Nawasalimu wakuu...
Nafurahi sana kuiona Jf ikikua na members kuongozeka sana!! Nimetumia muda mrefu kidogo kusoma kinachoandikwa hapa jukwaani kwa sasa nikifananisha na tulikotoka...
Naona sasa hivi kuna vitu hata watu ambao havi/hawaendani kabisa.
Nakubaliana na mabadiliko kabisa kabisa...
Kama ilivyo kwenye nyanja nyingine mfano soka, kikapu hata mchezo wa pete(netball)
Watu wana wika na ku potea lakini bado kuna namna ambavyo ubora wao hausahauliki...
Bila chuki, wala hiyana kuna watu ni ma legendary hapa, wengine bado wapo, wengine hawapo au wamebadili ID zao ili kuendana na wakati uliopo...
Sasa nitatumia uzi huu kutambua hawa watu.
Kwa Lugha Nyepesi nitawaita JF Legendaries of All Time.
Unaewika sasa hivi usijali sana utakuwa Legend wa baadae...
Si vibaya na wewe ukawatambua kwa kuwataja Malegendari wachache...
Mnakumbuka JF wings!! Arusha Wing, Mwanza Wing, Dar es Salaam Wing?
Naanza sasa na kwa heshima kila mmoja tumpe comment ya pekee.