Jamiiforums GYM (mazoezi ) thread

Unajipa sifa na kujichosha maujinga ninyi mkifika JKT SIKU MBILI HAMTOBOI UPUZI TUPU kama una manyama uzembe nenda kambi ya JKT jirani omba ujumuike mazoezini watakusaidia siku tatu tu fresh UNAUJUA USINGIZI WW... HIZO SODA NIKIWA JKT NILIKUWA NAKUNYWA KAMA TATU NAMANA SUKARI NA MAJI NILIKUWA NA HISI VINAPUNGUA MWILINI
 
Zoezi langu kuogelea na kuendesha baiskeli. Kwa mazingira ya Dar kuendesha Baiskeli changamoto sana, madereva wa pikipiki,bajaj na magari unakuwa mnyonge wao safety ipo chini sana
 
Mkumbushe pia mazoezi lazima yaendane na nidhamu ya ulaji sio anachoma carolies jioni anaenda kufakamia viepe pale uhasibu karibu na liquid
Ukichoma sana carolies unatakiwa ule sana chakula gani?
 
Uzi mzuri sana... wakuu shusheni madini sasa
 
mazoez huimarisha kinga ya mwili
Kweli mkuu,
Daa mkuu wengine tukipiga kumi mara nne ile round ya tano hunyanyuki,wewe 50!!!kweli kila kitu ni mazoea na daily practice.
 
Lengo ni kuwa smart na kuwa fit tu (body ya kawaida)
Ila ukielezea kwa namna zote itakuwa bora
Anhaa kabla sijaongelea chakula baada ya mazoezi umechoma calories nyingi ni vizuri ukapata muda wa kutosha kupumzika ili mwili ufanye recovery.

Upande wa ulaji sasa soma ukiwa umetulia misosi ya kuzingatia ni

PROTINI
Hii ndio inaenda kuripea na kuboresha tuseme ukuaji wa misuli yako so ukipata nafasi ya kupiga kuku,samaki,mayai,maziwa iwe mtindi au fresh usiichezee ndo maprotini yenyewe hayo.(Japo pia ipo PROTINI yenyewe kama yenyewe ya unga hii unachanganyia kinywaji unapiga wanatumia sana mabaunsa na wasanii kukuza misuli ipo ujazo tofauti kuanzia nusu kilo na kuendelea)

WANGA
Hii ndio chanzo cha energy yenyewe lakini Usitumie wanga wa vyakula vilivyokobolewa epuka sembe maandazi,chapati hizo sio nzuri sana we piga Ile mikate Ina rangi kama kahawia Ile si iringa tunaita mikate ya kikinga,piga ndizi za kuiva sana hizi hadi mia unapata sokoni ilala noma ukinunua za buku unapewa na nyongeza,piga viazi vitamu vile we mwenyewe utaona mabadiliko

Epuka vyakula vya mafuta kula maparachichi yana mafuta mengi tu yasiyo na madhara

Kunywa maji mengi maana ukichoma carolies sio mchezo lazima jasho likutoke so unafidia maji uliyopoteza kupitia jasho enhee halafu nimekumbuka Yale maji ya madafu ndo noma yaani ukiwa unakunywa madafu ukipiga zoezi unachelewa kuchoka na unakuwa na vibe sana maana maji ya dafu/maji ya nazi yana electrolytes

MUDA WA KULA
Ukipiga tizi kama kuanzia dakika 30 mpaka lisaa ndo ule hapo mwili unakuwa na hamu sana ya kuabsorb nutrient zile so inafyonza chap kula Bangladesh wazungu waliotufundisha huo muda wanaita "anabolic window"

Kwahiyo ndo hivyo mwanangu
Kama unataka body flani misulimisuli,chest six pack piga sana hayo mamisosi nlivyokwambia kama unataka mwili Fulani mdogomdogo mwepesi basi ulaji wako we punguza ila hivyo vyakula kula kwa kiasi usiache kabisa usije ukakauka kabisa wakajua umeukwaa ila ukizingatia hivyo mwili utakuwa unafanya recovery vizuri matokeo unayapata na huumizi mwili wako
 
mazoez mhim sana, nliingia gym kipindi niko secondary🤣, ila sasa sitak ule mwili aisee, mwendo wangu umeharibika natembea kifua mbele, naichukia hii hali.
 
Asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…