Jamiiforums kuna matajiri tupu

Jamiiforums kuna matajiri tupu

Huenda kuna ukweli japo jf kuna na uongo mwingi kwani hata ID nazo ni fake.

Ila nakubali kwamba mpaka uingie mtandaoni simu yenye uwezo wa kudown-load inahusika au kompyuta,chaji ya simu nikimaanisha umeme na muda wa kukaa kuchangia hoja si mara nyingi utamkuta maskini anajihusisha na mitandao.

Kwako unayepanga,mi naona una uwezo kwani hicho chumba si unalipia? kwa maneno mengine wewe ni mfalme kwa anayekupangisha,maana unamwingizia hela.Hivyo jione na wewe ni tajiri na endelea kuitumia JF.

Kumbe hata mie mambo safi .ilikuwa najidharau basi tu.
 
Nimepanga likizo niende vacation NEW YORK ...naomba kampani yako MankaM...
 
Last edited by a moderator:
Na mimi nnae umwa mafua, niko huku Uingereza Potland hospital, nawasalim tu....
 
  • Thanks
Reactions: kui
Kwakweli huwa nacheka sana maana thread za huku ndani inaonekana kila mtu mambo safi, anadrive, ananyumba, ofisi safi, anaenda nje mara kwa mara, je sisi tuliopanga na tuna baiskeli tu

Tuendelee kulogging in au tusepe, maana ukitafakari ni zaidi ya uswiss na marekani.

shehe bora wewe unabaiskeli wengine tuna piga tembe katembe mwanzo mwisho mara moja moja daladala hutusevu kusiko fikika.
 
Na mimi nnae umwa mafua, niko huku Uingereza Potland hospital, nawasalim tu....

pole sana ungekuwa huku kijijini kwetu ningekuchumia majani fulani unuse mafua kwisha kabisa ila kwasababu nawew ni tajiri ndio bas tena looo
 
Jina lako fake kila kitu lazima kiwe fake,......usijitaabishe sana yote haya yanafanya kijiwe chetu kiwe kizuri sana,bila haya kijiwe kingekuwa bored.
Well said, tutaabishwe na erikali, ada za watoto hakuna, kodi za nyumba juu, barabara foleni tupu, maji hakuna, yaliyopo ni ya chumvi, kigodoro kimepigwa marufuku, bia bei juu, ajira hakuna, katiba mbaya, Wapenzi wetu nao siku hizzi kila mtu yuko kimkakati zaid!! Ngoja tufurahie maisha ya JF aiseee, huwezi jua kuna watu saa hizi wanapost huku wanalia (wanajifariji tu).....kitanda Muhimbili buku tano, kulala tu na Dokta ajakuona bado, na sio ajabu akija akufanyie oparesheni ya kichwa badala ya mguu. Tapu tupu
 
Twende ukasafishe nyota...bibie.....ushawahi kunywa chai Hollywood....???
 
Niko zangu Ny nataka mchepuo wa bongo nimtumie nani ticket?
 
Ngoja ni parki benzi langu hapa kisha niwajibu .ooh nimesahau funguo za nyumba yangu pale ofisini TRA duuu

Aisee..nipo kwako huku juu nakusubiri...au niswim kidogo wakati nasubiri urudi😉
 
pole sana ungekuwa huku kijijini kwetu ningekuchumia majani fulani unuse mafua kwisha kabisa ila kwasababu nawew ni tajiri ndio bas tena looo

Hebu sema uko kijiji gani nitume chopper langu sasa hivi. Mafua yamenibana hapa na ninahitajika Zurich to sign a multi million euro business deal. My private doctor has advised me not to travel in this state.
 
Back
Top Bottom