Jamiiforums GYM (mazoezi ) thread

Jamiiforums GYM (mazoezi ) thread

Wakuu mambo vipi....Binafsi sio mkufunzi(gym trainer) ila napenda sana mazoezi na ninayajua mazoezi kuliko hata hawa wanaojiita ma-trainer,nimeanza kupenda mzoezi ya gym nikiwa form 3 (2013) so unaweza kuona nina experience ya miaka 11.

Mazoezi pia yanaambatana na aina ya vyakula tunavyokula ukiwa mwanamazoezi automatically kuna vyakula utaanza kuviepuka kama soda na vyakula vya mafuta.Binafsi nina mwaka wa 7 sijui soda na mwaka 4 sijui chips zikoje.Mimi nafanya mazoezi sili chipsi(mafuta food) wewe je nyama uzembe.Week inasiku 7 unahitaji siku tatu mfululizo za mazoezi na siku 4 unapumzika .anza leo after 6 monthes utaona matokeo.

Nitakuwepo hapa kuwapa-assistance kwa bigginer wote.hapa ni uwanja wa mazoezi ya aina zote both weight lift and cardio(mazoezi ya kukimbia na kucheza mziki,kupunguza mafuta na kutafuta pumzi)

Uzi huu ukawe wa kuhamasishana mazoezi na kupeana tips mbali mbali najua humu kuna wataalamu zaidi na wajuzi wa lishe wa kutosha.

Zifuatazo ni Faida za Mazoezi mwilini

1. Kuboresha Afya ya Moyo.
Mazoezi ya mara kwa mara husaidia kuimarisha moyo na kuboresha mzunguko wa damu, kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.

2.Kuongeza Nguvu na Uimara.
Mazoezi ya nguvu huongeza misuli na kuimarisha mifupa, huku mazoezi ya uvumilivu yakisaidia kuboresha uwezo wa mwili kustahimili uchovu.

3. Kupunguza Uzito.
Mazoezi husaidia kuchoma kalori na kupunguza mafuta mwilini, hivyo kusaidia katika kupunguza uzito.

4.Kuboresha Mvuto wa Mwili
Mazoezi ya mara kwa mara husaidia kuimarisha misuli na kufanya mwili kuwa na muonekano mzuri na wenye nguvu.

5.Kupunguza Stress na Kuboresha Hisia.
Mazoezi yanaweza kusaidia katika kupunguza viwango vya stress na kuboresha hisia kwa kuongeza uzalishaji wa endorphins, kemikali zinazofanya mtu ajihisi vizuri.

6.Kuboresha Usingizi.
Mazoezi yanaweza kusaidia kuboresha ubora wa usingizi, hivyo kukufanya uamke ukiwa na nguvu na mchangamfu.

Jinsi ya Kuanza Mazoezi
Najua wabongo wengi hatupendi mazoezi kutoka na mfumo wetu na ukuaji wetu wa maisha maana mazoezi ni sehemu ya maisha ni hii husaidia sana watu kuiishi umri ya miaka 70 mpaka 90.

1. Anza Kidogo Kidogo.
Usijaribu kufanya mazoezi mengi mara moja. Anza na mazoezi madogo na polepole ongeza muda na kiwango cha mazoezi.

2. Chagua Mazoezi Unayoyafurahia.
Tafuta aina ya mazoezi unayopenda, iwe ni kutembea, kukimbia, kuogelea, kucheza dansi, au hata mazoezi ya nyumbani. Kama unajifurahisha, utapata rahisi kuendelea.

3.Panga Ratiba.
Weka ratiba ya mazoezi na ujitahidi kuifuata. Hakikisha una muda maalum wa kufanya mazoezi kila siku au kila wiki.

4.Tumia Rafiki.
Kufanya mazoezi na rafiki kunaweza kufanya mazoezi yawe na furaha zaidi na kukuongezea motisha.

5.Lenga Malengo Madogo na Yanayowezekana.
Weka malengo madogo na yanayoweza kufikiwa. Kwa mfano, lengo la kutembea kwa dakika 20 kila siku kwa wiki moja.

6. Sikiliza Mwili Wako
Usijilazimishe kufanya mazoezi zaidi ya uwezo wako. Sikiliza mwili wako na pumzika unapohisi uchovu.
Unajipa sifa na kujichosha maujinga ninyi mkifika JKT SIKU MBILI HAMTOBOI UPUZI TUPU kama una manyama uzembe nenda kambi ya JKT jirani omba ujumuike mazoezini watakusaidia siku tatu tu fresh UNAUJUA USINGIZI WW... HIZO SODA NIKIWA JKT NILIKUWA NAKUNYWA KAMA TATU NAMANA SUKARI NA MAJI NILIKUWA NA HISI VINAPUNGUA MWILINI
 
Zoezi langu kuogelea na kuendesha baiskeli. Kwa mazingira ya Dar kuendesha Baiskeli changamoto sana, madereva wa pikipiki,bajaj na magari unakuwa mnyonge wao safety ipo chini sana
 
Mkumbushe pia mazoezi lazima yaendane na nidhamu ya ulaji sio anachoma carolies jioni anaenda kufakamia viepe pale uhasibu karibu na liquid
Ukichoma sana carolies unatakiwa ule sana chakula gani?
 
mazoez huimarisha kinga ya mwili
Kweli mkuu,
Kama una anza kabla ujaanza bench press kwa ajili ya kupata kifua push up ni muhimu sana kwani itakupa power ya kuinua weight na pia inajenga body structure

Anza push up kila siku jioni au asuhubi ukiamka uzuri wa push up kadri unazid kupiga ndio kiwango chako kinaongezeka unaweza ukafika hadi push up 100 kwa mara moja.

Kiwango changu ni push up 50 kwa round 10...jumla zinakuwa 500.sio powa.
Daa mkuu wengine tukipiga kumi mara nne ile round ya tano hunyanyuki,wewe 50!!!kweli kila kitu ni mazoea na daily practice.
 
Lengo ni kuwa smart na kuwa fit tu (body ya kawaida)
Ila ukielezea kwa namna zote itakuwa bora
Anhaa kabla sijaongelea chakula baada ya mazoezi umechoma calories nyingi ni vizuri ukapata muda wa kutosha kupumzika ili mwili ufanye recovery.

Upande wa ulaji sasa soma ukiwa umetulia misosi ya kuzingatia ni

PROTINI
Hii ndio inaenda kuripea na kuboresha tuseme ukuaji wa misuli yako so ukipata nafasi ya kupiga kuku,samaki,mayai,maziwa iwe mtindi au fresh usiichezee ndo maprotini yenyewe hayo.(Japo pia ipo PROTINI yenyewe kama yenyewe ya unga hii unachanganyia kinywaji unapiga wanatumia sana mabaunsa na wasanii kukuza misuli ipo ujazo tofauti kuanzia nusu kilo na kuendelea)

WANGA
Hii ndio chanzo cha energy yenyewe lakini Usitumie wanga wa vyakula vilivyokobolewa epuka sembe maandazi,chapati hizo sio nzuri sana we piga Ile mikate Ina rangi kama kahawia Ile si iringa tunaita mikate ya kikinga,piga ndizi za kuiva sana hizi hadi mia unapata sokoni ilala noma ukinunua za buku unapewa na nyongeza,piga viazi vitamu vile we mwenyewe utaona mabadiliko

Epuka vyakula vya mafuta kula maparachichi yana mafuta mengi tu yasiyo na madhara

Kunywa maji mengi maana ukichoma carolies sio mchezo lazima jasho likutoke so unafidia maji uliyopoteza kupitia jasho enhee halafu nimekumbuka Yale maji ya madafu ndo noma yaani ukiwa unakunywa madafu ukipiga zoezi unachelewa kuchoka na unakuwa na vibe sana maana maji ya dafu/maji ya nazi yana electrolytes

MUDA WA KULA
Ukipiga tizi kama kuanzia dakika 30 mpaka lisaa ndo ule hapo mwili unakuwa na hamu sana ya kuabsorb nutrient zile so inafyonza chap kula Bangladesh wazungu waliotufundisha huo muda wanaita "anabolic window"

Kwahiyo ndo hivyo mwanangu
Kama unataka body flani misulimisuli,chest six pack piga sana hayo mamisosi nlivyokwambia kama unataka mwili Fulani mdogomdogo mwepesi basi ulaji wako we punguza ila hivyo vyakula kula kwa kiasi usiache kabisa usije ukakauka kabisa wakajua umeukwaa ila ukizingatia hivyo mwili utakuwa unafanya recovery vizuri matokeo unayapata na huumizi mwili wako
 
mazoez mhim sana, nliingia gym kipindi niko secondary🤣, ila sasa sitak ule mwili aisee, mwendo wangu umeharibika natembea kifua mbele, naichukia hii hali.
 
Asante sana
 
Back
Top Bottom