LGE2024 JamiiForums na StarTV kuwahoji wanasheria kuhusu Hali ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa leo Novemba 23, 2024

LGE2024 JamiiForums na StarTV kuwahoji wanasheria kuhusu Hali ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa leo Novemba 23, 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Huyo mwanasheria wa ccm naona analeta vichekesho, anajaribu kuonyesha mgombea binafsi hata akishinda itakuwa ngumu kufanya kazi na mfumo hasa kupatiwa hela za maendeleo! Anajaribu kuonyesha ni hatari kuchagua kiongozi nje chama kilichoko madarakani eti, kisa atakuwa hachezi mziki wa ilani ya chama kilichoko madarakani.

Sasa najiuliza kama ni ngumu sana pesa za umma kumfikia kiongozi wa upinzani au mgombea binafsi kihalali kwa maendeleo ya wananchi wa eneo husika, zile pesa zinazoripotiwa kupotea kwenye ripoti za CAG inawezekanaje wakati ni ngumu hivyo hata kumpatia kuongozi aliyechaguliwa kihalali kwa shughuli halali?
 
Nilimuona kwenye sherehe za Mapinduzi zilizofanyika Zanzibar mwaka huu alikiwepo.
Huyo bwana ni kama "kifaa cha jeshi" alicho kuwa akikizungumzia marehemu Magufuli.
Wapiga picha na waandishi wa habari wanalielewa hilo.
 
Back
Top Bottom