JamiiForums ina mambo

Mleta mada nilishakuambia. Kwenye mitandao ya kijamii, "unaweza kuwa mtu yeyote tu unayetaka kuwa". Unaweza kuwa:
1. Mwenye hekima
2. Mpumbavu
3. Tajiri
4. Masikini
5. Mgonjwa
6. Mzima
7. Mtakatifu (sana)
8. Mdhambi (sana)
Kwa hiyo endelea tu kuchukuliana nayo mkuu.
 
Namaanisha Kama wengi duniani wanavyotumia google kupata majibu ya kile wanachokitaka pia baadhi ya watanzania wanaitumia jf kupata solution kwa matatizo yao.
Sio ukiitaka JF lazima Ugoogle?

Uzuri ni kuwa ukisearch kitu google kwa lugha ya Kiswahili basi unaletewa kwanza machaguo kutoka Jamiiforums.
N
 
Hiyo #1 kwamba watu wanakomenti kufuata alichokoment mtu wa kwanza sikubaliani nalo hasa ila ila hiyo ya like ni kweli kabisa,ukifungua thread hesabu post nane au kumi za mwanzo hata kama hazi-make sense basi utakutana na like balaa ila baada ya hizo ukisogea sogea hadi #20 hata kama zipo zilizojaa elimu na weledi unakuta zina like 1/2.ila hayo mengine yote mkuu screpa yupo sahihi.
 
Ndio nini? In Joti's voice.
 
Baada ya kugundua mtu fulani ndugu yangu naye ni member wa Jf huwa namtoa povu kila anacho post kwa kumwambia vitu kwa kujifanya kukisia kumbe ndo ukweli wenyewe ..utakuta namwambia "inaonekana hata elimu yako ni ya kuunga unga kutokana na kufeli". basi atavimba kwa kujidai "bwana mdogo......... " .
Kwahiyo JF wengi wanatoana mapovu kwa makusidi kabisa.
 
Unaweza kukuta ni rafiki yako, mnaongea vizuri, mnajuliana hali n.k lkn JF mna bifu mnatukana matusi makubwa makubwa ya nguon huku mkiwahusisha baadhi ya ndugu zenu.
Lkn upande wa pili utakuta jana tu umehudhuria happybirthday ya mwanae na zawad umetoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…