Tulipo ishia, nimemaliza form 4 rasmi naanza maisha ya mtaani
Nilikuwa mtafutaji wazee kwanza niliingia mtaani kusaka kazi, nilibahatika kupata kazi ya kumfundisha mtoto wa jamaa mmoja kompyuta,nakumbuka nilikaa pale kwa muda wa miezi kama 4 make alikuwa na duka la nguo na vifaa vya umeme na simu baada ya kijana wake kuelewa mafundisho ilibidi mkataba wangu uishie pale huyu baba pia ni mtoto wa yule mzee aliyenisomesha imagine familia hii ilivyonitendea natamani na mimi siku moja niwalipe wema walio nitendea hata kama ni kwa vitukuu vyao naamini mungu ni mwema ipo siku.
Baada ya mkataba kuisha ikabidi nirudi home nikaanza kumshinikiza baba mkubwa anioneshe au kuniambia mama yangu mzazi alipo na anipe kisa cha mama yangu kunitelekeza mzee alikataa kata kuniambia kisa na alisema anayejua mama yangu alipo ni mwanaye mkubwa ndo aliwahi kuishi naye kwa baba yangu mzazi. Huyo dada kipindi hicho alikuwa mwanza kwenye utafutaji nikasema siku akija nitamuomba anipe stori kuhusu mama yangu
Kama nilivyosema awali mungu sio Yuda dada alikuja pale nyumbani kusalimia ilikuwa ni kipindi cha sikukukuu kijana nikajitahidi kumfurahisha dada yangu ili anipeleke anapohisi mama atakuwepo nakumbuka kipindi hicho tayari nishapata compyuter naingiza muvi na muziki na hii ilikuwa ya jamaa yangu ( hii biashara ilikuja kuharibika baadae baada ya compyuter kuungua tukakosa vifaa make ilibidi vifatwe mjini )
Basi baada ya dada kumaliza siku zake pale akaaga nakuondoka ila tukaondoka wote kwenda kumtafuta mama bhana, sister angu huyu ni genius kwenye kumbukumbu aisee alikumbuka maeneo tukayapitia yote huku tunauliza jina kizuri mama hakubadili jina wazee hapo nina hamu sana ya kumuona mama yangu yaani upendo kama wote ila kichwani pia nina hamu ya kumuuliza maswali yangu hasa kwanini aliamua kunitelekeza kwa miaka zaidi ya 20 na alipo kuwa sio mbali kwamba utavuka mikoa 5 bado hata kama ingekuwa 5 alishindwa nini kufatilia kama nipo au nilikufa.
Basi bhana baadae tukafanikiwa kuelekezwa nyumba alimo kuwa anaishi ile tumeenda sista akamuona na kweli wakajuana ni nimefanana na maza kinoma hawezi nikataa basi bhana wakuu ule upendo niliokuwa nao sijui ulienda wapi nilijjkuta nakasirika mpaka wote wakaniuliza kulikoni nikavunga, nilisalimiana na mama kikawaida yaani utafikiri ni mtu nimetoka kuonana naye jana au juzi tu, baadae sista aliaga na kuondoka mi nikabaki pale nikatengewa maji ya kuoga nikaoga chakula ya mchna ilikuwa tayari baada ya hapo tukaufinya msosi, nikasema leo ngoja nivunge ila kesho nitauliza maswali yangu.
Kesho yake nilipata wasaaa wakuongea na mama swali langu la kwanza nilimuuliza kwanini hakuwahi kunitafuta wakuu huwezi amini mama aliniambia kuwa sababu ni baba yangu nikamuuliza mbona mpaka baba yangu anakufa hakuwahi kuniambia kitu chochote kuhusu wewe hata familia nilikokulia hawajawahi kuniambia chochote kuhusu ww walikuwa wanasema utaniambia ww na ww unasema sababu ni baba yangu.
Wakuu nilijikuta naanza kumchukia maza pole pole baada ya kumbana sana akanipa stori kamili ni hivi baba alipooana na mama kwao na mama hawakupenda hili maana mama yangu ni muislamu baba yangu ni mkristo so wakasema mtoto wao hawezi olewa na kafiri kama wasemavyo wao nikaichanganua hiyo hoja nikaona ni sawa ( hii nilikuja kulipiza baadae tutaona mbele ) nikamuuliza je walimkataza hadi kuja kuniona au kunitembelea au kunijulia hali hapa ndo ikawa kimbembe alikaa kimya akaanza kufoka foka nikasena barida isiwe tabu mimi nilichotaka ni kukujua kama upo hai mengine wacha yapite, nilikaa pale kwa maza kama miezi 2 hivi, nikarudi home ikabidi nijiingize kwenye masuala haya ya usajili wa line ikumbukwe upendo wangu kwa mama haukuwa mwingi kivile yaani hapa niwe mkweli hadi leo mama yangu amekuwa ni kama mtu baki sijui nielezeeje yaani upendo mwingi upo kwa upande wa baba yangu huko ujombani kuna watu wengine nahisi hawanijui afu ni watu wa kujitenga tenga yaani kujiona sana mimi sifagilii hizo mambo
Basi bhana nimenza kusajili line, nikapata mtaji pale nyumbani ikabidi nifungue kibanda kama kiduka flani hivi baba mkubwa hakuwahi kuniacha hasa kunipa ushauri na mambo mengine kiukweli nilikuwa nampenda sana (R.I.P) kweli bhana faida nilikuwa napata pia kazi yangu ya usajili line sikuiacha baada ya muda kibanda kilijaa kabisa nikaanza kuwa natoa chochote home ili waendeleze harakati
Kwenye swala la kusajili line, nilikuwa nina mwavuli na meza kuna jamaa alikuwa na duka na alikuwa anashona nguo nilimuomba niwe nakaa mbele ya duka lake na kimwavuli changu huyu jamaa mpaka sasa bado ni rafiki yangu ingawa ni mtu mzima jamaa baada ya kuona napata wateja wengi akaleta wazo la kufungua mpesa pale yaani mimi niwe nafanya niksema poa, kweli akatafuta line maana alikuwa na document zote hatimae nikaanza kazi piga kazi piga kazi matunda yakaanza kuonekana make kuna kipindi tulikuwa tunalipwa hadi laki 7 jamaa tulikuwa tumeelewana kuwa atakuwa ananilipa kutokana kam commision ilivyoingia
Aisee baada ya miezi kadhaa jamaa alipatwa na matatizo ikabidi asepe kwa muda so kazi ikaishia pale pale ila bado nyota yangu ilikuwa inang'aa akaja jamaa mwingine naye akanipa line za mpesa na mtaji tukaanza kupiga kazi kipindi hicho line za mpesa zilikuwa 2, ya kupigia kazi na ya kupokea malipo japo sidhani kama mpaka sasa ni hivo, aisee kumbe jamaa alikuja na target zake siku moja nipo kwenye job jamaa akaja anadai anataka line zake zote kuna kitu anaenda kufanya wazee hapa ndipo mzozo ulipoanzia nikampa line ile ya kupigia kazi maana ya kupokea commsion alikuwa anakaa nayo yeye si akanigeuka akasema yeye alinipa line zote mbili nikamuuliza kama ulinipa line zote mbili comision ulikuwa unapokeaje au unaonaje jamaa akaanza kuwaka na kuleta mambo mengi mara hao mgambo nikajikuta kituo cha polisi khaa nikaona lishakuwa tatizo hili kama unavyojua mikwara ya polisi japo nilimkuta mdada ndo alikuwa kama incharge namkumbuka hadi leo alikuwaga mkarimu mno mungu ambariki popote alipo
Mwisho mi nikasema sina hiyo line we ndo unayo ila amua ww unatakaje jamaa akasema nitoe hela tukaiswap hiyo till nikamuuliza gharama aisee alinitajia gharama sijui alikuwa ananikomoa sijui ni ushamba wangu wa kutokujua mambo ni kweli till ambazo zilikuwa hazina majina yako ilikuwa ni gharama kuzi renew ila sio kwa ile gharama
Ilibidi niwe mpole nikamwambia jamaa mi nakuachia kibanda chote na vilivyomo nakumbuka niliuwa nimeweka sola ya wats 20 na betri yake pia jamaa akakubali.
Kila kitu kilivoenda nilimuambia baba mkubwa yangu alinishauri kutoka kata tamaa akanishauri kwajinsi anavyoyajua mazingira ya home inabidi niondoke make nikikaa nitajikuta napagawa na nikweli aliniona maana nilikuwa na mawazo mengi mno ikabidi nimuambie naenda kwa mama ingawa sikuwa na ukaribu naye sana, then nitajua cha kufanya hii ndo ilikuwa mara yangu ya mwisho kumuona baba yangu mkubwa kipenzi sikuju...
Inaendelea...
Hapa tutaona jinsi nilivyokutana na mke wangu mwaka 2015, Baba yangu mkubwa alivyo fariki mpaka nikakosa nauli ya kwenda home kuzika nikaja kusaidiwa na mtu kutoka kwenye mtandao wa x zamanni twitter, mpaka leo sijawahi kumjua maana hakutaka hivo na njia aliyotumia kutuma pesa hakutumia no yake... kuanza mishe za kwenda upande wa pili aisee nyie
Sehemu ya tatu:
Kwanza niwambie mwanangu wa kwanza ana amezaliwa 2017, wa pili kazaliwa 2019 wa tatu kazaliwa mwaka huu 2025 huyu wa nne ana mama yake nitakuja kuelezea kisa chake na huyu ndo maana kwenye watoto wangu sipendagi kumtenga au kutomtaja namjumlisha kwa kuwa ni mwanangu na namtambua so wale mnao hisi uzazi wa mpango sijui nimewajibu
Nakumbuka kilikuwa kipindi cha uchaguzi nilitoka nyumbani na kwenda kwa mama yangu mzazi nilikaa kwake huku nikiplan mishe za kufanya kipindi hicho nilkuwa tayari ni kijana mzima hivo nishaanza kuyatafuta maisha, nilikaa kwa bi mkubwa kama mwezi mmoja nikaamua kurudi kwenye mishe zangu za kusajili line nimepiga kazi kweli kweli nikapata hela ya kuanzia kupanga chumba nikamuambia bi mkubwa akaona wazo ni zuri akanipa mazaga ya kuanzia mfano sufuria, vikombe nk
Ile baada ya muda kidogo napigiwa simu ba mkubwa yuko hoi na anasema niende nyumbani anataka kuongea na mimi neno lake la mwisho, nikiangalia mfuko sina hata mia hapo nasubiri commision ya tigo iingie mwisho wa mwezi commision yenyewe kipindi hiko ni ndogo kinyama make wanakulipa kulingana na wateja jinsi walivyotumia yaani walivyo weka vocha.
Nikajipa moyo wakinilipa tu nachomoka naenda kumcheki mshua mkubwa ni nini anataka kusema, aisee siku maliza siku hata 2 nikaoigiwa simu mzee amezima nilijihisi vibaya na nilijjhisi nina hatia kwanza alisha sema anataka kunipa neno la mwisho pili amezima hajaniona na alivyokuwa ananipenda sana aisee wanaume hatuliagi ila nilijikuta nalia, sasa haraki za kwenda kuzika zikaanza kuna jamaa yangu ni mtumiaji sana wa mtandao wa x zamani twitter hata mimi x ndo mtandao wangubno 1 ninao utumia ukifatiwa na jamii foruma sinaga habari sijui na insta, tiktok sijua whatsapp hajuna, nikampa mkanda mzima jamaa yangu naye ni kama mimi leo nawapa code ukitaka kufanikiwa tafuta marafiki wanao kuzidi kipato ila ukitafuta mnaolingana hamtafikia popote, basi bhana jamaa akalibandika bandiko lile twitter haikupita hata nusu saa jamaa moja akajitokeza kuwa atalipia gharama za kwenda na kurudi nakumbuka ilikuwa 160,000 jumala kwa sharti kuwa hataki nijue au yeye kujulikana kuwa yeye ndo katoa nakumbuka tulitafuta mabasi yanayopokea lipa no akafanya muamala mi nikapewa tiketi jamaa sijawahi mjua hadi leo ila popote ulipo jua baraka zangu ziko juu yako mungu azidi kukupa afya njema na kufungullia milango ya baraka zake yote iwe juu yako.
Nilifika home tukazika baadae maisha yakaendelea.
Ikabidi nirudi town kuendeleza harakati za maisha, Nimekaa muda kama miezi 5 ndo nakutana mama watoto sasa si mnajua ujana tukaanza kutekenyana hivo mwisho wa siku mimba hiyo taarifa za mimba hazikunistua koz hakuwa mwanafunzi ila ni je nitayaweza majukumu hapo ndo lilikuwa swali langu ila katika vitu niliambiwa na mshua ni kuwa hata siku moja nisije kukataa mtoto hata kama nihisi sio damu itajulikana huko mbele nikasema potelea pote nitalea tu hapo plan zangu ni kuwa nitakuwa natuma matumizi nyumbani kwao binti maisha yaendelee.
Wee hakuna mzazi anayependa mwanae kuchezewa afu akaachwa kirahisi rahisi hivo nyumbani sijui ilikuwaje binti akaja getoni nikajisemea labda anatka nikuzie kumbe navyoonyosha kidole gumba cha mguu pembeni ya kitanda nikiwa juu yake ye ananichora tu alikuja saa 11 jioni, saa 12 saa moja hiyo nikamuuliza vipi mma kija home maza hayupo au mbona unajiachia hivi kama haurudi akaniambia ataondoka badae oya saa 4 hiyo usiku mtu haondoki ndo kunichana ukweli kuwa ye ndo ashaolewa hivo khaaa mwanaume nilikuwa na 1000 tu yangu ya kujilia magimbi na chai nilale naletewa habari za kuoa, nikaona ushakuwa msala huu siwezi kimbia ikabidi nivunge nikachukua chipsi za buku tukala huyo tukalala nikaishona kisawa sawa si unajua ukiwa umeoa basi bhana asubuhi ikabidi nifanye mawasiliano nyumbani na kuwapa mkasa mzima kiukweli kwa upande wa familia yetu upande wa baba hatukimbiagi matatizo nikawaelezea kuwa sina hata 100 na kulingana na utaratibu ni kuwa huruhusiwi kukaa na mtoto wa mtu zaidi ya saa 48 hujatoa taarifa, ikabidi home waangalie chakufanya wakamtuma mtu akaja tukatafuta mzee huku wakaenda kwao na mama watoto hio ndivyo nilivyoa
Sasa kimbembe ni kuwa mama watoto ni muislamu mimi ni mkristu sasa tatizo likaanzia hapo aisee hawa wenzetu ni wabinafsi kinoma wakaanza kuleta maswala ya nibadili dini niwe muislamu nikasema aliyewadanganya kamwambie awambie ukweli kwanza nikikumbuka ishu ya maza alivyo niacha na mshua miaka yote kisa tu eti kisa dini, nikawambia hapa sibadili dini kama hamtaki bakini na mtoto wenu aisee hii ishu familia zilianza kupingana zenyewe kuna walio kuwa wanapinga kuna waliokuwa wanasema watuache chamsingi tunapendana aisee mwisho wa siku ikabidi nipewe uhuru wote.
Wakuu katika kitu sitakuja kuwapangia wanangu ni dini mimi nitaplay part yangu kama mzazi kipindi ambacho watakuwa hawajielewa ila wakifika umri wa miaka +18 ruksa kwa yeyote ukitaka kuwa muislamu ni ww, mlokole ni ww, pagani ni ww sijui sabato ni ww maana utakufa peke yako hutakufa na mimi na ww ndo utajibu dhambi zako sio mimi
Nilianza maisha mapya na mke wangu 2016 -2017 tukapata mtoto wa kike kiukweli nilifurahi mno kwasasa ana miaka 8 nikazuri na kana akili japo tunapitia magumu lakini hatujawahi kujutia kukazaa
Mwaka 2017 ndoa yangu inaenda kama mwaka 2 hivi nikapiga bingo kwenye mishe zangu hapo nishaacha kusajili line nimeingia kwenye blogging nilipiga zaidi ya milioni 7 ndani ya mwezi 1 nikajisemea baraka ndo hizi sasa tukapanga na wife hiyo hela tuitumie kujenga kibanda chetu tununue eneo hapa mjini tuweke kibanda aisee mimi nilikataa kitu nachojutia hadi leo kilikuja kunikost tutaona huko mbele mimi nikashauri tujenge home ili kumuenzi mshua maana alikuwa na shamba ameniachia basi bhana harakati zikaanza za ujenzi nikanunua bati msauzi tena wa vigae nikanunua mazaga mengine huyooo home, tukaanza ujenzi yaani kijiji kizima stori lilikuwa ni mimi nyumba ndani ya mwezi ilikuwa isha simama tumefika kwenye papi sijui ndo hilo jina hela ikakata ikabidi tukajipange tena nyumba ikabidi tuwe tumeiacha baada ya muda mambo yakajipa tena nikaenda nikaezeka nikamaliza ikabaki kuweka milango tu wazee hakuna kipindi nimdishi vizuri kama hichi hakuna kitu nilikuwa nakosa maisha yalikuwa safi kinoma, nilimfungulia wife biashara safi kabisa oya.
Picha ikaanza kila kitu kikaanza kujikata pole pole, kwanza ishu zangu za blogging wakanifungia akaunti yangu ya adsense nikajipa moyo nitafungua nyingine nikaendelea kula kupitia ki library changu kadri muda unavyozidi kwenda mambo yankuwa magumu pesa haionekani oya mpaka tukaanza kukosa kodi ikabidi niongee na wife vp ww biashara zako naye kumbe mabadiliko ni makubwa ila eti alikuwa anaogopa kuniambia kwa kuhofia kuwa nitajua amekula pesa aisee nakumbuka ilifika kipindi tukubali kuwa turudi home twende kwenye nyumba yetu hivo hivo milango tutaweka tukiwemo ndani ikabidi niuze vifaa vyangu vya library ili tupate nauli huyoo kiatu mpaka home
Nakumbuka tulifika usiku hapo tayari tuna mtoto wa pili huyu wa kiume, nakumbuka tulilala kwenye nyumba yetu haina milango tulichofanya ni kuweka vibati milangoni tu yaani kueheshea na vyenyewe si kwamba vinaenea yaani ni nusu ina maana mtu akija anaingia anawaona mlivyo lala ila wakuu niwambie kila mwanaume udhaifu wake ni familia yake amini hili niliuwa silali ule usingizi wa kweli yaani mimi ni kukaa nastuka na kuzunguka nyumba na panga langu mkononi nakumbuka tulikaa hivo nikajikusanya kidogo nikaweka mlango wa chumba changu tu kwingine nikapaacha huku tukiwa mimi na wife tunajitahidi kushika jembe yaani mwendo wa kulima kweli maisha ni kama tuliyazoea haraka baada ya muda nikaweka milango ya mbele na nyuma
Shetani hakai mbali na amani wife akapigiwa simu kutoka kwao kuwa kuna mishe na inabidi awepo aisee mambo ndo yalianzia hapo kipindi hicho kwanza kwenda aliwaacha watoto wote wawili kwasababu tulikubaliana kuwa anarudi mda si mrefu oya alivoenda wiki ya 1 ya pili ya 3 ikakata kumbuka hapo naishi na wanangu hawa ndugu watakupenda kwa muda tu usizae ukafikiria watakulelea nikaanza kuona mabadiliko ikabidi nianze kuingia jikoni mwenyewe kwangu na kuwaogosha watoto na kufua hii moment wanangu huwaambii kitu kuhusu mimi wananipenda sana kuliko hata mama yao maana mama yao ilikuwa ni anakuja nakuondoka hapo bado mishe zangu zinagoma kila nikijaribu nashindwa ndani amani sina mishe zangu haziendi oya wife kinacho mpeleka kwao hakieleweki ukipiga simu majibu unayopewa hayaridhishi nahisi lile swala la dini lilifurukuta tena kwahiyo wakawa hawataki arudi nimeishi maisha yalikuwa mabovu kuzidi hata ya town wazee sitasahau nyumba niliona chungu lakini sikuwahi kujuta kuwazaa wanangu, yaani wife kuna muda alikuwa anakuja anarudi yaani ikafika kipindi hajali hata watoto kuna uzi huko nyuma nilishawahi liongelea hili basi ni hivi haya yote kuna mtu alikuwa nyuma yake tena ndugu yangu kabisa yaani kipindi kile naanza ujenzi haraka haraka kumbe hakupenda lile jambo akaapa kuwa sitakuja kukaa ndani ya hiyo nyumba kwa kweli kwa hilo alifanikiwa maana ilibidi mimi na wife turudi town hii tuliambiwa na baadhi ya ndugu tunao elewana saba japo hatukutila maanani hili jambo ila baada ilibidi twende kwa mtaalamu kuangalia shida ni nini mbona tulikuwa vizuri mwanzo mtaalamu akagusia mule mule utafikiri alijua japo hakumtaja ila alisema kuna vitu tayari vimewekwa kwenye nyumba ( hapa kabla ya kwenda upande wa pili nishajaribu maombi mengi na wana maombi wengi walishakuja kuiombea nyumba ila wapi hapa ndo tuliamua kwenda uoande huo maana kuna msemo maarufu unasema muombe mungu huku na wewe ukionesha jitihada mungu atabariki jitihada zako ilimradi sio za kumdhuru mtu ) na tulipo rudi town amani ikatawala tukaanza upya kujipanga ukweli tulipo fika tena mambo yakajipa tena nikatoboa tena
inaendelea.... naleta sehemu ya mwisho
Hapa nakumbuka haka kipindi ungenikutana ungesema kweli maisha ni mazuri, ila shetani naye alikuwa bado anacheza na sisi kwa nara nyingine tena wife akashauri turudi home kwenye nyumba yetu maana kipindi tuko huku tukikuwa tunatuma pesa inarekebishwa mdogo mdogo hapa sasa ndo chanzo cha mimi mpaka leo nastrugle ila wapi japo naamini bado nitafanikiwa