JamiiForums ni bidhaa yetu, kwanini Rais haitumii?

Magufuli tunaye humu, naye huwa anaambiwa "kachukue posho ya buku 7 pale viungani vya Lumumba".
Hiyo ndiyo raha ya ID fake.
 
Mkuu kama anatumia ID. za kubumba kama zetu utamjuaje? au unapendekeza awe verified user..

Mwacheni Mkuu atumie ID yake ya kubumba kwani kwa utamaduni wetu akitumia VERIFIED ID badala ya kujadili hoja watu mtaanza kutukana matusi na huo sio ustaarabu!!! Yumo ndani ya JF siku nyingi na anashiriki, pamoja na kuchota hekima anazozikuta humo na kuzitumia!!!

Hakuna haja ya kumjua mbona mko wengi tu humu msiojulikana!!
 
Ebu jaribu kuziangalia kwa jicho la tatu ID za Bia Yetu na Kawe Alumni ambazo hujitokeza sana nyakati za uchaguzi, huenda akawa ndiye mmiliki. Jina Bia ama Pombe kuna msigishano fulani wa kiaina.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe Bwana rais wetu ana kazi nzito? Mungu amlinde na amdumishe na majukumu mazito ya kuliongoza taifa?
 
Aliyekuambia humu hayupo ni nani?

Tembelea thread ya "sema chochote upate likes"





Cc: mahondaw
 
Humu watanzania wengi wamo ila kanuni ya hapa ni matumizi ya majina ya kufikirika ndio maana tunatumia neno "mkuu" kwani unaweza ukawa unajibizana na mtu ambaye huko mtaani ingepaswa umuamkie kwani kakuzidi umri au cheo.

Jambo la msingi hapa ni kutumia huu mtandao vizuri kwa kujibizana kwa hoja na kuibua mambo ambayo yatalisaidia Taifa.
 
Inawezekana yupo ila ID yake haiwezi kuwa wazi kwa sababu wamiliki wa JF hawatoi siri za wateja wao kizembe jambo ambalo yeye nina uhakika halifurahii...kuweka wazi akaunti yake ya humu ni kubariki Yale asiyoyaamini
Si hata twiter hawatoi siri zawateja,na ipo account yake,

vivyo hivyo ni vema awepo as verified one.
ili tuhamasishe uzalendo wa kutumia vya ndani.
 
Kwenye ule uzi wa jf usiku wa manane hua tupo nae akiwa anasoma mafile yake kitandani
 
Anazo akili za kuandika chenye maana? Ukisoma makala za Bensa8 juu ya uwezo wa kiakili wa huyu mtu, unabaki unajiuliza hv watanzania tulirogwa na nani kumpa mamlaka makubwa hivi?
Wale wale mliopigwa dole na kuachwa, mna hasira lakini ndo hamna uwezo wa kumfanya chochote.
Bado Minne na miezi kumi, mtapta taabu sana nyie Vimbulu.
 
Wewe mleta uzi,unajuaje kama hayumo humu?
Au pengine ni ndiye anayeandika hapa?


Nasema uwongo ndugu zangu?
 
Ebu jaribu kuziangalia kwa jicho la tatu ID za Bia Yetu na Kawe Alumni ambazo hujitokeza sana nyakati za uchaguzi, huenda akawa ndiye mmiliki. Jina Bia ama Pombe kuna msigishano fulani wa kiaina.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app

Sikubaliani na wewe, hizo ID kuwa active kwenye chaguzi ni moja ya pingamizi kuwa Mzee asingaliweza kuwa na muda wa kutosha kuandika vile.

Pia, hizo ID ni sharp mno... Mzee ni mzito hawezi kutype chaap vile.

Yupo humu ila kwa ID fulani dormant ya kusomea tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…