha kwenye vitendo vya ngono na watu wengi wenye uwezo wa kifedha Ili waweze Kupata ela na kupelekwa sehemu nzurii kwa ajili ya kupiga picha waonekane kwenye mtandao ni wenye maisha mazuri.

Uvutaji wa shisha kwa vijana wengi huku wakijichukua video yameongezeka kwa asilimia kubwa Hadi kupelekea waziri wa Afya muheshimiwa Ummy Mwalimu ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Tanga kuanza kulifanyia uchunguzi jambo hili Ili kuona kama Lina uhalali wowote.Pia kuishi tamaduni za watu wa ughaibuni na kuacha tamaduni zetu za asili ni matokeo hasi ya mitandao ya kijami kuanzia kwenye uvaaji wa mavazi yanayoacha sehemu kubwa za miili yetu wazi hasa kwa dada zetu na pia nguo za kuangaza miili yetu.

IMG_20220823_233551.jpg

Mitandao ya kijami pia imechangia kwa asilimia kubwa kupunguza mda wa vijana kufanya kazi za kujenga jamii na kutumia mda mwingi katika kupeluzi mndaoni.takwimu nyingi zinaonesha vijana wengi wa sasa wanatumia masaa mengi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kufanya kazi za njee na hii imepelekea kupungua kwa ubunifu na uzalishaji Mali katika Nchi yetu.Pia mda wa kusoma kwa vijana haupo tena kwa kuwa vijana hawataki kufikiria na kutegemea mitandao katika kila kitu.
IMG_20220823_234017.jpg

Ongezeko kubwa la wizi wa mitandao ni Moja ya matokeo ya matumizi makubwaa ya mitandao ya kijamii.watu wengi wanatumia jukwaa la mitandao kufanya matukio ya wizi wa fedha kwa vijana.hii inaotokana na vijana wengi kuweka taarifa za Siri katika mitandao bila kujua madhara au athari zinazoweza kujitokeza mbeleni kama kuibiwa ela zao.

Je ni nini kifanyike Ili kupunguza athari za mitandao ya kijamii kwa vijana?
Kutokana na haya yote jamii inabidi iwe na mtazamo chanya kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii . Vijana wanatakiwa kuishi katika uhalisia wao na katika hali zao halisi za kiuchumi Ili waweze kujikwamua na Kutafuta njia za kujinua kimaisha kuliko kuonyesha wenye maisha Bora yasiyokuwa na ukweli ndani yake.Pia mitandao ya kijamii itumike kama jukwaa la elimu kwa vijana kuhusu masomo ya biashara na njia za kujikimu kimaisha na siyo jukwaa la kuoneshana uwezo wa kimaisha.

Wazazi, serikali na jamii nzima kwa ujumla ni jukumu letu kuwapa elimu watoto wa kike juu ya umuhimu wa kujilinda katika maisha Yao na kutoruhusu maisha ya wengine yakawafanya wapoteze heshima na utu wao.vijana wanatakiwa wapewe elimu juu ya umuhimu wa kuishi katika uhalisia na siyo maisha ya kuigiza .Maisha ya kuigiza katika mitandao kunafanya vijana kupoteza mda mwingi na kutumia nguvu kubwa kushawishi jamii kitu ambacho hakina msaada katika maisha Yao ya mbeleni.

Viongozi wa dini wanaweza toa mchango mkubwa katika kuikomboa jamii ya vijana wa Leo kwa kuwapa vijana elimu ya kidini inayowafundisha kuishi katika maisha Bora na kutofwata mienendo mibaya na isiyo na tija katika maisha yao.Vijana wengi wameacha kwenda katika nyumba za dini na kwa kulijua hili viongozi wa dini wanatakiwa kutumia fursa hii ya mitandao kuwapa vijana elimu ya kidini kupitia mitandao.Hii itapunguza kwa namna Moja ama nyingine vitendo vya ajabu vinavyofanywa na vijana wengi katika mitandao.

Ukosefu wa ajira na kazi kwa vijana pia kunapelekea matumizi makubwaa ya vijana katika mitandao ya kijamii . Serikali inatakiwa itoe ajira za kutosha kwa vijana Ili wawe na shughuli za kujikwamua na kupunguza mawazo na huzuni zinazotokana na kuona vijana wengi wakishi maisha mazurii yasiyo na uhalisia ndani yake.

Asanteni.

Marejeo.
PICHA KWA MSAADA WA GOOGLE.
 
Upvote 4
Utambulisho
Habari Wana jamii Forum,kwa majina naitwa Lenny Godfrey mkazi wa wilaya ya kinondoni jijini Dar-Es-Salaam.Na pia Mimi ni mwanachuo wa chuo kikuu Cha Sayansi na Teknologia Cha mtakatifu Joseph Mbezi jijini Dar-Es-Salaam katika ngazi ya Uhandisi.

Kutokana na ukuaji wa Sayansi na Teknolojia kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya mitandao ya kijamii na hii inaotokana na ongezeko la utumiaji wa vifaa vya kisasa vya mawasiliano kama simujanja na komputa mpakato,vishikwambi n.k hii imepelekea kuwa na mabadiliko makubwaa ya maisha ya vijana katika jamii ya Leo .

View attachment 2333025

Athari za mitandao ya kijamii kwa vijana wa Leo.
Hapa tagusia zaidi vijana walio katika ngazi ya elimu ya juu nikimaanisha vijana wengi walio machuoni.Tofauti na maisha ya zamani vijana wengi wa Leo wameathiriwa na mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter, Snapchat n.k katika mitandao hiyo vijana wengi wamekuwa wakijionyesha wenye furaha,maisha ya kifahari na yenye kupendeza lakini nyuma ya pazia ni tofauti na kile kinachoonekana katika mitandao.Jamii imekuwa na watu wenye picha za furaha lakini nyuma ya kioo wamejaa maisha ya kusikitisha na msongo mkubwaa wa mawazo.

Hii imepelekea vijana wengi kujihusisha na shughuli haramu Ili wapate ela waweze kuonekana wenye mafanikio katika mitandao hiyo.mfano mkubwa ni dada zetu ambao asilimia kubwa wamejihusisha kwenye vitendo vya ngono na watu wengi wenye uwezo wa kifedha Ili waweze Kupata ela na kupelekwa sehemu nzurii kwa ajili ya kupiga picha waonekane kwenye mtandao ni wenye maisha mazuri.

Uvutaji wa shisha kwa vijana wengi huku wakijichukua video yameongezeka kwa asilimia kubwa Hadi kupelekea waziri wa Afya muheshimiwa Ummy Mwalimu ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Tanga kuanza kulifanyia uchunguzi jambo hili Ili kuona kama Lina uhalali wowote.Pia kuishi tamaduni za watu wa ughaibuni na kuacha tamaduni zetu za asili ni matokeo hasi ya mitandao ya kijami kuanzia kwenye uvaaji wa mavazi yanayoacha sehemu kubwa za miili yetu wazi hasa kwa dada zetu na pia nguo za kuangaza miili yetu.

View attachment 2333027
Mitandao ya kijami pia imechangia kwa asilimia kubwa kupunguza mda wa vijana kufanya kazi za kujenga jamii na kutumia mda mwingi katika kupeluzi mndaoni.takwimu nyingi zinaonesha vijana wengi wa sasa wanatumia masaa mengi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kufanya kazi za njee na hii imepelekea kupungua kwa ubunifu na uzalishaji Mali katika Nchi yetu.Pia mda wa kusoma kwa vijana haupo tena kwa kuwa vijana hawataki kufikiria na kutegemea mitandao katika kila kitu.
View attachment 2333028
Ongezeko kubwa la wizi wa mitandao ni Moja ya matokeo ya matumizi makubwaa ya mitandao ya kijamii.watu wengi wanatumia jukwaa la mitandao kufanya matukio ya wizi wa fedha kwa vijana.hii inaotokana na vijana wengi kuweka taarifa za Siri katika mitandao bila kujua madhara au athari zinazoweza kujitokeza mbeleni kama kuibiwa ela zao.

Je ni nini kifanyike Ili kupunguza athari za mitandao ya kijamii kwa vijana?
Kutokana na haya yote jamii inabidi iwe na mtazamo chanya kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii . Vijana wanatakiwa kuishi katika uhalisia wao na katika hali zao halisi za kiuchumi Ili waweze kujikwamua na Kutafuta njia za kujinua kimaisha kuliko kuonyesha wenye maisha Bora yasiyokuwa na ukweli ndani yake.Pia mitandao ya kijamii itumike kama jukwaa la elimu kwa vijana kuhusu masomo ya biashara na njia za kujikimu kimaisha na siyo jukwaa la kuoneshana uwezo wa kimaisha.

Wazazi, serikali na jamii nzima kwa ujumla ni jukumu letu kuwapa elimu watoto wa kike juu ya umuhimu wa kujilinda katika maisha Yao na kutoruhusu maisha ya wengine yakawafanya wapoteze heshima na utu wao.vijana wanatakiwa wapewe elimu juu ya umuhimu wa kuishi katika uhalisia na siyo maisha ya kuigiza .Maisha ya kuigiza katika mitandao kunafanya vijana kupoteza mda mwingi na kutumia nguvu kubwa kushawishi jamii kitu ambacho hakina msaada katika maisha Yao ya mbeleni.

Viongozi wa dini wanaweza toa mchango mkubwa katika kuikomboa jamii ya vijana wa Leo kwa kuwapa vijana elimu ya kidini inayowafundisha kuishi katika maisha Bora na kutofwata mienendo mibaya na isiyo na tija katika maisha yao.Vijana wengi wameacha kwenda katika nyumba za dini na kwa kulijua hili viongozi wa dini wanatakiwa kutumia fursa hii ya mitandao kuwapa vijana elimu ya kidini kupitia mitandao.Hii itapunguza kwa namna Moja ama nyingine vitendo vya ajabu vinavyofanywa na vijana wengi katika mitandao.

Ukosefu wa ajira na kazi kwa vijana pia kunapelekea matumizi makubwaa ya vijana katika mitandao ya kijamii . Serikali inatakiwa itoe ajira za kutosha kwa vijana Ili wawe na shughuli za kujikwamua na kupunguza mawazo na huzuni zinazotokana na kuona vijana wengi wakishi maisha mazurii yasiyo na uhalisia ndani yake.

Asanteni.

Marejeo.
PICHA KWA MSAADA WA GOOGLE.
Andiko zur sana 😍
 
Back
Top Bottom