Jamiiforums kuna matajiri tupu

Jamiiforums kuna matajiri tupu

jembe afrika Ni kweli unayosema asilimia kubwa ya watu wenye halinzuri ya kiuchumi wapo hapa jukwaani. But you have to take it as ana advantage, we huoni raha kubadilishana mawazo na wafanyabiashara wakubwa, viongozi wa siasa kama wabunge, ma celeb kama miss chagga , MziziMkavu , Bujibuji Nawengineo kibao, Siwezi kukwambia ni wa kina nani kwaajili ya kuogopa Ban La namecalling lakini habari ndio hiyo.
 
Huenda kuna ukweli japo jf kuna na uongo mwingi kwani hata ID nazo ni fake.
Ila nakubali kwamba mpaka uingie mtandaoni simu yenye uwezo wa kudown-load inahusika au kompyuta,chaji ya simu nikimaanisha umeme na muda wa kukaa kuchangia hoja si mara nyingi utamkuta maskini anajihusisha na mitandao.
Kwako unayepanga,mi naona una uwezo kwani hicho chumba si unalipia? kwa maneno mengine wewe ni mfalme kwa anayekupangisha,maana unamwingizia hela.Hivyo jione na wewe ni tajiri na endelea kuitumia JF.
kwa hiyo nisisepe mkuu,maana nishaingiza upepo.....
 
Habar ndio hii humu jf raha sana fake ID threads, comments, yan kila kitu tuvumiliane jaman looo
 
Kwakweli huwa nacheka sana maana thread za huku ndani inaonekana kila mtu mambo safi, anadrive, ananyumba, ofisi safi, anaenda nje mara kwa mara, je sisi tuliopanga na tuna baiskeli tu

Tuendelee kulogging in au tusepe, maana ukitafakari ni zaidi ya uswiss na marekani.


Wacha woga mkuu,maisha ni mapambano
 
mm ni mpandaji mzuri sana wa madaladala huwa nawafuma baadhi ktk usafiri huo tena wakiwa busy ktk kupost issue ni watu wa kawaida mno kwa niliowabahatisha!
 
......... , je sisi tuliopanga na tuna baiskeli tu

Tuendelee kulogging in au tusepe.... .

Kumbe hata wewe ni tajiri! mie sina baiskeli na naishi kwa bibi, lakini humu JF hanitoi mtu, mods wenyewe wamejaribu kunitoa humu but in vain!
 
Ila mie ni mkweli daima.Kingine ni hiki cha watu wengi kuwa ni watu wa Dar,Arusha,Mbeya,Mwanza,Moro.Yani et ni watu wa mikoa mikubwa tu.
Pia suala la level elimu ni shidaaaaah
 
Back
Top Bottom