JamiiForums Usiku wa manane

Jamani kwaherini naona wale paka walioimbwa na Mwinshehe wamehamia mtaani kwangu...
Ama kweli uswahilini tabu tupu....bundi wakilala paka wanaamka.

Itabidi nihamie mtaa wa kumi,sina namna nyingine
Hahahaha palipo na Bundi hapakosi paka, na Hawa viumbe hutegemeana kwa asilimia kubwa[emoji40]
Vumilia tu hao ndo jirani zako wa kwenye viroba na balimi[emoji125]
 
Kuna kitu kinaitwa jinamizi, unakua nusu macho nusu umelala hauwezi hata kunyanyua kidole, sasa likiibuka hiyo mida si itakua tafrani? Ntaanzia wapi kuutangazia umma?
Hahaha jinamizi wao kazi yao sio hiyo, na hawawezi fahali wawili kukaa pamoja lazima mmoja amwache mwenzake afanye kazi akimaliza na yeye akipata chance aanze[emoji40]
 
Hahaha jinamizi wao kazi yao sio hiyo, na hawawezi fahali wawili kukaa pamoja lazima mmoja amwache mwenzake afanye kazi akimaliza na yeye akipata chance aanze[emoji40]

Sasa hapo ndio wazee wa kutafsiri muvi kiswahili wanakwambia naaaam, intamisheni! Wakati jinamizi linakuachia, babalaao popobawa nae anatua mithili ya mwewe, hapo hata kama uko macho utakubali matokeo tu.
 
Jamani kwaherini naona wale paka walioimbwa na Mwinshehe wamehamia mtaani kwangu...
Ama kweli uswahilini tabu tupu....bundi wakilala paka wanaamka.

Itabidi nihamie mtaa wa kumi,sina namna nyingine

Mze wa busara...akilia nyauuu!!!! Zamani kulikua na mziki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…