Tatizo unachukulia kila jambo humu sooo serious utaumia Buree...
Hahahahahaha hii thread imenichekesha hadi watu nilio panda nao tren ya umeme kutoka Los Angel kwenda New York wote wamenishangaa nacheka nini!
Unajua New York nimenunua Apartment kwa hiyo naenda kuingalia!
Lakini kilicho nishangaza kwenye hii treni ni usumbufu wa wahudumu maana kila muda Mara wamekuuliza utakunywa nini? Ukiwambia chai wanakupa na baga na ukiwambia Soda wanakuletea cret zima! Kwakweli ni wasumbufu sana!
Hapa nilipo wametoka kuniuliza ninataka kusoma nini muda huu nikawambia wanipe Kitabu cha Think Big cha Ben Carson au Gazeti La New York Times...kwakweli huku hakuna Uwazi wala Risasi!
Daaa kwakweli ni usumbufu mtupu halafu nimegundua kabisa kila Muhudumu humu ana Masters ya Customer care and economics!
Kwakweli wana Jf nimejuta kupanda hii treni lakini ni uzembe wangu wa kuchelewa flyt baada ya kutumia muda mwingi kujiandikisha masomo ya PhD kwenye chuo kimoja maarufu duniani kilichopo huku Marekani!
Ngoja nishuke naona treni imekaribia na kuna Profesa mmoja ananisubiri anataka nimsaidie kuandika Thesis!
Cc
wakishua Evelyn Salt!
brenda18 Dina Khantwe