JamiiForums ni kiboko, imenipa kazi mwenzenu

Anza kazi kijana kwa kampuni ambayo unadhani utaenda practise ulichosoma for Career Advancement.
Pia kumbuka hautakiwi in life kubweteka na mshahara you need to have altenative sources of income could be vibiashara vya apa na pale etc
 
Nenda kapige mchongo huo.
 
nenda kaanze kazi .utakuwa na ujuzi na itakuwa rahisi kupata kazi nyingine.........maisha ni kupanga/kuchagua ukitaka ya hali ya juu hautatosha ukitaka maisha ya kawaida utapanga na utaona mambo yanakwenda kutoka na mshahara wako
 
400,000/= ikikatwa kodi pamoja na nssf unabaki na kama 320,500/= sio mbaya, you should go for it wkt unatafuta maali kwingine!...kuna mshkaj wangu anafanya kule posta analipwa 300,000 net na anaishi kimara mbona anayamudu maisha vizur tu
 
Huo mshahara ni mdogo, lakini ni rahisi kupata kazi nyingine wakati ukiwa na kazi kuliko unapokuwa huna kazi. Uzoefu wangu: Nikiwa graduate nilianza na kazi ya 270,000/= , baada ya miaka miwili nikapata experience wanayo taja kwenye matangazo ya kazi, nikaomba kazi sehemu ingine at least kwa sasa hivi napata mara 4 ya hiyo ya kwako.

Ila usisahau kumchangia huyu kaka yako ambaye umepata kazi kupitia kwake ili naye aweze kuendelea kuishi katika dunia hii......Nina maana ya changia Jamii Forum
 
Hongera mkuu ....!!, chukua hiyo kaz kama pa kuanzia, kisha chakalika mpaka ufikie malengo yako ...
 
You must be jinias aiseeeeee........ila mkuu wewe noma unaamka na kuanza kupika??
 
...1)Hiyo uliyopiga 6*12*300,000 ni umezidisha tu 300,000 kwa miaka sita, haujaweka interest .

Hapo nilikuwa najaribu kusema hata kama ukiamua kuweka hiyo pesa yote ambayo ungeweka kila mwezi kwa miaka sita wakati unaanza (badala ya kufanya hivyo kila mwezi!) huwezi kupata interest itakayo kufanya uwe na kiasi cha pesa cha shiling milioni 150 baada ya miaka sita (katika rate hiyo ya 8% pa, compounded monthly).


Hiyo fomula A = P(1+r/n)^ nt (A ni amount including interest baada ya ya miaka hiyo sita, P ni principal, let say unaweka hizo 21,600,000 (=6x12x300,000) zote kwa mkupuo mmoja wakati unaanza badala ya kila mwezi ambayo kwa hoja yako tunategemea ilete amount kubwa zaidi, halafu r ndio rate yaani 0.08 (8%) kwa mwaka, n ni mara ngapi katika mwaka compunding inafanyika, let say ni kila mwezi na hivyo n itakuwa 12, halafu t ni muda (katika miaka) wa hiyo fixed deposit, yaani miaka 6).

Mimi nilifanya hivi hiyo hesabu:

P=21,600,000
[r/n = 0.08/12=0.0066667, nt =12x6=72]
1+r/n = 1+0.0066667=1.0066667
(1+r/n)^nt=(1.0066667)^72= 1.6135060140746 (type kwenye excel "=power(1.0066667,72)" au hivi "=1.0066667^72")
A = P(1+r/n)^ nt = 21,600,000 x 1.6135060140746 = 34,851,729.9040113

Labda kama kuna mahala ninakosea katika fomula hiyo!

Ukitaka kuitizama vema ni lazima uzingatie kuwa bank baada ya wewe kufanya deposit wanampa mtu mwingine anayehitaji mkopo (say kwa kipindi hicho cha miaka 6) kwa interest ambayo itakuwa kubwa kuliko 8% (i.e. kunakuwa na 'spread')...so strictly speaking anayekulipa interest sio bank bali ni mteja aliyekopa hiyo pesa ambayo wewe ume deposit bank. Sasa jaribu kufikiria leo hii mtu akikopa bank tzs 21,600,000 anaweza fanya biashara gani katika miaka sita ili akuze mtaji huo hata kufika zaidi ya tzs 150m (ili yeye abakie na mtaji/faidia, arudishe bank pesa yote aliyokopa na interest juu -bank ipate faida yake na baadae pia kukupa wewe uliye deposit tzs 21,600,000 kiasi cha tzs 150m karibia faida ya shiling 128m!). Hapana....labda kuna kitu sijaelewa/sielewi hapa.
 
Piga mzigo huo ili upate uzoefu, hakuna mtu atakaye anza kukulipa 4 mil. wakati huna uzoefu, jenga njia kwanza ndiyo upite. unataka kupita kwenye njia wakati hujaisafisha?
 
Hivi kwani ulipokuwa unatafuta kazi ulitarajia mshahara wa kiasi gani??? Na nani aliyekuroga kuwa mshahara huo hautoshi?? Acha dhihaka wewe...Usijaribu kulinganisha maisha yako na ya watu wengine?? Wewe ndo unayejua kwa kiasi gani unahitaji kazi..Ndo maana ukatoka huko kijijini ukaja mjini!!! Kama sivyo ungebaki hukohuko uendeleze kilimo kwanza!!! Chukua kazi hiyo wewe acha uzembe na ukianza kazi usiwe FISADI kwa kujitafutia UTAJIRI na MAFANIKIO ya WIZIWIZI....Na ukianza kazi tu hama mara moja kwa huyo jamaa yako....Maana kama yeye anamshahara wa mamilioni utajiona kazi yako haikufai wewee!!!!
 

Haya majibu ni ya kijinga sana. Ulitakiwa kuweka mchanganuo wa jinsi hiyo hela inavyoweza kutumika kwa mwezi na siyo kujaza ujinga wako wa kuhudumia nyumba ndogo. Yaani unataka mtu aanze kupokea rushwa au kuiba siku ya kwanza kazini?

Kwa aliyeomba ushauri
Daima mwanzo ni mgumu. Jaribu kujinyima vitu visivyo vya msingi huku ukitengeneza jina na CV yako. With time utapata kazi yenye kulipa vizuri zaidi.
 
Mkuu kweli wewe ni mzee wa budget,...ila siku ukioa kumbuka kubadilika maake_mmmmmmh
 
Nenda kafanye kazi. Cha maana zaidi ni kuweka mipango juu ya (1) Career development (2) Personal development. Members wengi wameshauri juu ya umuhimu wa kuepuka matumizi mabaya na kutafuta njia zingine za kuongeza kipato. Elewa kuwa muda ni kitu muhimu sana tafadhali uwe na mipango mbalimbali juu ya maisha, ikianzia ya muda mfupi na ya muda mrefu na kila mpya lazima ufanye monitoring & review.
 
Hongera sana .
Kama huna kazi kabisa ni bora ukasign contract na moja ya hizo kampuni,leo na kesho utapata kazi nyingine kwani utakuwa upo ndani ya soko la ajira .Uzoefu na social capital utakayoitengeneza ukiwa kazini itakuweka sehemu nzuri baadae.
 


Kwa hii hesabu naomba mkuu ufungue benki ili nije kuweka pesa zangu. Kwa kifupi mkuu kwenye hii computation yako umefanya kitu kinaitwa 'Multiple inclusion of entries' ambayo imekusababishia kupata 'Exaggerated output'.

Ukifanya hiyo hesabu vizuri kwa formula yako ya P(1+r/n)^nt huwezi kupata zaidi ya 35M kwa kipindi cha miaka 6. Kama namba hazikwei siku hizi kuna software kibao. Mfano hii hapa:


Compound Interest Calculator
 
Piga kazi wewe acha utani. Ngoja nikupe story kidogo

mimi nilimaliza shule 2009 nikapata mchongo Arusha. kama mnavyojua Arusha hakunaga mchezo hakuna njegere za 150 wala 200 ni noma lakini nilianza na Mshahara basic 395,000 na niliripoti mzigoni bila kujishauri...nikapiga mzigo huku natafuta better position, uzuri waliniweka sehemu nzuri ya Creditors kwa hiyo nikawa nawasiliana na supplier wengi sana na nilikuwa napiga kazi kwelikweli....baada ya miezi sita nikaitwa na kampuni moja baada ya kuappriciate kazi yangu kwenye kampuni nililokuwa... wakaniahidi kunipa Net ya 420,000 faster nikasepa maana kwanza nilikuwa bado nipo Probation.... nikachapa kazi pale mpaka probation ikaisha....ilipoisha jamaa waliniappriciate na kunipa gross ya 828,000 na hapo sasa ilikuwa ni 2010. wakanipa chance kama junior accountant tu. baada ya miezi sita ikafika increement na wakanipa 850,000 net. wakati huo pia nilikuwa napiga kazi huku naangalia upepo..... ilipofika April 2011 nikakutana na jamaa ambao nilikuwa nadeal nao sana ( infact waliomba nikutane nao wanataka Accountant) sikuvunga...nikakutana nao full maujanja ni kama ilikuwa interview hivi japo sikujua wanataka nini, wakaniuliza nafanya nini na napata ngapi? baada ya week mbili wakaniletea nisign Appointment ya 1.4M net wananitaka nifanye kazi kwao....sikuvunga nikasepa nikaenda kuanza nao......leo hii hata sikwambii napata ngapi tena...kwahiyo cha msingi ni wewe upate kazi kwanza then ujimarket mwenyewe ile mbaya.
 
Kwa hii hesabu naomba mkuu ufungue benki ili nije kuweka pesa zangu.
Hata mimi nipo tayari kukopa sehemu yoyote hata milioni 100 na kuweka kwenye hiyo benki yake!
 

kama jama amekusoma sasaivi anaenda kusaini mkataba maana maneno uliyompa ni mazito sana.
 
du hongera mimi nikimaliza chuo sijui itakuaje yaani we acha tu jamani.
 
You must be jinias aiseeeeee........ila mkuu wewe noma unaamka na kuanza kupika??

Ahaaaaa, mkuu! hilo tu?! kama kuna jambo gumu ktk kazi zangu binafsi basi hilo la kuamka saa 11 alfajiri na kupika c moja wapo!!! mbona cmpo tu wangu! kwanza, b4 cjaenda kulala, nahakikisha nimesafisha sufuria la kupikia pamoja na kuosha mchele ( na kuchuja maji yote). Nikiamka tu saa 11, ki2 cha kwanza ni kuchemsha maji kwa jagi la umeme, dak 1 yanakuwa tayari kisha nayatumia maji haya niliyochemsha kubandikia msosi wangu! Nikishaweka tu sufuria jikoni, nakimbia mara moja bafuni kwa ajili ya kuoga na ninaporudi huko nakuta tayari msosi ushakaukia! Nikisharudi toka bafuni, ki2 cha kwanza ni kupunguza moto na kugeuza ubeche na kufunika.....ninapomaliza kujipangusa maji, msosi nao unakuwa tayari.....no one minute is lost unutilised! jaribu hiyo ki2, utakuja gundua maisha iz very ize, ni kujipanga tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…