Research Solutions TZ
Member
- Jul 11, 2020
- 66
- 145
JamiiForums ni bidhaa ya Kitanzania iliyoundwa na watanzania kwa ajili ya watanzania. Rais wetu amekuwa akisisitiza sana Raia wetu kutumia vitu vyetu ili kukuza uchumi wetu lakini naona yeye ana account Twitter, Facebook nk lakini sioni akiwa na account yake JamiiForums ambao ni mtandao wa kitanzania
Hivyo namuomba Mheshimiwa Rais atoe maagizo kwa idara na taasisi zote za serikali kuwa na account JamiiForums ambazo zitakuwa verified ili watanzania wapate taarifa kutoka kwenye mtandao wao badala ya kusubiri Twitter ambao ni mtandao wa Marekani.
HOJA ninazoweza kujibu nikitofautisha na Twitter
Pascal Mayalla alisema twitter kumejaa matusi na aliomba ikibidi Twitter ifungiwe Tanzania, naamini hata matusi yanaweza kuwepo JamiiForums lakini tofauti ni kuwa ndani ya JamiiForums Uzi unaweza kufungwa ili mtu asikoment chochote mara baada ya Rais kutoa taarifa ya shukrani, pongezi au teuzi.
Aidha mtandao wa JamiiForums una namna nzuri ya kutoa matusi hata kama hayajaripotiwa kwa Mods hali inayoweza kuhakikisha mambo mazuri kwa utaifa.
Umuhimu wa yeye kuwa JamiiForums
Itaongeza idadi ya watu wanaotembelea JamiiForums na kuifanya JamiiForums kuzidi kukua, pia itafanya watu wachunge maneno yao, halikadhalika watu watajisikia huru kuuliza mambo mengi zaidi ndani ya JamiiForums na kupata majibu ya papo kwa urahisi.
Aidha kama ilivyoazimiwa kwa watendaji wa Serikali kutumia TTCL mtandao wa Nyumbani, ni vizuri kwa Rais kuonesha mfano na kuamrisha idara, asasi, taasisi na mashirika, wizara na ofisi ya rais kuwa na akaunti JamiiForums.
Nawasilisha
Narudi zangu kusolve some Mathematical Equation