Kuna panya amekuwa anatusumbua hapa. Anakula mlango. Sasa wife kumbe alinunua sumu ya Redox ya kuulia panya, ndo kaniomba niweke japo sipendi kuua hawa viumbe. Ikabidi niende jikoni kuleta nyanya kisha nikamtengenezea panya kachumbari. Shida imekuja ni kwamba nimesahau kuichanganya na mafuta sasa harufu ikasambaa chumbani. Imebidi tukurupuke na watoto hadi sebuleni. Baada ya nusu saa nimeitoa hiyo sumu ndani ila hadi sasa ni saa moja na nusu imepita bado sipo vizuri. Nimenawa na sabuni mara kadhaa lakini kisaikolojia bado sipo poa. Hata nikiwashwa kidogo nahisi inatenda kazi. Ngoja nisali kisha niungame makosa nilomkosea wife. Nilale.