Usiige: Ilikuwa hivi: nikiwa mgeni, siku moja nilikwenda kibandani kwake nikanunue mchele. Nilipofika nilimkuta kalala chini kwa ndani.
Nilipomsalimia niligundua alikuwa analia kimyakimya. Alifuta machozi ndipo aliinuka. Nikamchokoza kwa kumpa pole kwa kuumwa akajibu asante. Nikaondoka bila nyongeza.
Siku nyingine nilienda tena. Nikamkuta yuko kawaida na furaha yake. Nikamtania, akatabasamu na kuniuliza anisaidie nini. Nikamjibu mchele na furaha yake. Akacheka akanipa mchele na kusema furaha nitaipata nyumbani kwangu. Nikamwomba namba ya simu ili awe ananitumia hata mtoto aniletee mchele kwani alipafahamu ninapokaa. Alisita lakini akanipa kwa sharti kwamba anaamini nitakuwa na matumizi sahihi ya namba yake. Nikamwambia hilo uhakika 100%.
Muda wote nikimwangalia, navutiwa na utulivu katika kuongea, sauti nzuri na umbile lake japo kwa kumwangalia tu niligundua alikuwa afya dhaifu kuliko alivyopaswa kuwa. Kwa kuwa ni Mbeya nikahisi ana ngoma. Nikajipa muda kumchunguza. Nikagundua kwanza kaolewa, swali likawa kwanini anaonekana dhaifu? Nikaanza kuchunguza uzao wake kwani alikuwa anashinda na watoto wake hasa weekends. Nikagundua wako safi.
Siku moja nilimtumia sms kwa mara ya kwanza. Kwa kuwa hakuwa na namba yangu kama kawaida akauliza mwenzangu nani. Nilimjibu, mteja mgeni wa mchele. Yupi? Uliyempa namba. Akaonekana kunitambua chapu. Nikamwuliza, naweza kukupigia akasema ana kazi, akimaliza atanijulisha nimpigie. Hakufanya hivyo jioni ile badala ya alifanya jioni ya siku ya pili majira ya saa 3 usiku. Alituma ujumbe kuuliza kama nina nafasi nimpigie. Nilijikausha hadi siku ya pili muda kama uleule nami nikamwuliza una nafasi nikupigie? Akajibu karibu.
Nilimpigia nikamwomba radhi kwa kutopiga jana yake. Akasema hakuna shida ila alipata wasiwasi huenda alinigonganisha na mkewangu. Nikamwambia ninakaapekeyangu. Kwanini? Nikamwambia nisingeweza kuhamia mazingira mapya nikiwa na familia moja kwa moja. Akanielewa. Niligeuza swali lilelile kwake kwamba ninajua ni mke wa mtu, anapataje jeuri ya kuongea muda ule. Akasema hayupo. Nilimdadisi hadi akanieleza.
Nikahamia kumwuliza sababu ya kulia siku ile. Akasema mambo mengine ni ya ndani hawezi kunambia. Nikakubali. Tukaagana tulale.
Nilijifunza kuwa anatatizwa na ndoa, japo sikuwa na uhakika 100%. Tuliendelea kuchati mara mojamoja. Hakuonesha kuvutiwa sana na bidii yangu kumsalimia mara kwa mara. Niliendelea kumchatisha kila ninapopata nafasi. Mara chache alijibu. Siku moja nikamwomba nikutane nae sehemu nikae nizungumze naye jambo fulani. Alinambia hana nafasi hadi apate mtu wa kubaki kibandani. Nilimwomba akipata nafasi anitafute, alikubali.
Ikawa mumewe akiwa nyumbani ananiambia mumewe yupo, nami nilikaa kimya. Akaanza tabia tofauti. Mume akiondoka alinambia naweza kuchati mumewe hayupo. Tulienda hivyo kama mwezi miezi miwili.
Siku moja nikiwa sina imani kama ataniambia ana nafasi, nikapokea sms akisema, ametembelewa na mdogo wake, hivyo nimwambie lini ninataka nimutane nae kwa kuwa kubandani atabaki mdogo wake. Nikamwambia apange yeye. Alinipa ratiba na mahali pa kukutana ikawa amekubali kuja geto kwangu. Akaniambia ananiheahimu, asingependa kufanyiwa kitu chochote kisichokubalika. Nikamwambia sina kabisa hiyo tabia. Atafika na kuondoka bila madhara yoyote.
Kweli alikuja, ilikuwa kama saa nne asubuhi, alifika geto. Nilimwambia nimegundua anamsongo wa mawazo. Akasema siyo kweli. Nilimwambia ningependa nishiriki changamoto zake kwa kumshauri hivyo anambie na sitamtangaza kwa yale atakayoniambia. Alikubali.
Aisee, kumbe ni ndoa inamsumbua. Mumewe anaweza kuwepo pale mtaani ila kurudi kulala nyumbani ndo shida. Anabadilisha tu nyumba za kulala yaani kwa michepuko. Aliwaorodhesha kama wanne hivi japo sikuwafahamu. Mbaya zaidi hakuna mahitaji ya msingi anayotoa, hata hela ya kula tu hakuna. Kinachombeba ni lile banda la mchele ambalo mtaji wake aliupata kwa mkopo wa kikundi na anafanya marejesho. Aliongea hadi analia. Nilimbeleza hadi alinyamaza. Nilimpa maneno ya kumjenga kisaikolojia kwa kumwambia akiendelea kumfikiria mume atapoteza mwelekeo hadi atashindwa kutunza watoto na kurejesha mkopo. Nilimwambia tazame mbele kwenye biashara yake, aikuze kwa kuongeza bidhaa rahisi kama matunda na mafuta ya kula na chochote kinachoweza kupatikana kwa urahisi akakiuza. Kifupi nilimfunda hadi alinishangaa. Kikubwa aliniunga mkono na kuonekana kupata mood mpya. Baada ya mazungumzo nilimpa zawadi nilizomwandalia. Hakukataa, alishangaa na kupokea kwa shukrani.
Siku ilipita bila kumgeuzia kibao.
Alikoenda alizidisha kasi ya kutuma sms hadi niliona kero. Lakini sikumwonesha kama sipendi sana kuchati. Alianza kunieleza mwenendo wa biashara yake. Alianza kuimarika kisaikolojia na kibiashara. Nilimpongeza na kumpa moyo zaidi, naye akakazanana sana. Nikienda kununua mchele alinipa bure, nilipokea kila alichonipa.
Sasa hakuogopa tena kusema lolote kwangu, alinieleza hali ya ndoa yake na matendo ya mumewe. Nilimkazania kupuuza matendo ya mumewe. Cha ajabu nilipomwalika tena geto alikuja kwa wakati. Safari hii niliishia kumsifu na kumwambia naona anabadilika kiafya. Na ni kweli alionekana kupata afya na uchangamfu kuliko nilivyomwona mara ya kwanza. Niliendelea kumshauri. Alionekana kuniamini na kunitii. Muda huu wote sikuwahi kuomba mzigo.
Ilikuja kutokea mumewe alisafiri kwenda kutafuta ziwa Rukwa. Alifurahi sana kubaki pekeyake. Akaanza utaratibu wa kuniletea chakula cha jioni geto. Hapo ndipo alipokosea. Siku moja alipokuja nilimla yeye badala ya chakula kisha nikala chakula chake, yaani aliliwa mpishi na mapishi yake. Hakuonekana kuleta upinzani wa kusita zaidi ya kutoa ushirikiano. Nicho chanzo cha kufika hapa tulipofika. Ni mwaka wa 4 sasa.
Tukio ambalo mumewe hushangaa ni mkewe kutolialia tena, ananawiri na anaimarika kiuchumi. Aliwahi mwulize tetesi alizosikia, mke alikataa. Akabaki kurudia kumwuliza mara kwa mara bila majibu sahihi. Ameweka watu kufuatilia bila mafanikio. Imefikia mahali ni kama amekata tamaa kufutilia. Shida ni wapi tunakutana na muda gani tunakutana. Hii siwezi kueleza hapa ππ.
Sikushauri kutembea na wake za watu. Iwe mwiko kwa kila mwanaume. Hili ni kosa kubwa sana. Nasisitiza achana na mke wa mtu, ni kifo unachokoza.